Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Fundi
msanifu wa wilaya ya Mafia Ramadhan Madenge kuhusiana na mchoro wa kituo
cha afya cha Kilongwe.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwenyekiti
wa kijiji cha Kifinge Hamis Omary (kushoto) wakati alipotembelea kuona
maendeleo ya ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile (kushoto) akionesha moja ya dawa za serikali wakati
alipofanya ziara kuona hali ya utoaji wa huduma za afya katika Hospitali
ya wilaya ya Mafia kuona.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akisikiliza maelezo kutoka kwa mganga mkuu wa wilaya
ya Mafia Dkt. Zuberi Mzige kuhusiana na mchoro wa jengo la huduma kwa
wagonjwa wa bima ya afya wakati wa ziara katika Hospitali ya Wilaya
hiyo.
MARUFUKU MGONJWA KWENDA KUNUNUA DAWA NJE IKIWA DAWA ZIPO.
Na WAMJW-MAFIA
SERIKALI
kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
imepiga marufuku kwa watoa dawa kuwaandikia wagonjwa kwenda kununua
kwenye maduka binafsi ikiwa kwenye kituo kuna dawa na vifaa tiba vya
kutosha.
Hayo yamezemwa
na Naibu Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto
Dkt. Faustine Ndugulile wakati alipotembelea Hospitali ili kuangalia
hali ya utoaji huduma Wikayani Mafia .
"Nauagiza
uongozi wa hospitali ya wilaya ya Mafia mkoani Pwani kuwarudishia
wagonjwa wote gharama za vifaa tiba na dawa walizonunua katika maduka
binafsi ambazo zinapatikana Hospitalini hapo" alisema Dkt. Ndugulile.
Aidha
Dkt. Ndugulile amesema kuwa amebaini baadhi ya wagonjwa walioandikiwa
kwenda kununua dawa na vifaa tiba katika maduka binafsi huku baadhi ya
dawa hizo zikiwepo katika stoo ya kuhifadhia dawa.
Dkt.
Ndugulile amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri na Mganga Mkuu
wa Wilaya ahakikishe wanawarudishia wagonjwa wote gharama walizotumia
kununua dawa nje ya Hospitali hiyo.
Pia
Dkt. Ndugulile alishangazwa na Hospitali hiyo kutokuwa na dawa na vifaa
tiba muhimu huku serikali ikiwa imetenga kiasi cha Tsh. Bilioni 270
kuanzia mwaka 2015/16 kutoka bilioni 31 za hapo awali, ikiwa na lengo la
kuhakikisha dawa zote zinapatikana katika Hospitali na vituo vyote vya
afya nchini.
Vikevike
Dkt. Ndugulile ameuagiza uongozi wa wilaya ya Mafia kuhakikisha bajeti
ya dawa inapitiwa yakinifu na kutekelezwa ili kuepuka changamoto ambazo
zinaweza kuepukika za ukosefu wa dawa na vifaa tiba muhimu na kuleta
usumbufu kwa wakazi wa wilaya hiyo.
Amebaini
upungufu huo wa dawa na vifaa tiba baada ya kutembelea wodi za watoto
na akina mama waliojifungua na kuelezwa na baadhi ya wagonjwa hao
kununua dawa na vifaa tiba vya kusaidia kujifungua nje ya Hopitali hali
ambayo imekua kero kwa wagonjwa wanaoenda kutibiwa katika Hospitali
hiyo.
Wakati huo huo Dkt.
Ndugulile amesitisha ukarabati wa jengo la wagonjwa wa bima baada ya
kuona kuna ubadhirifu wa fedha ambao hauendani na mazingira halisi ya
ukarabati huo.
Pamoja na
hayo Dkt. Ndugulile amefanya ziara katika kituo cha afya cha Kilongwe
na zahanati ya kifinge na kutoridhishwa na maendeleo ya vituo hivyo
huku akibaini utaratibu usiofaa wa manunuzi ya vifaa vya ujenzi na
kuamuru Halmashauri hiyo ifuate utaratibu wa manunuzi wa Force Account.
Sambamba
na hilo Dkt. Ndugulile alisitisha mara moja ukarabati wa jengo katika
zahanati hiyo huku akiagiza kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya
ikishirikiana na kamati ya ujenzi kufuatilia uhalisia wa gharama hiyo.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mafia Shaibu Mnunduma amemshukuru Naibu
waziri huyo kufanya ziara kisiwani humo huku akiahidi kuzifanyia kazi
changamoto zote zilizobainika ili kutoa huduma bora za afya kwa wananchi
wa wilaya hiyo.
Naye
Fundi msanifu wa Wilaya ya Mafia Ramadhan Madenge alisema kuwa kuna
ukarabati wa jengo hilo unagharimu takribani Tsh. Milioni 94.
0 on: "MARUFUKU MGONJWA KWENDA KUNUNUA DAWA NJE IKIWA DAWA ZIPO"