Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatano, 21 Machi 2018

MAJUMUHISHO KIKAO MAWAZIRI WA ECSA
 Mkutano wa 65 wa Jumuiya ya Mawaziri wa Afya wa Nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini ECSA umemalizika leo jijini hapa kwa nchi wanachama kukubaliana maazimio mbali mbali yanayolenga  kutekeleza kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza kama vile kisukari, saratani, magonjwa ya moyo na ya mfumo wa hewa.

Akizungumza wakati wa kufunga mkutano huo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema makubaliano hayo yamelenga kuimarisha na kuboresha sekta hiyo na afya ya wananchi kwa ujumla.

Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa  wamekubaliana pia kuongeza uwajibikaji kwenye afya ya mama na mtoto ili kuepusha vifo vya mama na mtoto vinavyotokana na uzazi.

“Tumekubaliana kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza tumegundua katika nchi hizo magonjwa
yanayoongoza ni pamoja na kisukari, saratani, magonjwa ya moyo na ya mfumo wa hewa" alisema Waziri Ummy.

Kwa mujibu wa Waziri Ummy amesema kuwa Suala lingine walilokubaliana ni kutilia mkazo suala la heshima kwa wajawazito kwa sababu mawaziri wameshauri pia Tanzania kukitambua Chuo cha Upasuaji cha Afrika Mashariki, Kati na Kusini.  

Waziri Ummy ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, amesema wamkubaliana wamekubaliana pia kuimarisha ushirikiano na ulinzi katika maeneo ya mipaka.

0 on: "MAJUMUHISHO KIKAO MAWAZIRI WA ECSA"