Baadhi ya wadau wa Sekta ya afya wakifuatilia kwa
makini Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu hayupo pichani wakati wa uzinduzi wa dawa ya kutibu kifua kikuu kwa
watoto wadogo kueleka maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu tarehe 24 Machi 2019 .
NA WAMJW-DAR ES SALAAM.
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya
imetenga shilingi bilioni 5 kwa ajili ya kununua mashine za kupima vipimo vya
ugonjwa wa kifua kikuu katika zahanati na vituo vya afya nchini.
Hayo yamezungumzwa na Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa
uzinduzi wa dawa za kutibu ugonjwa wa Kifua Kikuu kwa watoto kuanzia umri wa
miaka 14 kushuka chini leo jijini Dar es salaam.
"Serikali imadhamiria kupambana
na ugonjwa wa Kifua Kikuu hivyo tumetenga shilingi bilioni 5 kwa ajili ya
kuongeza mashine nyingine za kufanya uchunguzi kwa haraka vya ugonjwa wa
Kifua Kikuu zinazoitwa Genexpert " alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa
marufuku kwa watoa huduma kutoa matibabu ya Kifua Kikuu kwa gharama yoyote
kwani huduma hiyo ni bure.
Kwa mujibu wa Waziri Ummy amesema
kuwa marufuku kwa waganga wa kienyeji kuwashikilia wagonjwa wa Kifua kikuu na
badala yake wawaruhusu waende hospitali kwa ajili ya msaada wa haraka.
Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa
takribani watu laki moja na 60 wana maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu
kwa makadirio ya mwaka 2016.
Sambamba na uzinduzi wa dawa hizo
Waziri Ummy amegawa mashine nyingne za Genexpert kwa ajili ya kufanyia
uchunguzi wa makohozi ili kugundua kuna maambukizi au hapana kwa hospitali
za ,Kairuki, Agakhan, Regency , TMJ na Indumandal ambazo kila
mashine moja inagharimu shilingi milioni 34 .
Aidha Waziri Ummy ametoa rai kwa
wazazi na walezi wa watoto kwenda hospitali mara wanapoona dalili moja wapo ya
TB ikiwemo kuumwa mara kwa mara kwa muda wa wiki mbili, kukosa furaha, mtoto
kulia mara kwa mara, kupungua uzito , kuchelewa kukua na kikohozi cha mara kwa
mara.
|
0 on: "SERIKALI YATENGA SHILINGI BILIONI TANO KWA AJILI YA KUNUNUA MASHINE NYINGINE YA KUPIMA VIPIMO VYA TB. "