Waziri wa Maendeleo kutoka nchi ya Uingereza Mhe. Penny Mordaunt
(katikati) akimsalimia mtoto mchanga aliyebebwa na baba yake katika
jengo la Kliniki ya Baba, Mama Na Mtoto. Kulia ni Waziri wa Áfya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.
Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu akisoma mbao ya matangazo katika Zahanati ya Tabata jijini Dar
es salaam pindi alipofika kupokea ugeni wa Waziri wa Maendeleo kutoka
nchi ya Uingereza.
Waziri wa Áfya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa Elimu juu ya
umuhimu wa kukata Bima ya Áfya kwa mtoto (Toto Afya Card) kwa mmoja kati
ya wazazi waliofika katika Zahanati ya Tabata kupata huduma za
matibabu ya mtoto.
Mshauri wa masuala Ya Afya kutoka ubalozi wa Uingereza
DKt. Gloria Ngaiza (wapili Kushoto) akimtafasiria Waziri wa Maendeleo
kutoka nchi ya Uingereza Mhe. Penny Mordaunt kilichokuwa kikisemwa na
Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Tabata (Wakwanza Kushoto).Wa mwisho Kulia ni Waziri wa Áfya Mhe. Ummy Mwalimu.
IDADI YA WANAWAKE WANAOTUMIA HUDUMA ZA ZA UZAZI WA MPANGO ZAONGEZEKA NCHINI
Na WAMJW - DSM
SERIKALI
kupitia Wizara ya Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
imesema kuwa idadi ya wanawake wanaotumia huduma za Afya za Kisasa za
uzazi wa mpango zimeongezeka nchini mpaka kufikia Asilimia 32.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Ummy Mwalimu leo wakati alipoupokea ugeni wa Waziri wa Maendeleo
kutoka nchini Uingereza katika Zahanati ya Tabata jijini Dar es salaam
ukiwa na lengo la kutatua changamoto za Sekta ya Áfya hususani katika
huduma za Afya ya mama na mtoto.
"Kupitia
Msaada wao tumeweza kuongeza idadi ya wanawake wanaotumia huduma za
Kisasa za uzazi wa mpango, hatupo vizuri, tupo Asilimia 32, tumeweka
lengo itapofika 2020 tufikie Asilimia 45 ya wanawake walioolewa
wanatumia njia hizi" Alisema Waziri Ummy Mwalimu.
Waziri
Ummy aliendelea kusema kuwa, bado kuna changamoto ya vifo vitokanavyo
na uzazi nchini, takribani wanawake 556,000 katika kila vizazi hai laki
moja wanafariki na kwa mujibu wa Wataalam uzazi wa mpango utaweza
kuchangia Mpaka Asilimia 30 katika Kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.
Pia
Waziri Ummy alisema kuwa Serikali ya Tanzania imechukua hatua kwa
kutenga fedha za ndani katika kupambana na changamoto za sekta ya Áfya
ikiwemo kuajiri watumishi wa sekta ya Áfya jambo linalosaidia Kupunguza
changamoto hizo za vifo vya akina mama wajawazito na mtoto wachanga.
"Sisi
kama Serikali tumejiongeza, tumechukua hatua na kutenga rasilimali
fedha za ndani ikiwemo kuajili watoa huduma za afya, kuhakikisha Kwamba
tunatatua changoamoto hiyo " alisema Waziri Ummy.
Hata
hivyo Waziri Ummy aliishukuru Serikali ya Uingereza kupitia kwa Waziri
wa Maendeleo Mhe. Penny Mordaunt kwa kushirikiana na Serikali ya
Tanzania katika kuboresha huduma za afya hasa katika huduma za mama na
mtoto.
Kwa upande wake
Waziri wa Maendeleo kutoka Uingereza Mhe. Penny Mordaunt ameshukuru
Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Áfya kwa kazi nzuri wanayoifanya
ya kuhudumia wananchi wa Tanzania na kuahidi kupeleka salamu za Tanzania
nchini Uingereza.
0 on: "IDADI YA WANAWAKE WANAOTUMIA HUDUMA ZA ZA UZAZI WA MPANGO ZAONGEZEKA NCHINI."