Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatatu, 5 Machi 2018

MADAKTARI BINGWA TANZANIA KUFANYA KAZI NA MADAKTARI BINGWA KUTOKA NCHINI PALESTINA.

- Hakuna maoni
Waziri wa Afya,maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu  kulia akibadilishana hati ya makubaliano ya kuimarisha mifumo ya afya nchini Tanzania na Balozi wa Serikali ya Taifa la Palestina Bw. Hazem Shabat kushoto wakati wa kutia saini makubaliano hayo yalioyafanyika leo jijini Dar es salaam.

Balozi wa Serikali ya Taifa la Palestina Bw. Hazem Shabat katikati akiongea na waandishi wa habari mara baada ya makubaliano ya kuimarisha mifumo ya afya nchini Tanzania wakati wa kutia saini makubaliano hayo yalioyafanyika leo jijini Dar es salaam kulia ni Waziri wa Afya,maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu

Waziri wa Afya,maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu  kulia akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kutia saini makubaliano ya kuimarisha mifumo ya afya nchini Tanzania kati ya Serikali ya Taifa la Palestina na Serikali ya Tanzania yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam Kushoto ni Balozi wa Serikali ya Taifa la Palestina Bw. Hazem Shabat.

Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto wakifuatilia kwa makini utiaji saini makubaliano ya kuimarisha mifumo ya afya nchini Tanzania kati ya Serikali ya Taifa la Palestina na Serikali ya Tanzania yaliyofanywa na Waziri wa afya Ummy Mwalimu na Balozi wa Serikali ya Taifa la Palestina Bw. Hazem Shabat hawapo pichani.

NA WAMJW-DAR ES SALAAM. 

MADAKTARI Bingwa wa magonjwa mbalimbali hapa nchini watashirikiana na madaktari bingwa kutoka nchini Palestina katika kuimarisha matibabu ya kibingwa katika hospitali mbalimbali hapa nchini ambayo bado hayakidhi viwango ili kutoa huduma bora kwa Watanzania.


Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa kutia saini makubaliano ya kuboresha mifumo ya afya nchini kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya Palestina leo jijini Dar es salaam.

“Tumejitahidi kupunguza rufaa za kwenda kutibiwa nje ya nchi kwa asilimia 50 hivyo katika juhudi za kumaliza kabisa rufaa za nje tumekubaliana na wenzetu wa Palestina kwamba watatuletea madaktari bingwa kutoka kwao ili kuweza kutibu baadhi ya magonjwa ambayo kwetu tuna changamoto za utaalam wa kutibu magonjwa hayo” alisema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa Serikali ya Palestina kupitia makubaliano  hayo wamekubaliana kuleta  madaktari  bingwa wa kutibu mifupa ya uti wa mgongo na fahamu  kwani nchi hiyo ina wataalam wengi wa magonjwa hayo.

Kwa mujibu wa Waziri Ummy amesema kuwa katika licha ya kufikia asilimia 80 katika upatikanaji wa dawa nchini makubaliano hayo pia yatalenga  kuimarisha uzalishaji wa dawa pamoja na chanjo hasa za magonjwa yasioambukiza ikiwemo kisukari,shinikizo la damu na saratani kwani vinaongeza idadai kubwa ya vifo nchini.

Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya wamekubaliana na Serikali ya Palestina  kuimarisha maendeleo ya  mifumo ya Tehama na Mawasiliano kwani ndio chachu ya kuimarisha Sekta ya afya hasa katika nchi zinazoendelea.

Kwa upande wake Balozi wa Serikali ya Taifa la Palestina Bw. Hazem Shabat amesema kuwa wamefurahishwa kuingia mkataba huo na Serikali ya Tanzania kwani wanahitaji kwa nia ya dhati kuisaidia sekta ya afya hapa nchini.

“Licha ya kukubaliana  kuleta madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali Tanzania pia tumekubaliana kubadilishana wataalam kwani kuna muda madaktari wa Tanzania kuja nchini Palestina kujifunza zaidi juu ya matibabu ya kibingwa yanayofanyika nchini kwetu” alisema Bw. Shabat.

 


Alhamisi, 1 Machi 2018

WAZIRI UMMY AKUTANA NA UGENI KUTOKA NCHI YA UTURUKI.

- Hakuna maoni


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu akutana na ugeni kutoka nchini Uturuki ukiongozwa na Balozi wao Dkt. Ali Daoutoglu mapema leo katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam.
Ugeni huo umejadili namna yakuboresha Sekta ya Afya nchini hususani katika kuboresha huduma za dharura, uzalishaji wa dawa na ubadilishanaji uzoefu wa Wataalamu wa Afya kati ya nchi hizo mbili.
Balozi Ali Daoutoglu ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tazania na ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano katika kuimarisha Sekta ya Afya nchini.