Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu akiteta jambo na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya uendeshaji wa hospitali za rufaa za mikoa mbele ya kamati ya kudumu ya bunge ya huduma na maendeleo ya jamii jijini Dodoma.
Wajumbe wakifuatilia mjadala uliokua unaendelea katika kikao cha
mawasilisho ya taarifa za uendeshaji wa Hospitali za rufaa za mikoa
kutoka wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto
katika kamati ya kudumu ya Huduma na maendeleo ya jamii jijini Dodoma
SERIKALI YASOGEZA HUDUMA ZA KIFUA
KIKUU SUGU KARIBU NA WANANCHI
Na.WAMJW,Dodoma
Serikali
kupitia Wizara ya afya imefanya ugatuaji kwa kusogeza karibu na wananchi huduma
ya kifua kikuu sugu (TB) ili kupunguza adha ya kusafiri umbali mrefu kwa
wananchi katika ngazi ya vituo vya
afya sabini na nane nchini.
Hayo
yamesemwa jana na Waziri wa fya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto ummy mwalimu wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa hospitali ya
magonjwa ambukizi Kibong’oto kwa kamati ya huduma za jamii ya Bunge jijini
hapa.
Waziri Ummy
alisema wamefanya ugatuaji wa vituo
hivyo vya afya ili kuwezesha wagonjwa kupata tiba jirani na jamii
inayowazunguka na hivyo kujenga uelewa
wa wananchi juu ya ugonjwa na kushiriki
kikamilifu katika kumhudumia mgonjwa hasa katika chakula,masuala ya kijamii na
kisaikolojia.
Alitaja
mikoa ambayo vituo hivyo vipo ni pamoja na Kagera, Mtwara, Kilimanjaro, Dar es
Salaam, Dodoma, Geita, Mbeya,
Pwani,Mrorgoro,Njombe,Iringa, Tanga, Mwanza , Lindi na Pemba na kuongeza kuwa
hadi sasa wagonjwa wapatao 112 wamepata huduma
za tiba ya TB sugu.
“Takwimu
zinaonesha kuwa kati ya watu laki moja, watu 287 wana TB na kati ya watu 100
kati yao 40 tunawagundua wana TB hapa
nchini”alisema Waziri Ummy.
Hata hivyo
mnamo mwaka 2017 Serikali ilizindua
kituo bora katika hospitali hiyo kwa kutoa huduma za afya kwa wachimbaji wa
migodi wanaougua magonjwa ya TB, Mapafu na usikivu unaosababishwa na ulipuaji
wa baruti migodini kwa kushirikiana na mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WCF).
Tangu
kuanzishwa kwa kituohicho jumla ya
wagonjwa 863 wamepata huduma,wagonjwa 614 walipima makohozi na 116(19%)
waligundulika kuwana TB na 123(15%) walikuwa na magonjwa ya mapafu
yanayosababishwa na vumbi na 125(15.3%) walikuwa na upotevu wa usikivu.
0 on: "SERIKALI YASOGEZA HUDUMA ZA KIFUA KIKUU SUGU KARIBU NA WANANCHI"