Na.WAMJW - Dodoma
Akina
Mama wajawazito wametakiwa kuwahi kliniki mara wanapohisi wana
ujauzito na kufuata ushauri wa wataamu wa afya ili kuwakinga watoto
wanaotarajia kujifungua dhidi ya maabukizi ya Virus vya UKIMWI
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa huduma za kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Leonard Subi mjini Dodoma hivyo
kuwataka wananchi kuchukua hatua katika kujikinga na maradhi mbalimbali
ikiwemo Virusi Vya Ukimwa (VVU).
Amesema Utafiti
uliofanywa mwaka 2010 maambukizi ya Virus yalikua asilimia 26 kutoka
kwa mama kwenda kwa mtoto huku utafiti uliofanywa mwaka 2016/2017
unaonesha kuwa maambukizi haya yamepungua na kufikia asilimia 7.6 ambapo
Serikali imesema inatarajia maambukizi haya yapungue mpaka asilimia 2
ifikapo 2020-2021.
“Ni muhimu kwa wajawazito
kuhudhuria kliniki na kupima VVU hii itasaidia kuzuia maambukizi ya VVU
kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, malezi na makuzi mzuri ya Mtoto
yanategemea wazazi wote wawili yaani baba na mama wazazi wote wanaaswa
kushirikiana hasa katika kupima afya afya ili mtoto atakaezaliwa asiwe
na maambukizi ya VVU”Alisema Dkt.Subi.
Aliongeza
kuwa moja ya changamoto inayokwamisha mpango huu ni wanaume kukumbatia
mila na destuli za kutoandamana na wenzi wao kliniki wakati wa kipindi
cha ujauzito,
“hivyo familia au makabila ambayo bado yanaona kwamba
mwanaume kumsindikiza mwenzi wake kliniki ni kujishushia hadhi waachane
nazo”.
Aidha, Dkt.Subi amewataka vijana kuchukua
hatua za kwenda katika vituo vya afya kupata elimu ya uzazi na kupima
afya zao maana wao ndio mama au baba wanaotarajiwa,mimba za utotoni ni
hatari kwa afya zao na kama kuna tatizo lolote wafike katika vituo vya
afya ili kupata msaada wa kitalaamu.
Alisisitiza
kuwa vituo vya kutolea huduma za afya vyote nchini hivi sasa vinatoa
huduma ya elimu bure kuhusiana na afya ya uzazi na endapo mama mjamzito
atagundulika ana maambukizi ya VVU ataanzishiwa dawa ambazo zitamkinga
mtoto asizaliwe na maambukizi ya Virus vya UKIMWI.
0 on: "DKT. SUBI AWAHASA WANAWAKE KUWAI KLINIKI PINDI WANAPOHISI WANAUJAUZITO."