“Tumejitahidi kupunguza rufaa za kwenda
kutibiwa nje ya nchi kwa asilimia 50 hivyo katika juhudi za kumaliza kabisa
rufaa za nje tumekubaliana na wenzetu wa Palestina kwamba watatuletea madaktari
bingwa kutoka kwao ili kuweza kutibu baadhi ya magonjwa ambayo kwetu tuna
changamoto za utaalam wa kutibu magonjwa hayo” alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa Serikali
ya Palestina kupitia makubaliano hayo
wamekubaliana kuleta madaktari bingwa wa kutibu mifupa ya uti wa mgongo na
fahamu kwani nchi hiyo ina wataalam
wengi wa magonjwa hayo.
Kwa mujibu wa Waziri Ummy amesema kuwa
katika licha ya kufikia asilimia 80 katika upatikanaji wa dawa nchini makubaliano
hayo pia yatalenga kuimarisha uzalishaji
wa dawa pamoja na chanjo hasa za magonjwa yasioambukiza ikiwemo
kisukari,shinikizo la damu na saratani kwani vinaongeza idadai kubwa ya vifo
nchini.
Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa
Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya wamekubaliana na Serikali ya
Palestina kuimarisha maendeleo ya mifumo ya Tehama na Mawasiliano kwani ndio
chachu ya kuimarisha Sekta ya afya hasa katika nchi zinazoendelea.
Kwa upande wake Balozi wa Serikali ya
Taifa la Palestina Bw. Hazem Shabat amesema kuwa wamefurahishwa kuingia mkataba
huo na Serikali ya Tanzania kwani wanahitaji kwa nia ya dhati kuisaidia sekta
ya afya hapa nchini.
“Licha ya kukubaliana kuleta madaktari bingwa wa magonjwa
mbalimbali Tanzania pia tumekubaliana kubadilishana wataalam kwani kuna muda
madaktari wa Tanzania kuja nchini Palestina kujifunza zaidi juu ya matibabu ya
kibingwa yanayofanyika nchini kwetu” alisema Bw. Shabat.
0 on: "MADAKTARI BINGWA TANZANIA KUFANYA KAZI NA MADAKTARI BINGWA KUTOKA NCHINI PALESTINA."