Baadhi ya wakazi wa Dodoma waliofika katika viwanja vya Nyerere Square wakisubiri kupata huduma ya afya ya macho na
magonjwa yasiyoyakuambukiza wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Afya ya
Macho yaliyofanyika mkoani humo leo.
NA WAMJW-DODOMA
Wagonjwa 300
waliobainika kuwa na matatizo ya macho wamefanyiwa upasuaji na kurejeshewa hali
ya kuona vizuri ndani ya siku 5 ambapo watu wenye matatizo ya macho takribani 700
wamefanyiwa uchunguzi.
Hayo
yamesemwa na Kaimu Meneja wa Mpango wa Huduma za Macho kutoka Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Bernadetha Shilio wakati wa
kilele cha maadhimisho ya siku ya siku ya afya ya macho duniani kilichofanyika
mapema leo katika viwanja vya Nyerere jijini Dodoma.
“Siku ya
afya ya macho duniani ina lengo kuu la kuhamasisha utekelezaji wa dira ya
kimataifa ya kutokomeza upofu unaozuilika ifikapo mwaka 2020, na kutathmini
haki ya kuona kwa wote ambapo mwaka 2003 serikali ya Tanzania iliungana na
mataifa mengine duniani katika kutekeleza azimio hilo”. Alisema Dkt. Shilio.
Dkt. Shilio
amesema Serikali ya Tanzania inashirikiana na mataifa mengine duniani
kuadhimisha siku ya afya ya macho ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa jamii,
kutoa huduma za uchunguzi wa macho pamoja na kufanya upasuaji kwa wagonjwa ambao
watabainika kuwa na matatizo.
Pia Dkt.
Shilio ameiasa jamii ya kitanzania kuzingatia kanuni sahihi za utunzaji wa
macho ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza na kusababisha uono hafifu na
kupelekea upofu.
“Matumizi
ya rangi na kope bandia kwenye ukingo wa macho, kuvaa miwani bila kupima,
kutumia dawa za mgonjwa mwingine wa macho bila ushauri wa daktari, kutokula
vyakula bora vyenye virutubisho na kutokua na tabia ya kupima macho angalau
mara moja kwa mwaka vimetajwa kuwa visababishi vikubwa vya kuathiri afya ya
macho” alisema Dkt. Shilio.
Aidha, Dkt.
Shilio amesema sambamba na huduma za macho pia kumekua na huduma za uchunguzi
na ushauri kwa magonjwa yasiyoambukiza jijini Dodoma, jumla ya watu 400
walifanyiwa vipimo vya sukari, shinikizo la damu na kiwango cha unene. Ambapo
asilimia 3 wamekutwa na kiwango cha juu cha sukari, asilimia 47 wamekutwa na
shinikizo la juu la damu na asilimia 50 wamekutwa na unene uliopitiliza
kiwango.
Kwa upande
wake Mgonjwa aliyepata huduma za macho Jijini Dodoma Bi.Veronica Maganga
ameishauri serikali kuendelea kutoa elimu, kusogeza na kutoa huduma za macho na
uchunguzi wa magonjwa mengine karibu na wananchi ili kuzuia magonjwa yanayoweza
kuleta madhara iwapo hayatachunguzwa mapema na kutoa matibabu sahihi.
“Tunaishukuru
sana Serikali kwa kutuletea huduma hii kwani wengi tumepata matumaini ya kuona
tena kwa uono mkubwa ila wangefanya huduma hii iwe endelevu mpaka vijijini ili
kuwanusuru wenye matatizo ya macho” alisema Bi. Veronica.
|
0 on: "WAGONJWA WA MACHO 300 NCHINI WAFANYIWA UPASUAJI NDANI YA SIKU TANO"