Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Picha. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Picha. Onyesha machapisho yote

Jumatano, 12 Agosti 2020

WATOA HUDUMA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI KWA KUZINGATIA MAADILI.

- Hakuna maoni

Mkurugenzi Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Grace Magembe akiwasalimia wagonjwa waliokuwa wakisubiri huduma katika eneo la wagonjwa wa nje (OPD) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara.

Mkurugenzi wa tiba Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Grace Magembe akimjulia hali moja kati ya wagonjwa waliofika kupata huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara, pindi alipofanya ziara katika Hospitali hiyo.

Mkurugenzi Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Grace Magembe (wa katikati) akiwa pamoja na  Mkurugenzi wa uhakiki ubora wa huduma kutoka Wizara ya Afya Dkt.  Eliakim Eliud wakikagua muongozo  wa utoaji huduma kwa kwa Wauguzi, pindi walipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara.


Mkurugenzi Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Grace Magembe akiwa na Wataalamu wa Maabara katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara.
 
Mkurugenzi wa tiba Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Grace Magembe akiwa na Wataalamu wa Maabara katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara,  wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali hiyo.

Mkurugenzi Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Grace Magembe akikagua kadi inayoonesha hali ya idadi ya dawa zilizopo (Bin Card) katika chumba cha kuhifadhia dawa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara.

 

WATOA HUDUMA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI KWA KUZINGATIA MAADILI.

Na Rayson Mwaisemba, WAMJW- MANYARA

MKURUGENZI wa tiba Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Grace Magembe ametoa wito kwa Watoa huduma za Afya nchini kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia maadili wakati wa kumhudumia mgonjwa.

Dkt. Grace Magembe ametoa rai hiyo leo, wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za afya, na ujenzi wa miundombinu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara.

Dkt. Grace amesema kuwa, kwa kiasi kikubwa Serikali imewekeza kwenye ujenzi wa miundombinu, vifaa tiba na hali ya upatikanaji wa dawa, ikiwa ni sehemu ya maboresho ya utoaji huduma za afya bora kwa mwananchi katika jamii.

"Serikali imewekeza kwenye miundombinu, kwenye vifaa tiba, hali ya upatikanaji wa dawa, lakini Watumishi wanatakiwa wafanye kazi kwa weledi kwa kuzingatia maadili ya kazi zao wakati wa kumuhudumia mgonjwa " alisema Dkt. Grace.

Aliendelea kusema kuwa, Serikali imekuwa ikisisitiza sana, kuhusu maadili mazuri wakati wa utoaji huduma kwa wateja, pindi wanapokuja kupata huduma, hii inajumuhisha mapokezi yake, muda anaotumia kusubiri huduma, muda wa kurejesha majibu yake na kauli zinazotumika wakati wa utoaji huduma.

Hata hivyo, Dkt. Grace ametoa wito kwa viongozi wa hospitali kuwa na mpango madhubuti wa matengenezo ya vifaa tiba ili kuepuka ewezekano wa kusimama kwa baadhi ya huduma, hali itayopelekea wananchi kukosa huduma na upotevu wa mapato.

"Kitu kingine ambacho tunasisitiza katika hospitali ni kuwa na mpango madhubuti wa matengenezo ya vifaa tiba, vifaa ambavyo vimenunuliwa na Serikali ni vya gharama kubwa mnoo, fedha nyingi sana zimetumika, kwahiyo tunasisitiza kuwa na mpango wa matengenezo" alisema

Aidha, Dkt. Grace kwa kiasi kikubwa ameridhishwa na hali ya upatikanaji wa dawa katika maeneo alipofanya ziara, huku akitoa rai kwa Watoa huduma kuhakikisha mgonjwa anapoandikiwa dawa azipate dawa alizoandikiwa lakini pia azipate kwa kwa muda sahihi.

" tumeangalia tena suala la upatikanaji wa dawa, namna dawa inavyohifadhiwa, namna dawa inavyotumika, namna dawa inavyotoka chumba cha kuhifadhia mpaka inapomkuta mhitaji wodini, hii yote tumeifanyia kazi kwasababu tunataka hizo dawa zitumike kulingana na mahitaji yaliyotakiwa" alisema Dkt Grace.

