Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
amwalimu akikagua vifaa vya moja ya kati ya wagonjwa waliopata Rufaa ya
kwenda kutibiwa katika Hospitali ya St. Francis pindi alipofanya ziara
ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika kituo cha Afya cha
Kibaoni.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu akimjulia hali mtoto aliefika na mama yake kupata huduma katika
kituo cha Kibaoni.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya viongozi wa Mkoa wa
Morogoro walioongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ifakara James Lihunyo (hayupo
kwenye picha)
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikagua cheti cha mgonjwa katika kituo cha
Afya cha Kibaoni wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji
huduma kisha kuelekea Hospitali ya Rufaa ya St. Francis.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu akimjulia hali mtoto aliefika na mama yake kupata huduma katika
kituo cha Kibaoni.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jisnsia, Wazee na
Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akieleza umuhimu wa Bima ya Afya kwa watoto kwa
mmoja kati ya wamama waliofika kupata huduma za Afya katika kituo cha
Afya cha Kibaoni.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa maelekezo kwa Baba Askofu wa jimbo la
Ifakara Salutaris Libenaambae baada ya kikao cha kuboresha hali ya
utoaji huduma za Afya katika Hospitali hiyo.
Upande wa mbele wa Hospitali ya Rufaa ya St. Francis.
WAZIRI UMMY AUAGIZA UONGOZI WA HOSPITALI YA ST FRANCIS KUSHUSHA BEI ZA MATIBABU MARA MOJA.
Na WAMJW - IFAKARA
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
ameuagiza uongozi wa Hospitali ya Dini ya St.Francis kupunguza gharama
za matibabu kwa wananchi ndani ya mwezi mmoja kabla hajarudi kufanya
ukaguzi wa mara ya pili.
Ameyasema
hayo wakati akiwa katika ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za afya
katika Hospitali ya St Francis iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Ifakara
Mkoa wa Morogoro kufuatia taarifa isiyoridhisha juu ya gharama za
matibabu iyoripotiwa siku ya Octoba 3 na Televisheni ya Taifa (TBC).
Waziri
Ummy alisema kwamba, Serikali inatoa Jumla ya Watumishi 243 sawa na
Asilimia 68% katika Hospitali hiyo, lengo ni kuwasaidia wananchi wa
kipato cha chini kupata huduma za bora za afya na zenye unafuu ikiwa ni
moja kati ya ahadi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli wakati anaingia madarakani.
"Kati
ya Watumishi 352, watumishi 219 wanalipwa mshahara na Serikali Kuu,
ambapo kila mwezi tunalipa shilingi milioni 153.7, bila kuhesabu gharama
za watumishi 12 walioshikizwa kutoka Wizara ya Afya, Watumishi 12
kutoka Halmashauri ya Kilombero, Katibu tawala Morogoro ameleta
watumishi 2, jumla watumishi 243, ambao ni sawa na Asilimia 68%
wanalipwa mshahara kutoka Serikali kwa Asilimia 100%". Alisema Mhe. Ummy
Mwalimu.
Waziri Ummy
aliendelea kusema kuwa mwaka wa bajeti 2015/2016 Serikali ilipeleka dawa
zenye thamani ya shilingi Millioni 119.5, bajeti ya mwaka 2016/2017
shilingi milioni 177.9 huku kwa mwaka 2017/2018 dawa zenye thamani ya
shilingi milioni 118.7 zilinunuliwa hospitalini hapo.
Kwa
upande mwingine Waziri Ummy alisema kuwa mwongozo wa Wizara ya Afya,
unazitaka Hospitali zote kuhakikisha kuwa wanawake wajawazito, wazee
wasio na uwezo na watoto walio chini ya umri wa miaka mitano kupata
huduma za matibabu bila malipo.
Mbali
na hayo Waziri Ummy alitoa rai kwa wananchi wa Mkoa wa Morogoro
kujiunga na mifuko ya Bima ya Afya bila kuwasahau watoto walio chini ya
umri wa miaka 18 ambao hupata bima ya afya kwa shilingi 50,400/=
"Wakati
umefika wa Watanzania kujenga utamaduni wa kuwa na uhakika wa matibabu
kabla ya kuugua, na uhakika huo ni wa kupitia Bima ya Afya", alihimiza
Waziri Ummy kwa msisitizo.
Waziri
Ummy, aliendelea kusema kuwa, Serikali inaelekea kutunga sheria ambayo
itamlazimu kila Mtanzania kupata Bima ya Afya, ili aweze kupata huduma
za matibabu ya Afya bila kikwazo chochote cha fedha.
Naye
Mbunge wa Jimbo la Kilombero Mhe. Peter Ambrose Lijualikali amemuomba
Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu kuikumbuka Halmashauri ya Wilaya ya
Kilombero kwa kujenga Hospitali ya Wilaya, jambo litaloimarisha hali ya
utoaji huduma za Afya kwa wananchi.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Hospitali ya St. Fransis, Baba Askofu Salutaris Libena
ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kufika hospitali hapo na
kuahidi kutekeleza maelekezo yote ambayo yametolewa na Serikali.
"
Tunaahidi kwamba tumeelewa na tutatekeleza maelekezo yote, katika lengo
la kuboresha huduma za Afya kwa wananchi ", alisema Baba Askofu Libena.
0 on: "WAZIRI UMMY AUAGIZA UONGOZI WA HOSPITALI YA ST. FRANCIS KUSHUSHA BEI ZA MATIBABU MARA MOJA."