Like us on Facebook

Powered by Blogger.

SERIKALI YAIMARISHA UPATIKANAJI WA VIPIMO VYA UGONJWA WA DENGUE

Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Mohammad Bakari Kambi akizungumza jambo kuhusu ugonjwa dengue na waandishi wa habari (hawapo pichani). ...

Search This Blog

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Yaliyojiri

Friday, May 17, 2019

SERIKALI YAIMARISHA UPATIKANAJI WA VIPIMO VYA UGONJWA WA DENGUE

- No comments
Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Mohammad Bakari Kambi akizungumza jambo kuhusu ugonjwa dengue na waandishi wa habari (hawapo pichani).

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Dkt. Yudas Ndungile akizungumza jambo na waandishi wa habari (hawapo pichani).
Picha ya pamoja Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohhamad Bakari Kambi (meza kuu) akizungumza na waandishi wa habari.


Na WAMJW - DSM


Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeendelea kuimarisha upatikanaji wa vipimo vya ugonjwa wa Degue kwa kununua vipimo 30,000 kwa ajili ya kupima ugonjwa huo.

Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohhamad Bakari Kambi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mapema leo katika ofizi ndogo za Wizara Jijini Dar Es Salaam.

Prof. Kambi amesema kuwa vipimo hivyo tayari vimeshanunuliwa na vitaingia nchini hivi karibuni na kusambazwa kwenye vituo vya umma JIjini Dar Es Salaam pamoja na mikoa mingine yenye athari za ugonjwa huo.

Amesema kuwa ugonjwa wa dengue hauna chanjo wala tiba ya moja kwa moja na kuwataka wananchi kuacha kutoa taarifa za upotoshaji kuhusu tiba za ugonjwa huo.

“Niwakumbushe tena wananchi kinga ni bora kuliko tiba, jikinge na ugonwja huu wewe mwenyewe, kaya na familia yako pamoja na jamii kwa ujumla” amesema Prof. Kambi.

Mganga Mkuu amesema kuwa mpaka sasa vituo vinavyopima ugonjwa wa homa ya Dengue katika Mkoa wa Dar es Salaam ni Muhimbili, Maabara kuu Muhimbili, Amana, Temeke, Mwananyamala, Sinza, Vijibweni, Mnazi mmoja, Lugalo, Mbagala, FFU Ukonga. Katika mkoa wa Tanga; vituo vya Bombo na Horohoro, vituo vingine ni Tumbi Mkuranga, Utete Rufiji na Mafia, Morogoro na Manyara Aidha natambua vipo pia vituo binafsi vinavyotoa huduma za upimaji. Katika mikoa mingine ufuatiliaji unaendelea na hatujapa wagonjwa wenye dalili za Homa ya Dengue.

Aidha Prof. Kambi amesema kuwa Wizara inatambua juhudi zinazofanywa na Mkoa wa Dar Es Salaam na kuwapongeza kwa kazi kubwa wanayofanya ya udhibitiwa ugonjwa huo kupitia zoezi la kunyunyizia dawa viuadudu (Biolarvicides) kwa ajili ya kuangamiza mazalia ya mbu sambamba na elimu ya kujikinga dhidi ya ugonjwa huo.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Dkt. Yudas Ndungile Amesema kuwa idadi kubwa ya wagonjwa wanaojitokeza katika vituo vya afya kupata vipimo ni kutokana na wananchi kupata uelewa wa ugonjwa huo baada ya kupatiwa elimu dhidi ya ugonjwa huo.

“Tumepita kwenye maeneo ya kata zenu kufanya ueleimishaji wa namna ya kujikinga na kutambua dalili za ugonjwa huu” amesema Dkt. Ndungile na kuendelea kusema kuwa vyombo vya habari vimetoa mchango mkubwa katika kuelimisha wananchi dhidi ya ugonjwa wa dengue.

Aidha Dkt. Ndungile amesema kuwa kwa kushirikiana na Wizara ya Afya wameweza kuandaa vituo vya upimaji wa homa ya dengue ambapo huduma za upimaji zinatolewa bure.

