Katibu Mkuu Wizara ya Afya akisema jambo kwa wajumbe wa Bodi ya Ushauri wa Hospitali za Rufaa za Mikoa (hawako pichani) katika Kikao kazi kilichofanyika jana Jijini Dodoma.
Wajumbe wa Bodi ya Ushauri wa Hospitali za Rufaa za Mikoa wakiwa katika kikao kazi.
Wajumbe wa Bodi ya Ushauri wa Hospitali za Rufaa za Mikoa wakiwa katika kikao kazi.
Na.WAMJW,Dodoma
Wajumbe wa bodi za ushauri za hospitali za rufaa nchini wametakiwa kutatua changamoto zilizopo kwenye hospitali zao ili wananchi wapate huduma zilizo bora
Rai hiyo imetolewa na Katibu Mkuu,Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Zainabu Chaula wakati akifungua kikao kazi cha uhamasishaji wa wajumbe wa bodi za ushauri za hospitali za rufaa za mikoa kinachofanyika jijini hapa
Dkt.Chaula alisema wizara inawategemea na kuwathamini wajumbe hao katika kuleta mabadiliko ya uimarishaji wa huduma za afya katika hospitali za mikoa zilipo katika maeneo yao hivyo wanatakiwa kuwa wabunifu.
“Nyie ndio macho yetu kule,tumewapa wajibu hivyo tunawategemea mtushauri na kuleta mafanikio katika maeneo yenu".Alisisitiza Dkt.Chaula
Aidha,aliwataka wabuni katika kuongeza vyanzo vya mapato ili hospitali hizo ziweze kuwahudumia wananchi ipasavyo na si kwenda hospitali za ngazi za juu“madaktari bingwa wanatengenezwa wananchi hawapaswi kwenda hospitali kubwa bali hospitali za rufaa"alisema Dkt.Chaula
Wakati huo huo Mganga Mkuu wa Serikali Prof.Mohhamad Bakari Kambi alisema wanatarajia mabadiliko makubwa katika rasiliamali watu hususan kwenye sekta ya afya kwa kuwa wabunifu.
"Tutawapima kwa utendaji na mafanikio yenu na hivyo tutapenda baadae muwe bodi tendaji ili muwe na uwezo mkubwa wa kufanya maamuzi na si ushauri kama ilivyo sasa.Alisema Prof.Kambi
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Tiba Dkt.Grace Maghembe alisema wanatambua mchango wa bodi hizo kwani ndio walezi kwenye hospitali za rufaa za mikoa hivyo watasaidiana panapotokea mapungufu ili kuweza kurekebisha kwa haraka.
Dkt.Maghembe aliwataka wajumbe hao kusaidia kwa utashi katika kuimarisha na kusimamia vyanzo vyanzo vya mapato yanayokusanywa pamoja na matumizi yake na kuzifanya hospitali za rufaa za mikoa kupunguza rufaa za hospitali kubwa na kuzifanya ziwe sehemu za kwanza za rufaa na kupunguza gharama za matibabu.
Kikao kazi hicho kinakutanisha wajumbe wa bodi za ushauri za hospitali za rufaa za mikoa kutoka mikoa kumi kutoka Tanzania bara
0 on: "BODI ZA HOSPITALI ZA RUFAA ZATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO "