Hayo yamesemwa leo na katibu Mkuu Wiraya ya
Afya,maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Mpoki Ulisubisya wakati
kikao cha wadau cha kujadili taarifa ya uchambuzi yakinifu kwa ajili ya kuhuisha mtaala wa watoa
huduma ya afya ngazi ya jamii kinachofanyika
jijini hapa.
Dkt.Mpoki alisema Serikali inaendelea kutekeleza
mikakati mbalimbali ya sekta ya afya yenye lengo la kuboresha huduma za afya na
kuimarifa afya za wananchi.
Aidha,alisema wahudumu wa afya ngazi ya jamii wana nguvu
kwani wana mchango mkubwa mkubwa kwani ni makomandoo ambao wanaweza
kutoa elimu kwa jamii na hivyo kusaidia kuzuia magonjwa yanayosababisha vifo
vitokanavyo na uzazi.
Alisema takwimu zinaonesha kuwa vifo vitokanavyo
na uzazi kati ya akina mama 100,000 ni
vifo 556 hutokea hivyo kuwapo wa hudumu
wa afya gazi ya jamii wanaweza kupunguza hali hiyo.
“ Katika kufikia malengo ya Tanzania ya uchumi wa
kati na viwanda, wahudumu wa afya ngazi
ya jamii wanatakiwa kutumika kuwaibua akina mama ambao hawapeleki watoto wao
kupata chanjo, na matumizi sahihi ya matumizi ya vyandarua ili kuepuka ugonjwa
wa Malaria nah ii imeonekana pia katika
nchi za afrika kam Ethiophia,Rwanda na zingine
Hata hivyo Dkt.Mpoki aliwataka wadau kuunga mkono
jitihada hizi za serikali na hivyo kubainisha maeneo ambayo watasaidia
Naye Mkurugenzi wa Mafunzo na Wataalam wa
Rasiliamali watu Dkt.Otilia Gowele alisema kwa sasa wanapitia upya mtaala wa mafunzo kwa wa hudumu wa afya
ngazi ili kuendana na hali halisi ya
sasa na mahiaji katika sekta ya afya.
“tuekutana ili kupokea na kujadili maoni ya wadau
kwa kuzingatia tathimini ya kina iliyofanywa katika kuuhisha mtaala wa mafunzo
ya wahudumu wa afya ngazi ya jamii na kuangalia changamoto ili kuendana na
mahitaji halisi na kukidhi soko la ajira katika hopsitali za umma na binafsi,”
alisema.
Alisema tangu kuanza kutumika kwa mataala wa
mafunzo ya watoa huduma wa afya ngazi ya jamii mwaka 2015 na kutumika kwenye
vyuo 78 hapa nchini, tayari wataoa huduma wapatao 9,000 wamehitimu.
.
0 on: "WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII WANAHITAJIKA NCHINI "