Wananchi kutoka sehemu mbalimbali za mkoa wa
Dodoma wakiwa wamejipanga katika mstari ili kupata huduma za macho katika
maadhimisho ya wiki ya afya ya macho duniani yanayoendelea katika viwanja vya
Nyerere mkoani humo.
NA WAMJW-DODOMA
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya,
imewaasa Watanzania kujijengea tabia ya kupima macho mara kwa mara ili kuweza
kuepuka aina mbalimbali za magonjwa ya macho ikiwemo vikope.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mganga Mkuu wa
Serikali Dkt. Eliud Eliakimu wakati wa kufungua hafla ya kuelekea siku ya Afya
ya Macho Duniani ambayo huadhimishwa kila alhamisi ya Pili ya mwezi Octoba.
“Asilimia kubwa ya magonjwa ya macho
yanatibika ikiwemo upeo mdogo wa macho kuona
ambao yanazuilika kwa miwani
endapo mtu akiwahi katika kituo cha kutolea huduma za Afya na
akigundulika ana tatizo la macho basi atapata matibabu mapema”alisema Dkt.
Eliakimu.
Aidha, Dkt. Eliakimu alisema kuwa kwa
Tanzania watu wasioona kabisa ni asilimia moja sawa na watu laki 5.7 huku watu
wenye matatizo mbalimbali ya macho wanakadiriwa kuwa mara tatu ya wasioona
kabisa sawasawa na mil.7.
Kwa mujibu wa Dkt. Eliudi amesema kuwa
takwimu zinaonesha kwamba ugonjwa wa macho umepungua kutoka asilimia 4.6 mwaka
1990 na kufikia asilimia 3.4 mwaka 2015 kutokana na hamasa ya juu ya upimaji
toka kwa wananchi.
Kwa upande wake Kaimu Meneja Mpango wa
Huduma za Macho Nchini kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Dkt. Benadertha Chilio amesema kuwa tatizo la macho linaloongoza
nchini ni mtoto wa jicho ambapo wagonjwa wanafikia kwa asilimia 50 na wengi wao
ni wanawake.
“Watanzania wanatakiwa kuacha matumizi
ya mitishamba na badala yake wanatikwa kuhudhuria hospitali pindi wanapohisi
wanamatatizo ya macho kwani matumizi ya mitishamba kunaweza kusababisha makovu
katika kioo cha jicho hivyo kunaweza kusababisha jicho kutofanya kazi kabisa”
alisema Dkt. Chilio.
Aidha,Dkt. Chilio amewataka
wanaohitaji tiba ya kuvaa miwani kwa ajili ya kuona vizuri waende hospitali
zilizosajiliwa wapate vipimo stahiki na kupewa miwani kutokana na uwezo wao wa
kuona na sio kupata huduma hizo kwenye vituo visivyosajiliwa.
Naye Mkanga Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt.
Charles Kiologwe amewataka wakazi wa Dodoma kujitokeza kupata huduma za macho
ili kutokomeza ugonjwa huo mkoani humo ili
kuendelea katika shughuli za kujenga
uchumi wa viwanda.
“Nawaomba wakazi wenzangu wa Dodoma
tujutokeze kwa wingi kupata huduma za macho ili kulinda afya zetu pamoja na
kuondoa ule usemi uliopo vichwani kwa watu wengi kwamba kila mgonjwa wa macho
anatokea Dodoma” alisema Dkt. Kiologwe.
|
0 on: "WATANZANIA WAASWA KUPIMA MACHO MARA KWA MARA."