Mwisho

Friday, May 10, 2019

WAANDISHI WA HABARI WAELIMISHWA KUHUSU USALAMA WA BARABARANI

- No comments
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wabunge katika Usalama Barabarani Mhe. Adad Rajab (kushoto) akigawa vitendea kazi kwa mwandishi wa habari wakati wa mafunzo ya usalama barabarani kwa waandishi wa habari Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wabunge katika Usalama wa Barabarani nchini Mheshimiwa. Adad Rajab (Mbunge wa JImbo la Muheza) akisema jambo kwa washiriki wa mafuzo ya usalama barabarani kwa waandishi wa habari yaliyofanyika Jijini Dodoma.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Tingest Mengenstu akiwasilisha hotuba yake wakati wa mafunzo ya Usalama wa Barabarani kwa waandishi wa habari yaliyofanyika  Jijini Dodoma.
 
Maafisa wa Polisi wakisikiza mada zinazoendelea katika mafunzo ya Usalama wa Barabarani kwa waandishi wa habari , Jijini Dodoma.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma Afande. Nuru Selemani Akizungumza jambo na washiriki wa mafunzo ya Usalama Barabarani (hawapo pichani) yaliyofanyika Jijini Dodoma.
icha ya washiriki wa mafunzo ya Usalama wa Barabarani kwa waandishi wa habari.
Na. WAMJW – Dodoma.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Shirikia la Afya Duniani (WHO) wamefungua rasmi programu ya mafunzo ya usalama barabarani kwa waandishi wa habari katika jitihada za kuelimisha jamii juu ya usalama wa barabarani na kuepuka ajali nchini.

Mafunzo hayo ambayo yamefunguliwa rasmi na Mwenyekiti wa Mtandao wa Wabunge katika Usalama Barabarani nchini Mheshimiwa Adad Rajab (Mbunge wa Jimbo la Muheza) yanaenda sambamba na maadhimisho ya wiki ya usalama barabarani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Mei 6 – 12 kila mwaka huku kwa mwaka huu yakiwa na kauli mbiu “Uongozi kwa usalama wa barabarani”

“Mafunzo hayo yana umuhimu kwa waandishi ili kuwawezesha kupasha habari za ajali barabarani  na kupunguza ajali hizo nchini” alisema Mhe. Adad.

Naye Mwakilishi Mkazi wa WHO nchini Tanzania Dkt. Tingest Mengestu amesema kuwa vifo vitonakavyo na ajali badoni tishio nchini na duniaini kwa ujumla huku akiiomba Serikali kuweka juhudi madhubuti juu ya suala hilo.

“Licha ya hatua mbalimbali ambazo zimechukuliwa, bado vifo vitokanavyo na ajali barabarani vimeendelea kuongezeka, takwimu zinaonyesha Duniani kwa mwaka kuna vifo milioni 1.35 vinavyosababishwa na ajali” amesema Dkt. Mengestu.

Akaendelea kwa kusema kuwa ajali za barabarani sasa ndizo zinazoongoza kusababisha vifo vya watu wenye umri mdogo huku akitaja waathirika zaidi ni kundi la wenye umri wa miaka 5 – 29.

Dkt. Mengestu amesema kuwa ulimwenguni, vifo vinavyotokana na ajali za barabarani, kwa upande wa watembea kwa miguu na waendesha baiskeli vimefikia asilimia 26 na kwa waendesha pikipiki pamoja na abiria vimefikia asilimia 28.

Hatari ya vifo vitonakavyo na ajali za barabarani imeendelea kuwa juu mara tatu zaidi katika nchi zenye kipato cha chini. Huku takwimu zikionyesha Bara la Afrika kuwa na ongezeko kubwa la ajali (Asilimia 26.6 kati ya watu 100,000), na Bara la Ulaya likiwa chini kwa nchi za (Asilimia 9.3 kati ya watu 100,000)

Akizungumzia takwimu za ajali za barabarani kwa Mkoa wa Dodoma, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoani humo Afande Nuru Selemani amesema kwa mwaka 2018 ajali za barabarani zilikuwa 350 zilizohusisha magari 155 na pikipiki 195, huku kwa mwaka huu ajali zilizotokea mpaka sasa zikiwa ni 75.

Afande Selemani amesema kuwa Kikosi cha Trafiki Polisi kimejipanga kuhakikisha Sheria za Usalama Barabarani zinafuatwa ili kupunguza ajali za barabani nchini na wale ambao watakuwa wamehusika kwa uzembe na kusababisha ajali wanachukuliwa hatua madhubuti.

