Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimkabidhi mguu wa bandia moja kati ya walemavu wa miguu waliojitokeza katika hafla ya utoaji vifaa tiba saidizi kwa watu wenye ulemavu katika taasisi ya mifupa MOI, wakwanza ni Mkurugenzi wa Taasisi ya MOI, Dkt. Respicious Boniface na wa mwisho ni Mhe. Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na mmoja kati ya watu wenye ulemavu wa miguu Bw. John Gido wakati wa hafla ya utoaji vifaa tiba saidizi kwa watu wenye ulemavu katika taasisi ya mifupa MOI
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakisaidiana na Daktari kutoka Taasisi ya MOI kumvisha mguu wa bandia motto Patrick katika hafla ya utoaji vifaa tiba saidizi kwa watu wenye ulemavu katika taasisi ya mifupa MOI.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiteta jambo na Balozi wa India hapa nchini Mhe. Sandeep Arya katika hafla ya utoaji vifaa tiba saidizi kwa watu wenye ulemavu katika taasisi ya mifupa MOI.
Ugeni kutoka Ubalozi wa India, Watumishi wa Taasisi ya MOI na Baadhi ya watu wenye ulemavu wa miguu, wakifuatilia kwa makini hotuba kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu (Hayupo kwenye picha) wakati wa hafla ya utoaji vifaa tiba saidizi kwa watu wenye ulemavu katika taasisi ya mifupa MOI.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Balozi wa India hapa nchini Mhe. Sandeep Arya wakiwa katika picha yapamoja na viongozi kutoka Wizara ya Afya na Watu wenye ulemavuwakati wa hafla ya utoaji vifaa tiba saidizi kwa watu wenye ulemavu katika taasisi ya mifupa MOI.
SERIKALI
YAWAFUTA MACHOZI WALEMAVU 600 NCHINI
Na
WAMJW – DSM
SERIKALI
kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa
kushirikiana Ubalozi wa India chini ya Taasisi ya utengenezaji viungo bandia
BMVSS imewafuta machozi watu wenye ulemavu wa miguu nchini kwa kugawa miguu ya bandia kwa zaidi ya Watu 600.
Hayo
yamejiri mapema leo katika hafla ya utoaji vifaa tiba saidizi kwa watu wenye
ulemavu katika taasisi ya mifupa (MOI) iliyoongozwa na Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu.
Waziri
Ummy amesema kuwa licha ya kuwepo changamoto ya upungufu wa miguu bandia kwa
ajili ya wenye ulemavu, Serikali kupitia Wizara ya Afya itaendelea na juhudi za
kuhakikisha wenye uhitaji wa miguu hiyo wanapatiwa msaada.
“Tulitangaza
watu 500 waombe, lakini watu walioomba wamezidi 900 ambao wamejisajili, huku
miguu ambayo imepatikana ikiwa ni 600, inamaana watu 300 hatutaweza kuwafikia,
Serikali kupitia Wizara ya Afya itaangalia nanmna gani itawafikia hao 300”
alisema Waziri Ummy.
Aidha,
waziri Ummy amesema kuwa ajali za barabarani zimekuwa chanzo kikubwa kwa
Wananchi wengi kupoteza viungo, hivyo
kuleta janga la ulemavu hali inayorudisha nyuma jitihada za kuleta
maendeleo nchini.
“Ukizunguka
katika hospitali za Wilaya na Hospitali za Rufaa za Mikoa unaona idadi kubwa ya
watu waliopata ajali za barabarani. Mwaka 2014 Hospitali ya Moi ilipokea
wagonjwa wa ajali kati ya 200 mpaka 300, sasa hivi wanapokea wagonjwa wa ajali
za Barabarani takribani 500 mpaka 600” alisema Waziri Ummy.
Waziri
Ummy aliendelea kusema kuwa Serikali iko kwenye mpango wa kupeleka muswada
Bungeni kuhakikisha moja ya masharti ya kuwa dereva wa pikipiki ni lazima uwe
na umiliki wa Bima ya Afya ili kujihakikishia uhakika wa matibabu pindi ajali
inapotokea.
Mbali
na hayo Waziri Ummy ametoa maelekezo kwa wadau na viongozi mbali mbali kufuata
taratibu za kiafya ikiwemo kupata vipimo kabla ya kugawa viungo hivyo kwa jamii
jambo litalosaidia kulinda afya zao.
Nae,
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya MOI,
Dkt. Respicious Boniface ameishukuru Serikali za kuiwezesha Taasisi ya Moi
kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi, ikiwemo upatikanaji wa fedha za kununua
vifaa vya kisasa jambo lililosaidia kupunguza idadi ya wagonjwa waliotakiwa
kwenda kutibiwa nje ya nchi.
MWISHO.
0 on: "SERIKALI YAWAFUTA MACHOZI WALEMAVU 600 NCHINI"