Mbali na hayo, Dkt. Grace amesisitiza agizo la Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi juu ya kufanya kazi kwa juhudi na ushirikiano ili kupunguza vifo vya mama na mtoto, huku akisisitiza kuwa, kuweka mikakati thabiti katika mapambano dhidi ya vita hii, na kuweka wazi kuwa vifo vya mama na mtoto vitakuwa ni kigezo cha kuangalia uwajibikaji na utendaji kazi wa Waganga Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Waganga wafawidhi.

"Hatutaki kuona mama wa Kitanzania anakufa wakati analeta kiumbe Duniani, vifo vingi vinasababishwa na sababu ambazo zinaweza kuzuilika, lazima kila Mtumishi afanye kazi, kuanzia Mganga Mkuu wa Mkoa, Mganga Mkuu wa Wilaya, hospitali zote zilizopo ndani ya Mkoa wake, wote wafanye kazi kwa kushirikiana, wake na mkakati, sisi kama Wizara kwa kushirikiana na TAMISEMI tutaendelea kufuatilia tuone kama vifo vinapungua au la na hatua zitachukuliwa " alisema.

Nae, Mkurugenzi wa uhakiki ubora huduma Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Eliakim Eliud amesisitiza kuwa, kuongeza kazi za utoaji huduma kwa kuzingatia ubora wa huduma na kufuata miongozo ya kujikinga wakati wa kuwahudumia wagonjwa.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dkt. Damas Kayera ameweka wazi kuwa, Mkoa wa Manyara umeendelea kuwa ma rekodi nzuri juu ya hali ya upatikanaji wa dawa muhimu wa kufikia wastani wa 91%, jambo lililosaidia kupunguza malalamiko kwa wananchi wanaokuja kupata huduma.

"Mkoa unaendelea kuwa na rekodi nzuri ya ongezeko la dawa muhimu, zinazofuatiliwa na Wizara ya afya kwa kila kituo, ambapo kwa kipindi cha nusu mwaka 2020 kumekuwa na wastani wa 91%" amesema.

Mwisho.

Ijumaa, 14 Februari 2020

“TANZANIA NI SALAMA HAKUNA UGONJWA WA CORONA” - DKT. NDUGULILE

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jisnai, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na Waandishi wa Habari (Hawapo kwenye picha) wakati wa ziara yake Jijini Arusha,



“TANZANIA NI SALAMA HAKUNA UGONJWA WA CORONA” -  DKT. NDUGULILE

Na Englibert Kayombo, WAMJW, Arusha.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amewahakikisha Watanzania kuwa nchi bado iko salama na hakuna mgonwjwa yeyote mwenye ugonjwa wa Virusi vya Corona.

Dkt. Ndugulile ametoa kauli hiyo akiwa Jijini arusha katika Ziara zake za kikazi ambapo waandishi wa habari walimuuliza juu ya tetesi za uwepo wa ugonjwa huo nchini, pamoja na kutaka kufahamu ukweli wa taarifa za mtu anayedai kuwa na dawa za ugonjwa huo.

“Niseme tuu kuwa Tanzania mpaka sasa hivi bado tuko salama na hakuna mgonjwa yeyoteambaye ameripotiwa na amethibitika kuwa na ugonjwa” amesema Dkt Ndugulile.

Amesema kuwa Serikali imekuwa ikifuatilia taarifa mbalimbali za washukiwa na watu wote ambao tunawahisi kuwa na ugonjwa huo na tumeweza kuwapima na kubaini kuwa hawana ugonjwa.

“Sambamba na hilo tumeendelea kuchukua tahadhari mbalimbali na mimi niko katika Mkoa huu wa Arusha na nitaenda Kilimanjaro kwenda kuangalia utayari” amesmea Dkt. Ndugulile na kuendelea kusema “ Nimepita hapa leo nimeongea na uongozi na nimeridhika na maandalizi ambayo tunayo hapa katika Mkoa huu wa Arusha katika kudhibiti ugonjwa huo” Ameeleza Dkt. Ndugulile.

Akijibu kuhusu mtu ambaye anasema kuwa anayo dawa ya kutibu ugonjwa huo ambaye anajulikana kwa jina la Mosses Mollel maarufu kwa jina la “Nabii namba saba” aliyetoa taarifa za kuwa na dawa yenye uwezo wa kutibu virusi vya corona, Dkt Ndugulile amesema kuwa anazo taarifa za mtu huyo ambazo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari akijitangaza kuwa anayodawa ya kutibu ugonjwa huo na kumtaka athibitishe kauli yake.

