Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Ijumaa, 19 Oktoba 2018

DKT. NDUGULILE AAHIDI UJENZI WA HOSPITALI MPYA YA WILAYA YA RUFIJI.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua dawa zilizopo katika stoo ya Hospitali ya Utete wilayani Rufiji kuhakikisha kama zina nembo ya serikali wakati wa muendelezo wa ziara yake katika mkoa wa Pwani.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akifafanuliwa jambo na Mganga Mkuu wa wilaya ya Rufiji Dkt. Juma Abdallah wakati alipofanya ziara katika Hospitali ya Utete iliyopo wilayani humo. Wengine ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Ibrahim Mohamed (katikati) na mbunge wa Rufiji Mohamed Mchengelwa.

NA WAJMW-RUFIJI
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ameahidi ujenzi wa Hospitali mpya ya Utete ili kuboresha huduma za afya wilayani Rufiji.

Dkt. Ndugulile amesema hayo  wakati alipokuwa anaendelea na ziara katika Mkoa wa Pwani ambapo alionekana kutoridhishwa na majengo ya Hospitali hiyo kongwe iliyojengwa kipindi cha ukoloni na majengo yake yakionekana chakavu.

"Naomba niwe balozi wenu, nimejionea mwenyewe majengo ya Hospitali hii, kwa kweli ni chakavu sana” alisema Dkt. Ndungulile na kuendelea “sasa baada ya nyinyi kuomba serikali ifanye ukarabati wa Hospitali hii, mimi nitahakikisha tunapata pesa ya kujenga Hospitali mpya"

Aidha, Dkt. Ndugulile alionekana kutoridhishwa na nyumba wanazoishi madaktari wa Hospitali hiyo huku zikionekana kuwa chakavu zinazohatarisha maisha ya watu wanaoishi humo na kuahidi kuzifanyia ukarabati ikiwa ni pamoja na kutafuta fedha kwa ajili ya kujenga nyumba mpya za kisasa.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Juma Abdallah amesema hali ya watumishi katika sekta ya afya siyo nzuri hasa kwa wenye taaluma mbalimbali. Amesema kuna upungufu wa asilimia 49 ya watumishi wenye ujuzi unaohitajika, huku akifafanua upungufu mkubwa katika kada ya wauguzi.

"Katika kada ya wauguzi tuna upungufu wa wauguzi 146, Madaktari 4, madaktari wasaidizi 11, wataalam wa mionzi 15, wataalam wa maabara 8, ustawi wa jamii 5, maafisa afya 12, makatibu wa afya 3 na watunza kumbukumbu za Hospitali 10". Amesema Mkuu huyo wa wilaya.

Pia amesema wilaya hiyo haina daktari bingwa wa aina yeyote na mtaalamu wa mionzi baada ya aliyekuwepo kuondoka mara baada ya kuripoti kwa maelezo kuwa mazingira ya Rufiji siyo rafiki kwake.

Kwa upande wa hali ya upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi, Mkuu wa Wilaya hiyo amesema upatikanaji wa wake ni wa wastani.  Hadi kufikia mwezi Septemba 30, 2018 dawa zinazofuatiliwa Tracer Medicine upatikanaji wake ni asilimia 90.6 na dawa zingine upatikanaji wake ni kwa zaidi ya asilimia 55.

Kufuatia hali hiyo, Naibu Waziri amemuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani Dkt. Yudas Ndungile kuhakikisha anatafuta mtaalam wa mionzi kutoka Wilaya nyingine ili kutoa huduma katika wilayani humo. Aidha Dkt. Ndugulile ameahidi kufanyia kazi suala hilo la upungufu wa watumishi hao muhimu.

Wakati huo huo Dkt. Ndugulile alihitimisha ziara yake katika Mkoa wa Pwani kwa kutembelea vituo vya afya vya Ikwiriri ambacho kimekamilisha ujenzi ya Wodi ya watoto, wodi ya Wanawake, jengo la kuhifadhia maiti na jengo la kufulia nguo.

Kwa upande wa kituo cha afya Kibiti, Naibu Waziri huyo ameonekana kutoridhika na huduma za afya zinazotolewa katika kituo hicho na kuona kuna ubadhirifu wa fedha za umma katika ujenzi wa miundombinu ya maabara, wodi na chumba cha upasuaji huku akiagiza kamati ya ulinzi na usalama kuchunguza na kuwachukulia hatua wote watakaobainika na ubadhirifu wa fedha za umma.

Katika kuhitimisha ziara yake katika Mkoa wa Pwani Dkt. Ndugulile alitembelea ujenzi wa kituo cha Bungu kwa lengo la kukagua miundombinu na hali ya utoaji huduma za afya, ambapo aliridhishwa na maendeleo ya kituo hicho na kuahidi serikali kuendelea kusaidia katika ujenzi huo lengo likiwa ni kusogeza huduma za afya karibu zaidi na wananchi.

MWISHO

0 on: "DKT. NDUGULILE AAHIDI UJENZI WA HOSPITALI MPYA YA WILAYA YA RUFIJI."