Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (aliyesimama) akiwasilisha taarifa
ya utekelezaji wa shughuli za mfuko huo kwenye kamati ya kudumu ya Bunge ya
Huduma na Maendeleo ya Jamii Bungeni jijini Dodoma.
Na.WAMJW,Bungeni, Dodoma
Idadi ya wanachama wachangiaji wa mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya imeongezeka kutoka wanachama 164,708 waliokuwa wameandikishwa mwaka 2001/2002 hadi wanachama 873,012 mwezi
Septemba 2018.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za mfuko
huo kwenye kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Bungeni
jijini Dodoma.
“Ongezeko hili limetokana na kanuni na misingi inayotumika katika kuendesha utaratibu wa
mfuko huu ikiwa ni pamoja na uchangiaji wenye usawa kwa kuzingatia viwango vya
mshahara,usawa katika kupata huduma na ushiriki wa Serikali katika usimamizi
kwa faida ya wanachama” alisema Waziri Ummy.
Waziri Ummy amesema kuwa kwa upande wa Mfuko wa Afya ya Jamii
(CHF), jumla ya kaya zilizojiunga hadi Septemba mwaka huu ni 2,220,953 ikiwa ni
sawa na wanufaika wapatao 13,506,330 sawa na asilimia 25 ya watanzania wote’
kwa hiyo mifuko hii yote inatoa huduma kwa watu 17,656,697 sawa na asilimia 33
ya watanzania wote kwa mujibu wa idadi
ya makadirio ya watanzania kwa sasa.
Idadi ya wanufaika imeongezeka kutoka 691,774 mwaka 2001/2002 hadi wanufaika 4,150,367 sawa
na asilimia 8 ya watanzania wote” alisema Waziri Ummy.
Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa mpaka sasa idadi ya wanachama
wengi waliojiunga asilimia 67 ni
watumishi wa umma ambao wanajiunga kwa mujibu wa sharia.
Hata hivyo Waziri Ummy alisema mfuko unaendelea kutoa elimu na
kubuni vifurushi mbalimbali vitakavyovutia wananchi wengi kujiunga na
kufaidika na mfuko ambapo utawawezesha
wanachama wengi zaidi kujiunga hasa wale wa sekta isiyo rasmi na kujiwekea
malengo ya kuwafikia watanzia asilimia 50 mwaka 2020.
“Mfuko umekamilisha uandaaji wa vifurushi vya michango na
mafao kulingana na uwezo wa wananchi kulipia bima ya afya,suala hili lipo katika hatua za
mwisho kabla ya kuanza kwa utekelezaji”. Alisisitiza Waziri Ummy.
Waziri Ummy amesema kuwa mpango huo utamwezesha mwananchi
kuchagua vifurushi vya aina mbalimbaliu vya huduma anayoitaka
kwa utaratibu utakaojulikana kama ‘JIPIMIE’ na wanachama watalipa kidogo
kidogo kwa utaratibu ujulikanao kama ‘DUNDULIZA’ ambao tayari umeshakamilika.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kwenye kamati ya kudumu ya
Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba amesema kuwa NHIF
wanatakiwa kuweka mfumo wa kutoa huduma za bima ya afya kwa mashirika makubwa
ya hapa nchi na yale ya nje kwa kuwauliza
huduma zipi wangependa kuhudumiwa katika hospitali za hapa nchini hususan zile za binafsi na hivyo kuweza
kuongeza idadi kubwa ya wateja watakaohudumiwa na NHIF.
Naye Mkurugenzi wa NHIF Bw. Bernad Konga akijibu maswali ya
wajumbe wa kamati hiyo alisema kwamba NHIF imekubali kuboresha huduma zao na
hivyo wapo tayari kuanza huduma za vifurushi za
‘JIPIMIE’ mara moja ili wananchi
waweze kupata huduma za afya kulingana na vipato vyao.
Aidha, alisema hivi sasa wameajiri madaktari wapatao kumi na
nane na kuwaweka kwenye hospitali kubwa
za Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutatua changamototo za wateja wa huduma
za bima hiyo zikiwemo za kunyanyapaliwa
pamoja na kukagua fomu zinazojazwa na wataalam wa hospitali hizo ili
kupunguza malalamiko ya wateja wa huduma za bima ya NHIF na kuahidi wataongeza hospitali
zingine awamu inayofuata
0 on: "IDADI YA WANACHAMA WACHANGIAJI WA MFUKO WA BIMA YA AFYA NCHINI YAONGEZEKA."