Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB)
akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wa Habari (Hawapo kwenye Picha), wakati wa
Maazimisho ya siku ya Kifua Kikuu Duniani, tukio limefanyika mapema leo katika
ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dodoma.
Kundi
la Waandishi wa Habari likifuatilia kwa ukaribu tamko la Kifua Kikuu (TB)
lililokuwa lililotolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB) katika ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dodoma
mapema leo.
Na WAMJW-Dodoma.
TAMKO LA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,
WAZEE NA WATOTO UMMY MWALIMU KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA KIFUA
KIKUU DUNIANI MACHI 24 - LEO MJINI DODOMA
# Kifua Kikuu(TB) ni ugonjwa wa kuambukiza unaoongoza kwa kusababisha vifo vingi Duniani.
#
Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani(WHO) inakadiriwa kuwa
zaidi ya watu milioni 10.4 huugua Kifua Kikuu kila mwaka Duniani na
Milioni Moja kati ya hao ni watoto wenye umri chini ya miaka 15.
#
Tafiti nyingi zinaonesha kuwa karibia theluthi moja ya Watanzania
tayari wamepata maambukizo ya Kifua Kikuu na wanaishi na vimelea mwilini
mwao.
# Kauli mbiu ya mwaka huu inasema *" Viongozi Tuwe Mstari wa Mbele Kuongoza Mapambano ya Kutokomeza TB."*
#Nchini Tanzania kila mwaka jumla ya watu 160,000 wanakadiriwa kuwa na ugonjwa wa Kifua Kikuu.
# Nitoe wito kwa viongozi wa ngazi zote kuifanya vita dhidi ya TB kuwa agenda muhimu na ya kipaumbele.
#
Napenda kuwakumbusha TB inatibika na kupona kabisa, dawa zake
zinatolewa bure na zinapatikana sehemu zote nchini katika vituo vya Umma
na Binafsi.
# Serikali
imechukua hatua mbalimbali kukabiliana na tatizo la Kifua Kikuu nchini
ikiwemo kuimarisha uchunguzi na ugunduzi wa Kifua Kikuu katika Vituo vya
Afya.
# Serikali na
wadau mbalimbali tunaendelea na utekelezaji wa kampeni za uhamasishaji
na upimaji wa Wananchi katika maeneo ya migodi, makazi duni kwenye miji
mikubwa, magereza na shule za bweni.
#
Pia Serikali imezindua dawa mpya za TB za watoto ili kuhakikisha
zinakidhi matakwa ya Shirika la Afya Duniani ( WHO), dawa hizo mpya ni
za watoto za mseto ( RHZ/RH) zilizoboreshwa na tayari zimeshawasili
nchini na tumeanza kuzisambaza kwenda Mikoani na Halmashauri zote
nchini.
# Nawaagiza
waganga wafawidhi wote wa hospitali na vituo vya huduma kuhakikisha
watoto wote wanaoanza shule za bweni wanafanyiwa uchunguzi wa TB
kikamilifu kabla ya kuanza masomo.
#Ni
marufuku kwa Madaktari kujaza fomu za uchunguzi wa Afya bila kupima
wanafunzi husika. Kufanya hivyo ni kuliangamiza kwa makusudi Taifa kwa
uzembe ambao hauwezi kuvumilika.
# Serikali inatambua umuhimu wa ushirikishwaji wa jamii katika mapambano ya kutokomeza TB.
#Mpaka
sasa takribani watoa huduma1530 kati ya 5000 katika ngazi ya jamii
ambao wamepata mafunzo ya muda mfupi ya Kifua Kikuu wanawezeshwa ili
kuibua wagonjwa wa TB na kuwafuatilia watoto wanaopata matibabu katika
maeneo yao.
0 on: "ALIYOYASEMA WAZIRI UMMY KATIKA SIKU YA KIFUA KIKUU (TB) DUNIANI"