Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy
Mwalimu (MB) akisisitiza jambo katika Mkutano uliowakutanisha viongozi
na watendaji wakuu wa Halmashauri na Wilaya kutoka Mkoa wa Tanga wenye
lengo la kuendeleza juhudi za Serikali juu ya masuala Ya uzazi wa
mpango, chini ya JhPiego unaofadhiliwa na Melinda Gate.
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe ambae alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Kisa
Kasongwe akitoa neno umbele ya viongozi na watendaji wakuu wa
Halmashauri na Wilaya baada ya kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Áfya
Mhe Ummy Mwalimu.
Mganga mkuu wa Mkoa wa Tanga DKt. Asha Mahita akielezea hali ya huduma
za uzazi wa mpango Mkoani Tanga katika Mkutano wa wenye lengo la
kuendeleza juhudi za Serikali juu ya Uzazi wa mpango nchini.
Viongozi wa Halmashauri na Wilaya kutoka Tanga leo waliohudhuria kikao
chenye lengo la kuendeleza juhudi za Serikali juu ya uzazi wa mpango.
Picha ya pamoja ikiongonzwa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akiwa na
viongozi wa Halmashauri na Wilaya ya Tanga baada ya Mkutano wenye lengo
la kuendeleza juhudi za Serikali juu ya masuala Ya uzazi wa mpango ulio
chini ya JhPiego unaofadhiliwa na Melinda Gate.
WIZARA YA AFYA YATENGA BILIONI 14 KWA AJILI YA HUDUMA UZAZI WA MPANGO
Na.WAMJW-Tanga
Viongozi
na watendaji wakuu wa halmashauri ya Jiji la Tanga wametakiwa kuwa
wabunifu katika kuhakikisha wanawafikia wanawake wengi wanaoishi mjini
ili waweze kujiunga na huduma za uzazi wa mpango.
Wito
huo umetolewa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto Ummy Mwalimu wakati akifungua mkutano uliowakutanisha Viongozi na
watendaji wakuu wa Halmashauri ya Jiji,Wilaya ya Tanga Mjini pamoja na
Wilaya ya korogwe wenye lengo la kuendeleza juhudi za uzazi wa mpango
nchini.
Waziri Ummy alisema kwamba Serikali ya
awamu ya tano imejipanga kutokomeza vifo vya akina mama wajawazito na
watoto wachanga hivyo imejipanga kuwafikia wananchi wengi ili kuweza
kupunguza kwa asilimia 30 vifo vitokanavyo na uzazi.
“lazima
muonyeshe utayari na umakini kama viongozi katika kuwekeza kwenye uzazi
wa mpango, mkiwa wabunifu mtawawezesha kuwafikia akina mama wengi wa
mjini, hata akina baba kwa kuwapa elimu ya kutosha na kufanya maamuzi
ili wapange lini wanataka kuzaa,watoto wangapi na watofautiane kwa miaka
mingapi”.Alisema Waziri Ummy.
Aidha, aliwataka
viongozi kutumia fedha hizo kuziweka kwenye vitu endelevu ili mradi huo
uongeze wanawake wengi kutumia njia za uzazi nchini.
“Msiweke
mipango ya mardi huu kwenye semina bali mradi huu uwe njia ya kufungua
miradi mingine kutoka kwa wadau wa maendeleo” alisema Waziri Ummy.
Waziri
Ummy aliendelea kusema kuwa Serikali kupitia Wizara ya afya kwa mwaka
huu wa fedha 2018/2019 umetenga shilingi bilioni 14 kwa ajili ya afya ya
uzazi wa mama na mtoto tofauti na miaka ya nyuma ambapo kabla Serikali
ya awamu ya tano haijaingia madarakani wizara ilikua ikitenga shilingi
bilioni 2 kwa ajili ya matumizi kitengo hicho.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Bi.Kisa Kasongwe ambaye alimuakilisha Mkuu wa
Mkoa wa Jiji la Tanga alisema halmashauri ya Jiji la Tanga ipo tayari
kutoa ushirikiano na shirika hilo kwani mradi huo utaleta hali nzuri kwa
akina mama pamoja na watoto wachanga.
Wakati huo
huo Kaimu Mwakilishi Mkazi wa shirika la jhpiego Dkt.Dustan Bishanga
alisema kuwa mradi huo unakuja kuongeza rasiliamali ambazo hazitoshi
katika kusimamia na kutekeleza katika uwekezaji wa uzazi wa mpango.
“Mradi
huu utafanikiwa endapo viongozi wa Jiji la Tanga mtatekeleza na
kufanya mpango huu kufanikiwa hivyo mtapelekea tuwaletee mradi mwingine
wa afya ya uzazi kwa vijana endapo mradi huu wa kwanza mtaufanikisha
ipasavyo”.Alisema Dkt.Bishanga.
Mradi wa “Tupange
pamoja” ulianzishwa mwaka 2016 na kutekelezwa na halmashauri ya Jiji la
Dar es Salaam na Arusha ambapo kwa jiji la Dar es Salaam walipatiwa
shilingi milioni 250 kwa ajili ya kutekeleza uzazi wa mpango kwa
halmashauri zote na hivi sasa unaanza kwa Jiji la Tanga.
Idadi
ya akina mama wanaotumia uzazi wa mpango kwa Jiji la Tanga ni asilimia
31 ambapo kitaifa inatakiwa kufikia asilimia 45 hadi mwaka 2020 na vifo
vya akina mama kwa halmashauri hii imepungua kutoka vifo 69 mwaka 2014
hadi vifo 45 kwa mwaka 2017.
0 on: "WIZARA YA AFYA YATENGA BILIONI 14 KWA AJILI YA HUDUMA UZAZI WA MPANGO"