“Kimsingi nimeiona hiyo taarifa ya huyo mtu  anayejiita Nabii Saba kuwa anayo dawa ya kutibu ugonjwa wa Corona ,ila hapa kwetu Tanzania hatuna maambukizi yoyote ya ugonjwa huyo ,tunachotaka huyo mtu  atuthibitishie uwezo wake wa kutibu huo ugonjwa wa Corona” Amesema Ndugulile

Ameongeza kuwa iwapo atashindwa kuthibitisha atachukuliwa hatua Kali za kisheria.
Amesema hadi sasa Serikali imetuma wataalamu wake kwenda kumsaka na kumhoji kama anavyo vibali Vya kutoa huduma ya Tiba na kujitangaza kuwa anatoa Huduma ya kutibu ugonjwa huo  hatari ambao hadi sasa mataifa bado yanahaha kusaka  Tiba ya ugonjwa huo.

Nabii Namba Saba ambaye ni mkazi wa Ngaramtoni Wilayani Arumeru,Mkoani Arusha amekuwa akijitangaza kuwa anayo dawa ya kutibu ugonjwa huo wa virusi vya corona na kuweka mawasiliano yake  kwenye mitandao .

Dkt. Ndugulile amesema kuwa mtu yeyote anayetoa tiba asili na mbadala kwanza ni lazima asajiliwe na mamlaka husika ambayo ni Wizara ya Afya, pili lazima dawa zake ziwe zimesajiliwa na Wizara ya Afya na kusisitiza kuwa nabii huyo pia anapaswa kuthibitisha amesajiliwa wapi na lini.

“Tuepuke kutoa kauli ambazo zinakwenda kuchanganya jamii, na endapo tutabaini mtu huyu hana sifa ambazo anasema kuwa nazo tutamchukulia hatua za kisheria” Amesema Dkt. Ndugulile.

HOSPITALI YA WILAYA MWANGA YAPEWA WIKI MBILI KUJA NA MKAKATI WA UPATIKANAJI WA VIPIMO MUHIMU VYA AFYA

- Hakuna maoni
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua kadi ya bima ya afya ngazi ya jamii iliyoboreshwa kutoka kwa mgonjwa aliyefika hospitali ya Wilaya ya Mwanga kupata huduma za afya.

 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (kulia) akifafanua jambo kwa watumishi  wa Wilaya ya Mwanga (hawapo pichani) kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Bw. Thomas Apson.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto)  akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Bw. Thomas Apson (kulia) mara baada ya kuwasili katika ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Mwanga.



HOSPITALI YA WILAYA MWANGA YAPEWA WIKI MBILI KUJA NA MKAKATI WA UPATIKANAJI WA VIPIMO MUHIMU VYA AFYA

Na WAMJW - Mwanga, Kilimanjaro.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ameutaka uongozi wa Hospitali ya Wilaya ya Mwanga kuandaa mkakati madhubuti utakaowawezesha kuwa na vipimo muhimu vya afya.

Dkt Ndugulile ametoa agizo hilo leo alipotembelea Hospitali ya Wilaya ya Mwanga kujionea hali ya utoaji huduma na kubaini kuwa hospitali hiyo haina vipimo vya damu, vipimo vya kemia pamoja vipimo vya CD4.

”Kwa miaka miwili sasa hakuna vipimo vya msingi katika hospitali hii, tunawakosesha huduma wananchi” amesema Dkt. Ndugulile

”Haiwezekani Hospitali kubwa ndani ya Wilaya kukosa vipimo vya msingi, haiwezekani mtu hapa sasa hivi anahitaji kipimo cha damu atoke hapa aende Hospitali ya Mawenzi Moshi kwa ajili ya vipimo” amesema Naibu Waziri Ndugulile.

Katika hatua za kutafuta ufumbuzi wa changamoto hiyo, Waziri Ndugulile ameushauri uongozi wa afya ndani ya Wilaya kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga kuhakikisha wanatenga fedha kwa ajili ya kununua vifaatiba hivyo ili wananchi waweze kupata huduma za vipimo ndani ya Wilaya ya Mwanga.

Aliendelea kushauri kuwa kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wao wanatoa mkopo wa majengo na vifaa kwa taasisi za umma na binafsi, mnaweza kuwafikia NHIF na kujadili kuhusu suala hili.

”Huko kwingine wanazitumia hizo fursa, kaeni na watu wa NHIF, Meneja wa NHIF kaa na viongozi wa Hospitali hii ikiwezekana mkubaliane hivyo vitu vipatikane kwa haraka” ameshauri Dkt. Ndugulile.

