Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Bakari Kambi wa kwanza kulia
akikagua kituo cha muda mfupi cha kuhifadhia wagonjwa watakaopatikana
au kusadikika kuwa na ugonjwa wa Ebola katika Bandari ya kigoma kabla
ya kuwapeleka katika Kituo husika wakati wa ukaguzi na mafunzo kwa
watumishi wa afya juu ya kujikinga na ugonjwa huo leo Mkoani Kigoma,
katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya
Wizara ya Afya Dkt. Mohammed Ally Mohammed.
Mkurugenzi wa Idara ya Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya Wizara ya Afya
Dkt. Mohammed Ally Mohammed akitoka kukagua ndani ya kituo cha muda
mfupi cha kuhifadhia wagonjwa watakaopatikana au kusadikika kuwa na
ugonjwa wa Ebola katika Bandari ya kigoma kabla ya kuwapeleka katika
Kituo husika wakati wa ukaguzi na mafunzo kwa watumishi wa afya juu ya
kujikinga na ugonjwa huo leo Mkoani Kigoma.
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Bakari Kambi wa kwanza kulia
akikagua maeneo mbalimbali ya Bandari ya Kigoma wakati wa ukaguzi na
mafunzo kwa watumishi wa afya juu ya kujikinga na ugonjwa huo leo Mkoani
Kigoma katikati ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt. Paul Chawote na
kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya Wizara
ya Afya Dkt. Mohammed Ally Mohammed.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt. Paul Chawote aliyesimama akisoma
taarifa ya ugonjwa wa Ebola na hatua wanazochukua kujikinga na ugonjwa
huo pindi utakapoingia nchini kwani kwa sasa ugonjwa huo umetaarifiwa
upo nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemocrasia ya Congo wakati wa ukaguzi
na mafunzo kwa watumishi wa afya juu ya kujikinga na ugonjwa huo leo
Mkoani humo.
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Bakari Kambi katikati akiongea na
baadhi ya watumishi wa afya pamoja waandishi wa habari wa Mkoa Kigoma
hawapo Pichani wakati wa mafunzo ya kujiandaa kujikinga na Ugonjwa wa
Ebola ambao umetaarifiwa kuwa katika nchi jirani ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo leo mkoani humo. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa
Idara ya Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya Wizara ya Afya Dkt. Mohammed
Ally Mohammed na wa kwanza ni Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Bi. Mwanamvua
Mulindoko.
VIONGOZI WA DINI WAWE SEHEMU MUHIMU KATIKA MIKAKATI YA KUJIKINGA NA EBOLA.
NA WAMJW-KIGOMA
VIONGOZI
wa dini zote wametakiwa kushirikishwa kwenye maandalizi ya mapambano
ya ugonjwa wa ebola ambao umetaatifiwa upo nchi jirani ya Jamhuri ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo endapo itatokea utaingia nchini
Tanzania ili kuweza kuutokomeza kabisa.
Hayo
yamesemwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Bakari Kambi wakati
alipotembelea Mkoa wa Kigoma akiongozana na timu yake ya wataalam kwa
ajili ya ukaguzi wa nyenzo na afua mbalimbali zilizowekwa ili kupambana
na ugonjwa wa ebola leo Mkoani humo.
"Afua
muhimu ya mkoa wowote katika kupambana na ugonjwa huu ni
kuwashirikisha vizuri viongozi wa dini zetu pamoja na viongozi wa kimila
na jamii kwani ndio wanaokutana na wanajamii kwa muda mwingi zaidi
hivyo kuwashirikisha kwao elimu juu ya kujikinga na Ebola itakuwa kubwa
zaidi na hatimae tutafanikiwa kujikinga na ugonjwa huu" alisema Prof.
Bakari.
Aidha Prof.
Bakari Kambi amesema kuwa Mkoa wa Kigoma upo kwenye hatari zaidi ya
kupata ugonjwa wa Ebola kwa kuwa kuna mipaka mingi iliyo wazi ambayo
inaingiza wageni kutoka Burundi na Congo ambapo ugonjwa huo umetaarifa
upo maeneo ya nchi ya Congo.
Mbali
na hayo Prof. Bakari Kambi ameuoingeza uongozi wa Mkoa wa Kigoma kwa
jitihada na mikakati waliyoiweka na kuifanyia kazi ili kuweza kudhibiti
ugonjwa wa Ebola endapo utaingia Mkoani humo.
Kwa
upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt. Paul Chaote amesema kuwa
Kigoma amesema kuwa hadi sasa hakuna mgonjwa yeyote aliyeripotiwa kuwa
na dalili za ugonjwa wa Ebola katika maeneo yote ya Mkoa huo.
"Utambuzi
wa joto la Mwili kwa wageni kutoka nchi jirani ya Congo wanaoingia
kupitia bandari ya Kigoma, Manyovu, Kibirizi, Mabamba , Uwanja wa Ndege ,
Kituo cha Gari Moshi bado unaendea kufanyika kwa uhakika kwa kutumia
Thermo scanner ili kudhibiti ugonjwa huo" alisema Dkt. Chaote.
Aidha
Dkt. Chaote amesema kuwa bado wanaendelea kutoa elimu kwa jamii,
watumishi wa Afya, madereva wa magari ya kubebea wagonjwa kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali ili kujikinga na ugonjwa huo endapo
utaingia nchini.
"Tumetoa
mafunzo kwa timu za kitaalam mbalimbali za Mkoa pamoja na kuhakikisha
madawa, vifaa tiba na PPE vipo vya kutosha wakati wote katika vituo
vyote vilivyoanishwa kupokea na kutoa huduma kwa wagonjwa wa Ebola"
alisema Dkt. Chaote.
Mganga
Mkuu wa Serikali Prof. Kambi ameambatana na jopo la wataalam ikiwemo
idara ya uhakiki ubora wa huduma za afya , Kitengo cha Dharura na
Maafa,Elimu ya Afya kwa Umma , Kitengo Cha mawasiliano Wizara ya Afya
zote kutoka Wizara ya Afya pamoja na Wawakilishi kutoka Shirika la Afya
Duniani (WHO) ili kukagua na kujiridhisha mikakati ya kujikinga na
Ebola endapo itaingia nchini.
0 on: "VIONGOZI WA DINI WAWE SEHEMU MUHIMU KATIKA MIKAKATI YA KUJIKINGA NA EBOLA."