Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy
Mwalimu (MB) akisisitiza jambo mbele ya watumishi wa Serikali na
wanafunzi wa Kada ya uuguzi leo wakati wa hafla ya makabidhiano ya
Majengo ya chuo cha uuguzi Tanga.
Mkuu wa mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigela akiwasamia wanafunzi wa Kada
ya uuguzi wakati alipomkaribisha mgeni rasmi, Waziri wa Áfya Mhe. Ummy
Mwalimu katika hafla ya makabidhiano ya Majengo ya chuo cha uuguzi
Tanga.
Mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa chuo cha uuguzi Tanga Felister Bulali
akitoa maelekezo ya namna ya kumuudumia Mtoto aliyetoka kuzaliwa ,
mbele ya Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Mhe. Ummy Mwalimu (wapili Kushoto), Wakwanza ni mkuu wa chuo hicho Bi.
Leah Makala na watatu ni Mkuu wa mkoa wa Tanga Mhe Martine Shigela.
Waziri wa Áfya Mhe Ummy Mwalimu akiteta jambo juu ya kifaa cha
kujifunzia chenye umbo la Mtoto, wakati wa hafla ya makabidhiano ya
Majengo ya chuo cha uuguzi Tanga. Wakwanza ni mkuu wa chuo hicho Bi Leah
Makala.
Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy
Mwalimu akisakata ngoma na kikundi cha ngoma cha kinamama leo wakati wa
hafla ya makabidhiano ya Majengo ya chuo cha uuguzi Tanga
Bweni la ghorofa nne la wanafunzi lenye uwezo wakulaza wanafunzi 380 kwa
wakati mmoja likiwa ni baadhi ya majengo yaliyogharimu kiasi cha
shilingi Bilion 3.5.
Picha ya pamoja ikiongonzwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe
Martine Shigela wakiwa na baadhi ya watumishi wa Serikali wakati wa
Hafla ya makabidhiano ya Majengo ya chuo cha uuguzi Tanga.
SERIKALI YATARAJIA KUDAHILI
WANAFUNZI 380 WA KADA ZA AFYA KATIKA CHUO CHA UUGUZI TANGA.
Na WAMJW - TANGA
SERIKALI kupitia Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, inatarajia kufanya udahili
wa wanafunzi kwa asilimia 100 kutoka wanafunzi Mia moja na Hamsini (150) hadi
Mia tatu themanini wa kada za Afya nchini katika chuo cha Uuguzi Bombo Tanga.
Hayo yamesemwa leo na Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu (Mb)
wakati wa hafla ya makabidhiano ya majengo ya chuo cha Uuguzi Tanga,
yaliyojengwa kupitia ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kupambana na UKIMWI, KIFUA
KIKUU (TB) na MALARIA (Global fund).
Waziri ummy aliendelea kusema
kuwa majengo yaliyokabidhiwa ni juhudi
za Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo katika kuhakikisha wanazalisha
wataalamu wa kada za Afya, hususani Wauguzi na Wakunga jambo litalowawezesha kuwa
Wataalamu bora.
“Udahili wa wanafunzi
umeongezeka kutoka 190 hadi 260, Huwa tunapata shida sana, wanafunzi wengi
wanafaulu na tunakuwa hatuna nafasi ya wapi
pakuwapeleka, kwahiyo tunawashukuru Global fund , tunaweza kudahili hadi
wanafunzi 368” Alisema Waziri Ummy Mwalimu.
Aidha, amemwagiza Mkurugenzi
wa Mafunzo na Rasilimali watu kutoka
Wizara ya Afya kushirikiana na NACTE
kuwachukua wanafunzi wote waliosoma na kufaulu vizuri masomo nya Sayansi
na wenye vigezo na wenye vigezo katika kada ya Afya.
Waziri Ummy aliongeza kuwa,
kutokana na jitihada hizo kumekuwepo na ongezeko la wahitimu ngazi ya
astashahada na Stashahada kwa mafunzo kutoka wahitimu 4473 mwaka 2012/2013 hadi
7561 kwa mwaka 2016/2017 , ongezeko hili ni sawa na Asilimia 69.
Wakati huo huo Kaimu katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Otilia
Gowelle amesema kwa mwaka huu wa fedha , Wizara imetenga shilingi Bilion 8
kwaajili ya ukarabati wa majengo chakavu katika chuo hicho.
Aliendelea kuwa Wakufunzi 143
wamepangiwa kufanya kazi katika vyuo vya Afya nchini, vikiwemo vyuo vya Wauguzi
na Wakunga ambao ndio msingi wa kupunguza athari ya uzazi pamoja na vifo vya
wakina mama wajawazito wakati wa kujifungua.
Nae Mwakilishi wa Global Fund
Dkt. Hiltruda Temba amesema kuwa, Global fund
imeboresha miundombinu yakufundishia katika vyuo 14 na kuwezesha
kufadhili zaidi ya wanafunzi 1500 wa kada za Uuguzi na Ukunga wa Technolojia
dawa, Technolojia maabara na Tabibu katika kipindi cha Mwaka 2015/2016 hadi
2017/2018, pamoja na kutenga shilingi Billion 1.1 kwaajili yakuboresha mifumo
ya Afya.
MWISHO.
0 on: "SERIKALI YATARAJIA KUDAHILI WANAFUNZI 380 WA KADA ZA AFYA."