”Naamini mna wadau wa maendeleo ambao mnashirikiana nao katika mambo mbalimbali, timu ya afya ndani ya mkoa, wilaya pamoja na hospitali nawaombeni sana tuwe tunaomba vitu ambavyo vina manufaa kwa wananchi” amesisitiza Dkt. Ndugulile.

Awali akitoa salamu za wananchi wa Wilaya ya Mwanga, Mbunge wa Jimbo la Mwanga Profesa Jumanne Maghembe amesema kuwa changamoto ya kijiografia ndani ya Wilaya hiyo inachangia wananchi kukimbilia hospitali za Wilaya jirani ili kuweza kupata huduma.

”Wilaya yetu hii ina upande wa mlimani na huku tambarare, wananchi wengi walio huku tambarare wanaona ni bora kwenda Moshi kwa ajili ya matibabu kuliko kwenda juu mlimani iliko Hospitali” amesema Prof. Maghembe.

Hata hivyo Prof. Maghembe amesema kuwa tayari ndani ya Wilaya wameshaanza taratibu za kujenga Hospitali nyingine eneo la chini (tambarare) ili wananchi wanaoishi maeneo hayo waweze kupata huduma za afya ndani ya Wilaya ya Mwanga.

-Mwisho-

Ijumaa, 20 Desemba 2019

SERIKALI YADHAMIRIA KUBORESHA HUDUMA ZA RUFAA

- Hakuna maoni
Waziri Ummy, akieleza jambo wakati akiwa katika ziara ya kukagua hali ya utoaji  huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Honoratha Rutatinisibwa akitoa taarifa ya hali ya Afya katika Mkoa wa Tabora wakati wa ziara ya Waziri Ummy katika Mkoa huo.

Waziri wa Afya,Maendeleo  ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.@umwalimu akiongea na baadhi ya wanawake waliofika kupata huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.@umwalimu akikagua uboreshaji miundombinu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, pindi alipofanya ziara katika Mkoa huo.
Wananchi wa Tabora wakisikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwasilisha Salam kutoka kwa Mhe. Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Dkt.@MagufuliJP kwa wananchi hao.

Picha ya Pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.@umwalimu baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya na miundombinu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora.



SERIKALI YADHAMIRIA KUBORESHA HUDUMA ZA RUFAA

Na Rayson Mwaisemba WAMJW- TABORA

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imedhamiria kuboresha huduma za Rufaa katika Hospitali za Rufaa za mikoa kwa kuhakikisha inaboresha kwa kujenga miundombinu ya majengo ya dharura na ajali.

Hayo yamesemwa, na Waziri wa Afya, Mh. Ummy Mwalimu wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora.

" Sisi kama Serikali, tumedhamiria kuboresha huduma za Rufaa katika Hospitali za Rufaa za Mikoa, kwa kuhakikisha tunaweka miundombinu, hususan jengo la dharura na ajali ". alisema Waziri Ummy Mwalimu.

Hata hivyo, Waziri Ummy alisema Serikali imedhamiria kuboresha huduma za Afya kwa wananchi, kwa kutenga takribani Bilioni 8.8 kwa ajili ya ujenzi wa zaidi ya Vituo vya Afya 13, huku akieleza kuwa Hospitali za Wilaya za Sikonge na Uyui nazo zinaendelea kujengwa hali itakayosaidia kupunguza mzigo kwa Hospitali ya Mkoa.

"Sisi kama Serikali tumedhamiria kuboresha huduma za Afya, kuanzia miundombinu, Serikali tunajenga vituo vya Afya zaidi ya 13, ambayo takribani Bilioni 8.8 zimeshaingizwa na vingine nimeanza kutoa huduma lakini tunajenga Hospitali mbili za Wilaya ambazo ni Sikonge pamoja na Uyui" alisema

Licha ya kupunguza kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa Malaria nchini, Waziri Ummy ameagiza kupitia Maafisa Afya kutoa elimu kwa wananchi ili kutokomeza mazalia ya mbu waenezao Malaria, huku akisisitiza kuwa ni lazima Halmashauri kununua viuadudu vya kuangamiza viluilui katika mazalia ya mbu.

