Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumanne, 27 Machi 2018

DKT. MAGUFULI ATHIBITISHA UWEPO WA DAWA ZAKUTOSHA



ILI kufikia katika uchumi wa kati kwakutumia sekta ya viwanda Serikali inatak iw a kujikita katika kuimarisha sekta ya afya kwa watanzania ili kuwa na rasilimali watu wenye afya njema kwa ajili yakuleta mafanikio hayo kupitia viwanda.
Hayo yamesemwa na Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa uzinduzi wa magari 181ya kusambazia dawa uliofanyika leo katika Bohari Kuu ya Dawa ya Taifa (MSD) jijini Dar es salaam.
“Tunatakiwa kuwekeza kwenye uchumi wa Viwanda ili tufikie uchumi wa kati hivyo ni lazima tuwekeze kwenye sekta ya afya kwa kiwango kikubwa ili kuwa na wananchi wenye afya njema tayari kutumikia viwanda vyetu kwa muda wote” alisema Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli amesema kuwa Tanzania inatakiwa kujijengea viwanda vya dawa na vifaa tiba hapa nchini ili fedha zinazotumika kununua bidhaa hizo nje ya nchi zirudi mikononi kwa watanzania wenyewe pamoja na kutoa ajira kupitia viwanda hivyo.
Mbali na hayo Rais Magufuli amesema kuwa katika kuimarisha Sekta ya afya Serikali imetenga shilingi Bilioni 269 za kununua dawa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 kutoka bilioni 31 katika bajeti ya fedha mwaka 2016/2017.
Kwa upande wake Waziri wa afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa katika kuimarisha Afya ya mama na Mtoto Serikali imepunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa asilimia 60 kutoka asilimia 20 ya upunguzaji wa vifo hivyo.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa fedha zilizotengwa kwa ajili ya dawa zina mawanyo ikiwemo asilimia 42 zahanati na vituo vya afya ,asilimia 16 zinatumika kwa chanjo za watoto ,asilimia 10.2 zianenda hospitali za wilaya ,asilimia  6.8 zinatumia hospitali za mikoa ,asilimia 3.4 zinaenda hospitali maalum na asilimia 3 zinatumika kwa ajili ya dawa za saratani.

0 on: "DKT. MAGUFULI ATHIBITISHA UWEPO WA DAWA ZAKUTOSHA"