Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akionesha baadhi ya mashine za mionzi 10 zilizonunuliwa na Serikali
zenye thamani ya shilingi bilioni 1.7 na kusambazwa kwenye Hospitali za
Rufaa za Mikoa.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana Dkt.Mashack
Shimwela,akiongea na waandishi wa habari baada ya kupokea mashine
hizo(picha zote na Wizara ya Afya
Waziri Ummy akiongea na vyombo vya habari wakati wa kupokea mashine hizo
za mionzi (digital X-ray) ambazo zitaboresha huduma za afya nchini
hususani za uchunguzi wa mionzi
SERIKALI YANUNUA MA SHINE ZA MIONZI ZENYE THAMANI YA BILIONI 1.7
Na.WAMJW, Dar es Salaam
Serikali
kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto
imenunua mashine za Mionzi (digital X-ray) zipatazo kumi zenye thamani
ya shilingi bilioni 1.7.
Hayo yamesemwa leo na
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
wakati akipokea mashine hizo kwenye Bohari ya Dawa(MSD) jijini hapa.
Waziri
Ummy amesema kuwa Serikaki inaendelea kutoa kipaumbele katika kuboresha
huduma za afya nchini ikiwa ni lengo la kuhakikisha huduma za afya
zinawafikia watanzainia wote karibu na maeneo wanayoishi.
"Maendeleo
ya Taifa letu la Tanzania yataletwa na wananchi wenye afya na wenye
uwezo wa kuzalisha mali,hivyo tunaboresha na kuimarisha huduma za tiba
na uchunguzi wa magonjwa katika hospitali zetu kuwa na vifaa vya kisasa
zaidi na kuondokana na utaratibu wa kupeleka wagonjwa nje ya
nchi".Alisema,Waziri Ummy Mwalimu.
Alisema
mashine hizo zitapelekwa kwenye hospitali za rufaa za mikoa 10 ambazo
X-ray za zamani zimekwisha muda wake na zimekua zikiharibika mara kwa
mara.
Alizitaja hospitali hizo ni Amana, Bukoba, Katavi,Morogoro,Njombe,Ruvuma, Simiyu na Singida pamoja na hospitali za Wilaya ya Magu na Nzega.
Aidha,Waziri
Ummy alisema katika bajeti ya mwaka 2018/2019, Wizara yake imepanga
kununua mashine za mionzi nyingine zipatazo ishirini na nne(24) zenye
thamani ya shilingi bilioni 4.1 ambazo zitapelekwa kwenye hospitali za
rufaa za Mikoa na Wilaya ambazo hazina au zina X-ray za kizamani au
chakavu.
Akizungumza kwa niaba ya Waganga Wakuu
wa hospitali zinazopelekwa mashine hizo,Mganga Mkuu wa Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Amana Dkt.Mashack Shimwela alisema ujio wa mashine hizo
za kisasa zitasaidia kupunguza gharama za uendeshaji wa uchunguzi za
mionzi pia utunzaji wa mazingira tofauti na aina zilizokuwa zikitumika
mwanzo
Aidha,alisema mashine hizo zina ubora wa
picha pia ina mifumo ya Tehama ambayo ni rahisi kusomwa hata nje ya
hospitali husika endapo hakuna msoma picha
0 on: " SERIKALI YANUNUA MA SHINE ZA MIONZI ZENYE THAMANI YA BILIONI 1.7"