Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulileakitoa neno mbele ya Kamati ya Afya na Huduma za Jamii (Hawapo kwenye picha) wakati wa Semina ya Kifua Kikuu (TB) iliyoandaliwa na kuratibiwa na Mpango wa
Taifa wa kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma Wizara ya Afya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akifafanua shughuli na vitengo mbali mbali vinavyopatikana ndani ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto - Idara kuu ya Afya.
Waheshimiwa wa Bunge walio katika kamati ya Afya na Huduma za Jamii, wakifuatilia kwa umakini semina ya masuala ya TB iliyoandaliwa na Mpango wa
Taifa wa kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma Wizara ya Afya.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akifuatilia kwa ukaribu elimu juu ya ugonjwa wa Kifua Kikuu(TB) iliyokuwa ikitolewa, pembeni yake ni Mwenyekiti wa kamati ya Afya na huduma za jamii na Mbunge wa Chemba Mhe. Juma Nkamia.
Na WAMJW. Dodoma
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amewahasa viongozi nchini kote hususani viongozi wa Siasa kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha mapambano dhidi ya ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB), kutokana na ukaribu wao na kuaminiwa na jopo kubwa la wananchi.
Ameyasema hayo akiwa katika Seminar ya Kifua Kikuu (TB) iliyoandaliwa na kuratibiwa na Mpango wa
Taifa wa kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma Wizara ya Afya iliyofanyika jana katika ukumbi mdogo wa mikutano wa Bunge jijini Dodoma.
Semina hiyo iliyolenga kuwaelimisha Waheshimiwa wa Bunge walio katika kamati ya Afya na Huduma za Jamii, ili kuisaidia Serikali kupaza sauti juu ya masuala ya Kifua Kikuu (TB) na kubadilisha mitazamo ya jamii juu ya ugonjwa huo.
Alisema kuwa tafiti nyingi zinaonesha kuwa karibia theluthi moja ya Watanzania tayari
wamepata maambukizo ya Kifua Kikuu na wanaishi na vimelea mwilini mwao hivyo kuwakumbusha kuwakumbusha TB inatibika na kupona kabisa, dawa
zake zinatolewa bure na zinapatikana sehemu zote nchini katika vituo
vya Umma na Binafsi.
0 on: "DKT. NDUGULILE AWAHASA VIONGOZI KUWA MSATARI WA MBELE KUTOKOMEZA TB"