Mbali na hayo, Waziri Ummy aliipongeza timu ya Afya ya Mkoa kwa jitihada inazozichukua katika kuimarisha usafi wa mazingira hususan katika ujenzi na matumizi ya vyoo bora jambo litalosaidia kupunguza magonjwa ya kuhara, magonjwa ya tumbo na Kipindupindu.

"Ujenzi na matumizi ya vyoo Bora ndani ya mwaka mmoja mmetoka Asilimia 53.7 mpaka asilimia 59, lakini pia tumepunguza kaya ambazo hazina vyoo kabisa kutoka asilimia 7 mpaka asilimia 2" alisema.

Kwa upande mwingine, ameagiza asilimia 2 ya watu wasiokuwa na vyoo kutafutwa ili kuhakikisha wanajenga vyoo na kuvitumia kwa usahihi, huku akisisitiza wasiofanya hivyo ndani ya muda wa makubaliano wachukuliwe hatua za kisheria, alisisitiza.

Pia, Waziri Ummy alisema kuwa katika Mkoa wa Tabora vifo vya akina mama wajawazito vimepungua kutoka wajawazito 99 mpaka wajawazito 60 kwa mwaka huku akisisitiza Watoa huduma kuendelea kujituma ili kuhakikisha usalama wa mama na mtoto.

Aliendelea kusema, Wanawake ambao wanajifungulia katika vituo vya kutolea huduma za Afya katika Mkoa wa Tabora ni zaidi ya Asilimia 100%, huku kitaifa ikiwa ni asilimia 63, hivyo ametoa Wito kwa wanawake kuendelea kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma za Afya.

"Tumeona kwamba Wanawake ambao wanajifungulia katika vituo vya kutolea huduma za Afya katika Mkoa wa Tabora ni zaidi ya 100%, wakati kitaifa tunazungumizia asilimia 63 kwahiyo hongereni sana kwa kupunguza vifo, kutoka wajawazito 99 mpaka 60" alisema.

Mwisho.

Jumatatu, 16 Desemba 2019

MAOFISA AFYA WATAKIWA KUWAKINGA WANANCHI DHIDI YA MAGONJWA-DKT. SUBI

Mkurugenzi wa Kinga, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi akieleza jambo mbele ya Maafisa Afya wa Mikoa na Halmashauri, wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya usafi wa mazingira.

Afisa kutoka Idara ya Mazingira Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee naWatoto Bw. Anyitike Mwakitalima akieleza mafanikio mbali mbali yaliyopatikana kutokana na afua mbali mbali za usafi wa mazingira zinazotekelezwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Wadau.

Maafisa Afya kutoka Mikoa, Halmashauri na Wadau wakifuatilia kwa makini neno kutoka kwa Mkurugenzi wa Kinga, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi.


MAOFISA AFYA WATAKIWA KUWAKINGA WANANCHI DHIDI YA MAGONJWA-DKT. SUBI

Na Catherine Sungura, WAMJW - Dodoma

Maofisa afya wa mikoa na halmashauri wametakiwa kusimamia afya ya jamii kwenye maeneo yao ili wananchi wajikinge dhidi ya magonjwa yakuambukiza na yele yasiyoambukiza.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa kinga Dkt. Leonard Subi wakati akiongea na maofisa hao ambao wanakutana jijini hapa  kwa  kikao kazi cha siku tatu wakijadili utekelezaji wa maazimio yaliyotolewa kwenye mkutano mkuu wa kwanza mwaka jana  na  Waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.

“Mkutano huu ni wa pili mwaka huu,ni mkutano muhimu kwa maofisa afya kwani ndio wasimamizi wa shughuli za afya katika ngazi za jamii kwa kuhakikisha wananchi wanajikinga na maradhi, kula chakula bora kuishi makazi bora,usafi wa mazingira pamoja na kuwa vyoo bora”.Amesema Dkt. Subi

Aidha, amesema katika mkutano huu mambo mbali mbali yatajadiliwa ikiwemo  afya mazingira,usafi na uchafuzi wa mazingira na kila kinachotumiwa na kumzunguka  mwananchi ,pia wataangalia mabadiliko ya tabia nchi na kupata taarifa kutoka ngazi za mikoa ni jinsi gani walivyotekeleza majukumu yao.

“Maafisa afya muendelee kuishauri wizara kwa kutumia takwimu kwani tunatarajia mkutano huu mtabadilishana uzoefu  kutoka sehemu zenu za kazi,kama wizara tumekua tukitengeneza sera na miongozo mbali mbali ya kudhibiti maradhi yote yanayoweza kuathiri afya za binadamu hivyo kazi ya wizara ni kukusanya taarifa,kuchakata na kuzitolea miongozo na maelekezo”. Aliongeza Dkt. Subi.

