Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akisisitiza jambo mbele ya Wadau mbali mbali wa
masuala ya Afya baada ya kufungua mkutano wa masuala mbali mbali ya Afya
uliofanyika jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akifungua Mkutano wa Wadau mbali mbali wa
masuala ya Afya
uliofanyika jijini Dar es salaam.
Naibu Katibu Mkuu anaeshughulikia masuala ya Afya TAMISEMI Dkt. Zainabu
Chaula akiongea na Wadau mbali mbali wa masuala ya Afya katika mkutano
uliofanyika jijini Dar es salaam.
Kiongozi Mkuu wa Mkutano wa Masuala ya Afya, hususani
katika mfumo wa upatikanaji na usambazaji wa Dawa, Vifaa tiba na
Vitendanishi Bw. Mavelle Tukai akiwakaribisha Wadau wa masuala ya Afya waliofika katika Mkutano huo uliofanyika jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akiongea jambo na Mkurugenzi wa Bohari kuu ya Dawa
nchini Bw. Laurean Bwanakunu, katikati ni Afisa mfamasia kutoka Wizara
ya Afya Siana Mapunjo.
Wadau mbali mbali wa masuala ya Afya wakifuatilia kwa makini mgeni rasmi
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk.
Faustine Ndugulile (hayupo kwenye picha)
DKT. NDUGULILE AAGIZA KUBORESHWA KWA MFUMO WA UKUSANYAJI TAKWIMU NCHINI.
Na WAMJW - Dar es salaam.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile ameagiza kuboreshwa kwa mfumo wa ukusanyaji wa
Takwimu nchini utaosaidia upatikanaji wa takwimu sahihi na zinazifanana
katika taasisi zote.
Ameyasema
hayo mapema wakati akifungua Mkutano wa masuala ya Afya, hususani
katika mfumo wa upatikanaji na usambazaji wa Dawa, Vifaa tiba na
Vitendanishi leo jijini Dar es salaam.
Dkt.
Ndugulile alisema kuwa Serikali inataka kuona mifumo yote ya ukisanyaji
Takwimu inaboreshwa mara moja huku akisisitiza kuwa mifumo hiyo ni
lazima iweze kuwasiliana jambo litalosaidia kupata Takwimu sahihi na
zinazofanana kwa mifumo yote.
"Tunataka
kuona mnaboresha mfumo wa ukusanyaji Takwimu, Takwimu bado ni
changamoto kubwa sana katika utoaji wa huduma za Afya na katika mfumo
mzima wa usambazaji, na ni lazima kuhakikisha kuwa mifumo hii
inawasiliana na inakuwa endelevu" Alisema Dkt. Ndugulile.
Kwa
upande mwingine Dkt. Ndugulile amewaonya watumishi wa Serikali hususani
kutoka Wizara ya Afya wanaokwamisha mawazo endelevu yanayopelekea
kupiga hatua kwa Sekta ya Afya, na kuahidi kuwachukulia hatua endapo
yeyote atabainika kufanya hivo.
"
Muda wowote, mtu yeyote mwenye Mawazo mazuri na Endelevu kwaajili ya
Maendeleo ya Sekta yetu ya Afya, njoo unione Mimi au Waziri wangu,
milango yetu ipo wazi, wengine sisi hatuna urasimu, Serikali hii ya
awamu ya tano haitaki ubabaishaji" Alisema Dkt Ndugulile.
Aidha,
amewaagiza Waganga Wafawidhi wote nchini kuhakikisha wanaandaa orodha
ya Dawa zilizopo kila mwanzo wa wiki ili kusaidia kufahamu orodha ya
Dawa zilizopo na zinazohitajika kwa kipindi hicho, huku akisisitiza
kumchukulia hatua yeyote ataebainika.
"Tumepata
taarifa baadhi ya makampuni ya Dawa yanapita katika Hospitali zetu,
hususani Hospitali kubwa na wanawarubuni Madaktari wetu kuandika kwa MSD orodha ya Dawa ambazo hazipo katika mwongozo wetu wa Serikali,
tutachukua hatua Kali" Alisema Dkt Ndugulile.
Mbali
na hayo Dkt Ndugulile amepiga marufuku Madaktari wote nchini kuandika
Dawa kwa kutumia majina ya bishara na kuwataka kutumia majina ya asili
ya Dawa hizo.
"Jukumu la
Serikali sio kufanya Bishara ya kumtangazia mtu, mfano Panaldo sio jina
lake kitaalamu, ukienda baadhi ya nchi unaweza usikute Panaldo jina lake
halisi ni Parasetamo na ndio linatakiwa litumike" Alisema Dkt
Ndugulile.
0 on: "DKT. NDUGULILE AAGIZA KUBORESHWA KWA MFUMO WA UKUSANYAJI TAKWIMU NCHINI"