“Kupitia mafunzo haya tunaamini tunaweza kushirikaina vizuri na waandishi wa habari ili kuweza kupaza sauti na kuwaelimisha na kuwakumbusha watumiaji wa barabara kuzingatia Sheria za usalama barabarani na kuweza  kupunguza ajali za barabarani” alisema Afande Sulemani.

Thursday, May 9, 2019

TAHADHARI YA HOMA YA DENGUE YAZIDI KUTOLEWA

- No comments
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Kambi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kuwepo kuendelea kuwepo kwa ugonjwa wa Homa ya Dengue nchini.

Baadhi ya waandishi wa habari waliojitokeza kusikiliza tamko la kuhusu kuwepo kwa ugonjwa wa Homa ya Dengue nchini wakati likitolewa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Kambi Jijini Dodoma.


NA WAJMW-DODOMA

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imezidi kutoa tahadhari ya  kuwepo kwa ugonjwa wa homa ya Dengue nchini hususani katika Jiji la Dar Es Salaam na Tanga.

Tahadhari hiyo imetolewa leo na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Kambi wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za wizara hiyo zilizoko jijini Dodoma.

Prof. kambi amesema hadi kufikia tarehe 6 Mei 2019, kati ya watu waliopimwa, wagonjwa 1237 wamethibitishwa kuwa na virusi au walikwishapata ugonjwa wa Dengue na kati yao 1150 ni kutoka Dar Es Salaam, 86 ni kutoka Tanga na mtu mmoja kutoka Singida.

Aidha, Prof Kambi amesema takwimu za ugonjwa wa Dengue kwa kipindi cha Januari hadi Aprili 2019 zinaonesha mwenendo wa ugonjwa huu kuwa na idadi ya wagonjwa 1237, vifo vya watu wawili na kuongeza kuwa waliofariki walikua na maradhi mengine.

Pamoja na hayo Mganga Mkuu huyo wa Serikali amelipongeza jiji la Dar Es Salaam kwa kuanza kunyunyizia dawa viuadudu (Biolarvicides) kwa ajili ya kuangamiza mazalia ya mbu ili kupambana na ugonjwa huu.

Vile vile amesema Wizara inaelekeza Mikoa na Halmashauri zote nchini kuendelea kuchukua hatua katika kudhibiti ugonjwa huu ikiwa ni pamoja na kufukia madimbwi ya maji, kunyunyizia dawa ya kuua viluwiluwi, kuondoa vitu vinavyosababisha mazalia ya mbu, kufyeka vichaka, kufunika mashimo ya maji taka kwa mifuniko pamoja kusafisha gata za paa la nyumba na kutoruhusu maji kusimama.

Prof. Kambi amesema Wizara kwa kushirikiana na Mikoa na Halmashauri zote nchini itaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kudhibiti ugonjwa huu ikiwa ni pamoja na kuendelea kuangamiza mazalia ya mbu na viluwiluwi, kuweka mpango wa dharura wa miezi sita kuanzia Mei mpaka Oktoba ili kukabiliana na ugonjwa huu. Pia amesema Serikali imenunua Vitendanishi vyenye uwezo wa kupima wagonjwa 1870 na vimesambazwa kwenye vituo maalum vya ufuatiliaji wa ugonjwa huu nchini kote.

Mwisho Prof. Kambi amewataka wananchi kuendelea kuchukua hatua za kujikinga kuumwa na mbu kwa kuvaa nguo ndefu, kutumia vyandarua vyenye viuatilifu, kutumia dawa za kufukuza mbu na kuweka nyavu kwenye madirisha na milango ya nyumba za kuishi ili kukabiliana na ugonjwa huu.

MWISHO

Wednesday, May 8, 2019

HOTUBA YA WAZIRI UMMY MWALIMU KUHUSU MAKADIRIO YA BAJETI YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2019-2020

- No comments
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Ally Mwalimu akiwasilisha makadirio ya Bajeti ya Wizara yake katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mei, 07, 2019 Jijini Dodoma.

 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akijibu hoja za wabunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mei 07, 2019.