TAARIFA KWA UMMA KUHUSU VYETI VYA WAHITIMU WA KADA ZA AFYA
Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inapenda
kuwajulisha kuwa imepokea vyeti vya wahitimu kutoka Baraza la Taifa la
Elimu ya Ufundi (NACTE).Vyeti hivyo ni kwa wahitimu waliofanya mitihani 2016, mwezi Septemba na Oktoba 2017 kwa Mafunzo ya Astashada na Stashahada ya
Uuguzi na Ukunga, Mafunzo ya Astashahda ya Wahudumu wa Afya ya Jamii na
Mafunzo ya Sayansi Shirikishi za Afya (Utabibu, Wateknolojia wa Maabara,
Famasia, Sayansi ya Afya ya Mazingira, Utunzaji kumbukumbu za Afya,
Mazoezi ya viungo ,Utabibu wa Meno na Wateknolojia Macho).
Wizara
inawajulisha wahitimu wa mafunzo hayo kuwasiliana na Wakuu wa Vyuo
kuanzia tarehe 20/08/2018 ili kuweza kupewa utaratibu wa kwenda kuchukua
vyeti vyao kwenye vyuo walivyopatia mafunzo hayo.
Imetolewa na,
KATIBU MKUU (AFYA)
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
20 Agosti, 2018.
0 on: "TAARIFA KWA UMMA"