Hata hivyo amesema maofisa hao wana majukumu ya kusimamia na  kulinda afya mipakani ili kusiingie magonjwa ya milipuko kutoka nje hususan  nchi za jirani pamoja na utoaji wa chanjo ambapo Tanzania ipo vizuri.

Mkutano huo ambao utafunguliwa kesho na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu umebeba Kauli mbiu isemayo “Huduma bora za afya mazingira na usafi ni kichocheo muhimu cha uchumi endelevu.


Jumamosi, 14 Desemba 2019

KITUO CHA AFYA KOME CHAFANYA UPASUAJI WA KWANZA

Bango la Kituo cha Afya Kome, linalotoa maelekezo ya Huduma zinazotolewa katika kituo hicho.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiongea na moja kati ya mama aliyefika kupata huduma katika kituo cha Afya Kome, Halmashauri ya Buchosa, Sengerema Mwanza.


KITUO CHA AFYA KOME CHAFANYA UPASUAJI WA KWANZA

Na.Catherine Sungura

Kituo cha afya Kome kilichopo halmashauri ya buchosa wilayani Sengerema kimefanikiwa kufanya upasuaji wa kwanza  wa dharura wa kumtoa mtoto tumboni na hivyo kumuokoa mama na mtoto wake.

Akiandika kwenye mtandao wa kijamii Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa kwa mara ya kwanza kituo hicho kimeweza kufanya upasuaji huo baada ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  kujenga “theatre” na kuweka vifaa tiba kwenye kituo hicho.

Waziri Ummy ameendelea kuandika kuwa chumba hicho cha upasuaji ambacho kipo kituoni hapo kitawasaidia akina mama wajawazito wa kisiwa cha kome watakaopata uzazi pingamizi na hivyo kutokufuata huduma hizo wilayani sengerema na hivyo kutokuvuka tena maji.

“Hakika tumedhamiria kuokoa maisha  ya akina mama wajawazito na watoto wachanga,tutaendelea kuchukua hatua ili kuhakikisha huduma za uzazi  za dharura ikiwemo ya upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni(CEmONC) zinapatikana katika vituo vyote vya afya vya umma ,mama na mtoto huyo mwenye uzito wa kilo 3 na nusu wanaendelea vizuri”Amesema waziri Ummy

Naye Mganga Mkuu wa halmashauri ya buchosha Dkt. Ernest Chacha amesema walimpokea mama huyo kituoni hapo siku ya ijumaa ambaye alikua akihudhuria kliniki kwenye zahanati moja huko kisiwani hakuweza kujifungua kawaida kwani alikua akikabiliwa na uchungu pingamizi kwani nyonga zake  hazikuwa zinapanuka hivyo ili kumuokoa ilibidi afanyiwe upasuaji kuweza kumuokoa mama pamoja na mtoto .

Dkt. Chacha ameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa uboreshaji wa vituo vya afya nchini ikiwemo kituo cha afya cha kome ambacho kipo kisiwani kwa kuboresha miundombinu kwa kujengewa chumba cha upasuaji pamoja na kuwekewa vifaa tiba hivyo kusaidia kuokoa maisha ya akina mama wajawazito na watoto wachanga hususan visiwani humo.

“Wananchi walikua wanapata adha kubwa sana ya kuvuka maji kutoka kisiwani na kufuata huduma kwenye hospitali ya wilaya iliyopo sengerema,tunamshukuru Waziri Ummy Mwalimu kwa kuiagiza MSD kutufungia taa kwenye chumba cha upasuaji wakati wa ziara yake hivi karibuni visiwani hapa kwani tumeweza kuokoa maisha ya huyu mama muda mfupi baada ya taa hizo kufungwa”Amesema Dkt. chacha

Hivi karibu waziri wa afya alitembelea kisiwa hicho na kuwaahidi  kuwapatia xray mashine ya kidigitali  kwenye kituo hicho cha afya na kuwataka MSD kufunga taa kwenye chumba hicho cha upasuaji mara moja.

Kisiwa cha kome kimeongeza  idadi ya akina mama wanaojifungulia  kwenye vituo vya afya  kwa  asilimia 80  kwa mwaka ambapo wastani akina mama  50 wanajifungulia kwa mwezi