JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
TANGAZO KWA UMMA
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
(Afya) anawatangazia watumishi wote waliopata udahili wa kusoma masomo
ya Shahada ya Uzamili (Masters Degree) katika fani za Afya kwa mwaka
2018/2019, kwamba Wizara inaanza kupokea maombi ya Ufadhili kwa mwaka
2018/2019. Maombi haya yatawasilishwa kwa njia ya kielektroniki kwa
kujisajili kupitia fomu zilizopo kwenye tovuti ya Wizara www.moh.go.tz (https://sponsorship.moh.go.tz ).Maombi
yatakayofanyiwa kazi ni yale yaliyowasilishwa kwa njia ya mfumo huu tu,
hivyo waombaji waliowasilisha maombi yao kabla ya tangazo hili
wanapaswa kurudia kuomba kupitia utaratibu huu.
Ufadhili huu ni kwa ajili ya kulipiwa ada ya mafunzo (Tuition fee), pamoja na posho ya utafiti (Dissertation allowance).
Vigezo vitakavyotumika kuchagua ni hivi vifuatavyo :
Kuwasilishwa kwa maombi rasmi ya ufadhili kwa njia ya mfumo (online application)
Mwombaji kuwa Raia wa Tanzania.
Awe amedahiliwa Chuoni kuanza masomo kwa mwaka wa kwanza 2018/2019
Kipaumbele kitatolewa kwa:
Watumishi
wa Serikali waliomo kwenye sekta ya Afya wanaofanya kazi katika vituo
vilivyoko Wilayani/Mikoani hususani katika Hospitali za Rufaa za Mikoa
ambao baada ya mafunzo watarudi kuendelea kufanya kazi katika vituo vyao
vya awali, au watapangiwa vituo vya kazi sehemu nyingine yeyote nchini
Waombaji
waliodahiliwa katika fani ambazo ni za msingi katika utoaji wa huduma
za rufaa katika Hospitali za Rufaa za Mikoa. Nyanja hizo ni
Anaesthisiology, Surgery, Neurosurgery, Obstetrics and Gynaecology,
Orthopaedics Surgery, Emergency Medicine, Paediatrics, Internal
Medicine, Critical Care in Nursing na Midwifery and Womens Health,
Radio-pharmacy,Epidemiology and Lab.Management
Waombaji
waliodahiliwa katika nyanja za Ubingwa/Ubingwa wa Juu (Specialities na
Super-specialities) zenye umuhimu mkubwa katika Hospitali za Kitaifa
(kama Cardiology, Nephrology,Opthalmology, Radiography na Oncology)
ili kujenga uwezo wa ndani ya nchi katika jitihada za kupunguza wagonjwa
wa rufaa wanaotibiwa nje ya nchi.
Aidha, mwombaji atatakiwa aambatanishe nyaraka zifuatazo wakati wa kufanya maombi:
Barua ya ruhusa ya masomo kutoka kwa mwajiri wake
Barua ya udahili kutoka chuoni
Cheti cha taaluma
Cheti cha kuzaliwa
Mwisho wa kupokea maombi haya ni tarehe 10/11/2018.
Imetolewa na:
Katibu Mkuu,
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Chuo Kikuu Dodoma,
Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Maendeleo ya Jamii
S.L.P 743
DODOMA
11/10/20
0 on: "TAARIFA KWA UMMA"