Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akikagua cheti cha mgonjwa katika wodi ya akina mama wakati alipotembelea Hospitali ya wilaya ya
Manyoni kuona hali ya utoaji huduma za afya.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile (kushoto) akikagua madaftari ya wagonjwa waliolazwa
katika wodi ya akina mama wakati alipotembelea Hospitali ya wilaya ya
Manyoni kuona hali ya utoaji huduma za afya. kulia ni Mkuu wa wilaya
hiyo Bi. Rahabu Solomon.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile (Kulia) akifafanua jambo wakati alipotembelea kitengo
cha kuzalisha chakula cha lishe kwa mama wajawazito na watoto katika
Hospitali ya Mtakatifu Gasper. Kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa
Hospitali hiyo Fr. Seraphine Lesiriam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akiongea na wananchi waliokuwa wakisubiri huduma
Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Singida wakati alipofanya ziara
hospitalini hapo kuona hali ya utoaji wa huduma za afya.
SERIKALI YAAHIDI KUPELEKA GARI YA WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MANYONI
NA WAMJW-SINGIDA
Serikali
imetangaza neema ya kupeleka gari ya wagonjwa (Ambulance) katika
Hospitali ya Wilaya ya Manyoni ili kutatua tatizo linaloikabidi Wilaya
hiyo hususan ya vifo vitokanavyo na uzazi.
Ahadi
hiyo imetolewa jana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati alipoitembelea
hospitali hiyo kwa lengo la kutazama utoaji wa huduma za afya ikiwa ni
sehemu ya ziara yake ya siku tatu katika mkoa wa Singida.
Dkt.
Ndugulile amefikia uamuzi huo baada ya kusikiliza kero kutoka kwa
wananchi wanaotumia hospitali hiyo ambapo wengi walisema kungekuwepo na
gari ya wagonjwa kungeepusha vifo vya akina mama wajawazito na watoto
pamoja na wagonjwa wanaohitaji huduma za dharura.
"Naomba
niwaahidi wananchi wa Manyoni, Serikali imeagiza magari ya kubebea
wagonjwa ambayk yanaweza kufika mwezi Disemba mwaka huu,hivyo
nitahakikisha katika mgao wa magari hayo basi na hospitali hii ya Wilaya
inapata gari moja kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi wa hapa.
Alisema Dkt. Ndugulile.
Aidha,
Dkt.Ndugulile aliahidi kuwatafutia wataalam wa Afya watakaoweza kwenda
kupunguza uhaba wa watumishi wanaokabiliana nayo hospitali hiyo
Naye
Mganga mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Atupele Mohamed alisema
hospitali hiyo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa majengo ikiwemo chumba
cha huduma za uzazi ambapo uwezo wake kwa mwezi ni kuzalisha akina mama
90 lakini kwa sasa huzalisha wastani wa akina mama 400.
Aidha,
Dkt. Atupele alisema Hospitali hiyo ina upungufu mkubwa wa watumishi
wenye sifa, ambapo ina jumla ya watumishi 107 sawa na asilimia 53 ya
watumishi wanaohitajika.
Dkt.
Atupele alitaja uhaba mkubwa wa watumishi hao ni Madaktari, Wauguzi,
Wataalamu wa mionzi na wataalamu wa kutoa huduma za usingizi.
Katika
Wilaya hiyo Naibu Waziri huyo aliweza kutembelea kutembelea kituo cha
kulea wazee na wasiojiweza cha Sukamahela pamoja na Hospitali ya rufaa
ya Mtakatifu Gasper iliyopo Itigi na kuridhika na hali ya utoaji wa
huduma za afya katika Hospitali hiyo.
0 on: " SERIKALI YAAHIDI KUPELEKA GARI YA WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MANYONI"