Mkurugenzi wa Sera na Mipango ambae pia ni Kaimu
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Bw.
Edward Mbanga akifungua Mkutano wa Wataalamu wa TEHAMA (ICT) wa Wizara ya Afya na
Taasisi zake pamoja na Hospitali za Mikoa na Mabalaza ya kitaaluma uliofanyika
leo Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango ambae pia ni Kaimu
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Bw.
Edward Mbanga akisema jambo mbele ya Maofisa TEHAMA kutoka Wizara ya Afya na Taasisi
zake pamoja na Hospitali za Mikoa na Mabalaza ya kitaaluma katika kikao cha
siku mbili kilichofanyika jijini Dodoma ili kujadili changamoto na mapendekezo ili
kuboresha utendaji kazi wao. Kushoto kwake ni Mkurugenzi anaesimamia viwango,
usalama na miongozo ya TEHAMA (EGA) Bw. Moses Makoko na kulia kwake ni Kaimu
Mkurugenzi wa TEHAMA Wizara ya Afya Bw. Walter Ndesanjo.
Mkurugenzi anaesimamia viwango, usalama na
miongozo ya TEHAMA (EGA) Bw. Moses Makoko akiwasilisha mada mbele ya jopo la
Wataalamu wa masuala ya TEHAMA (ICT) kutoka Wizara ya Afya na Taasisi zake
pamoja na Hospitali za Mikoa na Mabalaza ya kitaaluma katika kikao cha siku
mbili kilichofanyika jijini Dodoma ili kujadili changamoto na mapendekezo ili
kuboresha utendaji kazi wao.
Jopo la Wataalamu wa masuala ya TEHAMA (ICT) kutoka
Wizara ya Afya na Taasisi zake pamoja na Hospitali za Mikoa na Mabalaza ya kitaaluma
wakifuatilia kwa karibu ujumbe kutoka Mkurugenzi anaesimamia viwango, usalama na
miongozo ya TEHAMA (EGA) Bw. Moses Makoko
Picha mbali mbali za Maofisa TEHAMA wakifuatilia
kwa makini mada iliyotolewa na Mkurugenzi anaesimamia viwango, usalama na
miongozo ya TEHAMA (EGA) Bw. Moses Makoko katika kikao cha siku mbili kilichofanyika
jijini Dodoma ili kujadili changamoto na mapendekezo ili kuboresha utendaji
kazi wao.
Jopo la Wataalamu wa masuala ya TEHAMA (ICT) kutoka
Wizara ya Afya na Taasisi zake pamoja na Hospitali za Mikoa na Mabalaza ya kitaaluma
wakifuatilia kwa karibu ujumbe kutoka kwa Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Sera na
Mipango ambae pia ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na watoto Bw. Edward Mbanga
Na WAMJW- DOM
Mkutano wa siku mbili wa Maafisa TEHAMA (ICT) kutoka wa Wizara ya Afya naTaasisi zake pamoja na Hospitali za Mikoa na Mabalaza ya kitaaluma umefunguliwa
leo na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Edward Mbanga Jijini Dodoma.
Lengo la Mkutano huo ni kupitia miongozo ya
matumizi sahihi ya TEHAMA Serikalini ili kuongeza ufanisi wenye tija katika
matumizi ya TEHAMA utaosaidia kuboresha utoaji huduma katika Sekta ya Afya
nchini.
Mbali na hayo kikao hicho kimelenga kupitia
mbali mbali wanazokumbana nazo Wataalamu hao katika utoaji huduma na kutoa
mapendekezo ya kutatua changamoto hizo ili kuboresha utendaji wao katika Sekta
ya Afya.
Hata hivyo kikao hicho kilichowakutanisha
Wataalau wa masuala ya TEHAMA kimekusudia kujenga uelewa wa pamoja baina ya Wataalamu
hao hususan katika masuala ya Sera, Sheria, Kanuni, Miongozo na matumizi sahihi
ya TEHAMA Serikalini.
Kwa upande mwingine Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya
Afya ambae pia ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bw. Edward Mbanga amepongeza
uwepo wa mkutano huo jambo litalosaidia kuiboresha zaidi taaluma hiyo, hovyo
kuahidi kumwalika Afisa Mwandamizi wa Idara ya Utawala ataesikiliza na kutatua
changamoto zinazowakumba.
0 on: "MKUTANO WA WATAALAMU WA TEHAMA WIZARA YA AFYA NA TAASISI ZAKE WAFUNGULIWA"