Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya Wabunge wa kamati ya Huduma za Jamii
na Wadau wa Masuala ya Afya (hawapo kwenye picha) katika uzinduzi wa
taarifa ya utafiti wa Viashiria vya Malaria nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya
TAKWIMU Dkt. Albina Chuwa akionesha Kitabu cha Taarifa ya Takwimu za Viashiria vya Ugonjwa wa Malaria mbele ya Wabunge wa Kamati ya Huduma za Jamii na Wadau wa Masuala ya Afya wakati wa uzinduzi wa
taarifa ya utafiti wa Viashiria vya Malaria nchini.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakioneshana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya TAKWIMU Dkt. Albina Chuwa (wakatikati).
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa taarifa ya utafiti wa
Viashiria vya Malaria nchini uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Wabunge wa Kamati ya Huduma za Jamii na Wadau wa Masuala ya Afya
wakifuatilia taarifa ya Utafiti ya Viashiria vya ugonjwa wa Malaria
nchini iliyokuwa ikisomwa na Mgeni rasmi Waziri wa Afya Mhe. Ummy
Mwalimu (hayupo kwenye Picha) jijini Dar es salaam.
Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa taarifa
ya utafiti wa Viashiria vya Malaria nchini.
MAAFISA AFYA WATAKIWA KUSIMAMIA USAFI WA MAZINGIRA ILI KUTOKOMEZA MALARIA
Na WAMJW – Dar Es Salaam.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
amewaagiza Maafisa Afya nchini kusimamia kwa ukamilifu usafi wa
mazingira katika jamii ili kutokomeza ugonjwa wa Malaria.
Waziri
Ummy ametoa agizo hilo leo Oktoba 22, 2018 wakati akizindua Taarifa ya
Utafiti wa Viashiria vya Ugonjwa wa Malaria wa Mwaka 2017 katika Ukumbi
wa Karimjee jijini Dar Es Salaam
“Nawaagiza Maafisa
Afya, badala ya kupoteza muda mwingi wa kukagua migahawa, bucha za
nyama na sehemu ambazo wanajua zinaleta fedha, tunataka pia wajikite
katika kusimamia usafi wa mazingira katika Kata, Vijiji na Mitaa
yetu”Alisema Mhe. Ummy.
Katika kuhakikisha hali ya
usafi wa mazingira inakuwa endelevu, Waziri Ummy ameagiza Mabalaza yote
ya Halmashauri nchini kuweka Sheria na adhabu kali kwa wote ambao
wamekuwa wagumu katika kushiriki katika usafi wa mazingira huku Waganga
Wakuu wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanasimamia vyema
utekelezaji wa kanuni na sheria za afya na usafi wa mazingira jambo
ambalo litaibua chachu ya ushindi katika mapambano dhidi ya Ugonjwa wa
Malaria.
“Niyatake
Mabalaza ya Hamashauri kuweka hatua kali, sheria kali na adhabu kali kwa
wote ambao hawashiriki katika usafi wa mazingira” alisema Waziri Ummy.
Licha
ya hivyo Waziri Ummy alisema kuwa Serikali kupitia Wizara inaendelea
kutekeleza Mpango endelevu wa ugawaji vya ndarua kupitia wanafunzi wa
shule za msingi, kupitia Kliniki za wajawazito na watoto, ambayo
hujulikana kama Chandarua Kliniki huku hadi sasa jumla ya vyandarua
milioni 31 vimeshagawiwa nchini kote.
Aidha, Waziri
Ummy alisema kuwa Matokeo ya mpango endele u wa ugawaji wa vyandarua
yameonesha kuwa asilimia 78 ya kaya nchini Tanzania zinamiliki angalau
chandarua kimoja chenye dawa, Katika utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto
na Viashiria vya Malaria wa mwaka 2015-16, ni asilimia 66 tu za kaya
zilikuwa zinamiliki angalau chandarua kimoja chenye dawa huku Umiliki wa
vyandarua vyenye dawa ni wa kiwango cha juu kwa kaya za mijini
(asilimia 81) ikilinganishwa na kaya za vijijini (asilimia 77).
Kwa
upande mwingine Waziri Ummy alitaja Halmashauri zenye maambukizi ya
kiwango cha juu ni pamoja na Kakonko 30.8%, Kasulu DC 27.6%, Kibondo DC
25.8%, Uvinza 25.4%, Kigoma DC 25.1%, Buhigwe 24%, Geita DC 22.4%,
Nanyamba TC 19.5%, Muleba DC 19.4%, Mtwara DC 19.1%, huku Halmashauri
zenye maambukizi ya kiwango cha chini ya asilimia 0.1 ni Mbulu TC,
Mbulu DC, Hanang, Hai, Siha, Moshi MC, Mwanga, Kondoa TC, Meru DC,
Arusha CC, Arusha DC, Munduli, Ngorongoro, Rombo DC
MWISHO
0 on: "MAAFISA AFYA WATAKIWA KUSIMAMIA USAFI WA MAZINGIRA ILI KUTOKOMEZA MALARIA"