Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa
nchini (MSD) Bwa. Laurean Bwanakunu akichangia mada wakati wa kikao cha kamati
ya Bunge ya Huduma za jamii nchini kinachoendelea katika ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, aliyekaa kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,
Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile.
SERIKALI
kupitia Wizara ya Afya imeainisha dawa aina 135 kama dawa muhimu na za
kipaumbele cha wizara kwa lengo la
kuhakikisha kuwa zinapatikana nyakati
zote katika bohari zote za kanda za MSD.
Hayo
yameelezwa leo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Janii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy
Mwalimu wakati akitoa taarifa ya
utendaji ya Bohari Kuu ya Dawa nchini(MSD)
aliyowasilisha katika kamati ya kudumu ya Bunge huduma na maendeleo ya
jamii jijini Dodoma.
Waziri
Ummy alisema tathimini ya upatikanaji wa dawa hizo ni wa hadi mwezi Julai 2018 ambapo ni sawa na asilimia 93 hivyo Wizara
yake imeitaka MSD kuongeza idadi ya dawa muhimu 177 na kufikia
dawa za kipaumbele 312 ambapo upatikanaji wa dawa hizo ni asilimia 73
kufikia robo mwaka ya kwanza ya mwaka wa fedha 2018/2019.
“Hali ya
upatikanaji dawa muhimu umeimarika
kuanzia mwaka 2016/2017 na kufikia
asilimia 93 nchi nzima katika mwaka
2017/2018 na hivyo kuweza
kufanikiwa katika maeneo mengi na
kufikisha dawa moja kwa moja katika
vituo vya kutolea huduma za afya nchi
nzima”.Alisema Waziri Ummy Mwalimu.
Aidha,
Waziri Ummy alisema MSD imeweza kusambaza dawa moja kwa moja hadi vituo vya
kutolea huduma za afya vinavyofikia 5,432 nchi nzima kwa kutumia magari 215 na hivyo kusambaza dawa zenye thamani za
shilingi bilionini 600 kwa mwaka kupitia mfumo wa ugavi ulio enea nchi nzima.
Hata hivyo
Waziri Ummy amesema kuwa hivi sasa MSD inapeleka dawa mara 6 kwa mwaka na pale
kwenye mahitaji ya dharura tofauti na zamani ambapo ilikua inapeleka dawa mara
nne kwa mwaka.
Mbali na
hayo Waziri Ummy alisema Bohari ya dawa imeendelea kuimarika kifedha katika
kipindi cha miaka mitano iliyopita hususan katika mwaka wa fedha 2017/2018
ambapo Serikali iliongeza bajeti ya dawa, vifaa na vifaa tiba na kuweza kutoa kiasi cha shilingi bilioni
80.1 na kwa mwaka wa bajeti 2018/2019
kwa robo hii ya mwaka imepokea shilingi bilioni 20.
Kwa upande
wake Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile amewataka wafamasia wote wa Hospitali na vituo vya afya
kupeleka orodha ya dawa zilizopo kwenye
stoo kwa madaktari kila mwanzo wa wiki.
“Wafamasia
wote wa Hospitali na zahanati za Serikali wanatakiwa kuwapelekea madaktari
orodha ya dawa zilizopo kwenye stoo ili kama dawa ya ugonjwa Fulani haipo
Daktari awe na uwezo wa kuandika dawa mbadala kwa mgonjwa” amesema Dkt.
Ndugulile.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya dawa nchini Bw. Laurean Bwanakunu amesema kuwa
katika kuhakikisha upatikanaji wa dawa unadumu nchini wapo katika hatua za
mwisho za kukamilisha ubia kati ya Serikali na Sekta binafsi kujenga kiwanda
cha dawa nchini.
“Tunatarajia mpaka kufikia Machi 2019 kukamilisha ubia kati ya Serikali
na Sekta binafsi kujenga kiwanda cha dawa nchini ambapo utafanyika kwa haraka
ili kukamilikia mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2019” alisema Bw. Bwanakunu.
|
Some examples embrace; soccer, ice hockey, tennis, boxing, and even mixed martial arts. You can also guess on politics and finish result} of particular occasions such as the Eurovision contest, 카지노 사이트 X Factor and the FIFA World Cup Qatar 2022. The manner by which you place your bets varies depending on the type of|the sort of} sport or sport. We also supply live betting along with our traditional pre-event betting.
JibuFuta