Baadhi wa washiriki wa mafunzo ya hedhi salama wakifuatilia mada iliyokua ikiendelea katika Shule maalum ya watoto wasioona ya Bwigiri iliyopo Wilayani Chamwino Jijini Dodoma. |
Na.WAMJW, Chamwino
Jamii imetakiwa kuchukua hatua ikiwemo ya kutoa elimu sahihi katika makundi mbalimbali ikiwemo ya walemavu wa aina zote hususan wasioona.
Hayo yamesemwa leo na muelimishaji mwandamizi wa masuala ya hedhi salama Bi.Dhahia Mbaga kutoka shirika la kimataifa la Water Suppliers Sanitation Corraborative Council wakati wa mafunzo kwa walimu na walezi wa shule maalum ya watoto wasioona ya Buigiri iliyopo wilayani hapa katika kuelekea maadhimisho ya siku ya hedhi salama duniani.
Bi.Mongi amesema malengo ya mafunzo hayo ni kuongeza maarifa na kuweka mazingira rafiki kwenye vyoo ambapo vinatakiwa kuwa na usafi, maji yanayotirirka pamoja na chumba maalumu kwa ajili ya watoto wanaopevuka kwa kubadilisha vifaa vya hedhi.
Aidha, amesema katika chumba maalum kunatakiwa kuwe na sanduku la huduma ya kwanza ambayo itakua na dawa za kutuliza maumivu pindi wanapopata maumivu kutokana na hedhi.
Pia Bi Mbaga amesema wanaokuwa na maumivu makali wanatakiwa wapelekwe kwenye kituo cha huduma za afya kupata matibabu.
Hata hivyo aliongeza kuwa kufika katika shule hiyo ni pamoja na kuibua changamoto za hedhi salama kwani ni nyingi.
” kwani tunapokuwa na watoto waliopevuka na wenye ulemavu kunakuwa na changamoto nyingi zikiwemo za kuwa na vyoo vyenye kuwawezesha walemavu wa macho ambapo kuna ujenzi maalumu ambayo imeanishwa kwenye miongozo ya kitaifa ya shule kwenye masuala ya maji na masuala ya mazingira”. Alisisitiza Mbaga.
Vilevile alisema mafunzo katika shule hiyo watawafundisha walimu na wanafunzi kuweza kutengeneza taulo za kike kwa kutumia vifaa ambavyo vinapatikana katika eneo hilo na kwa bei rahisi.
Kwa upande wa unyanyapaa muelimishaji huyo alisema kuwa linakuja kutokuwa na taarifa sahihi hususani kwa wanaume kwani wanapaswa kujua ni jambo la kawaida na wapo baadhi ya wanaume hawana taarifa sahihi kwani na wanaume nao wanapevuka kwahiyo hayo ni mabadiliko ambayo hayawezi kuzuiliwa.
Maadhimisho ya siku ya hedhi salama duniani mwaka huu kitaifa yanatarajiwa kufanyika jijini Dodoma tarehe 28 mwezi Mei na kauli mbiu ya maadhimisho hayo “Ni wakati wa kuchukua hatua ili kuhakikisha hedhi salama kwa msichana/mwanamke”.
-Mwisho-
0 on: "WALIMU WA SHULE YA MAALUM YA WASIOONA WAPATIWA MAFUNZO YA HEDHI SALAMA"