Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akifungua Mkutano Wa Balaza la
Wafanyakazi Wa Wizara ya Afya mapema leo Jijini Dar es salaam.
Mganga Mkuu Wa Serikali Prof.
Muhammad Bakari Kambi akimkaribisha mgeni rasmi Waziri Wa Afya, Maendeleo ya
jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu(hayupo kwenye picha).
Mkurugenzi Wa Mafunzo na Rasilimali
watu Dkt.Otilie Gowelle wakwanza kulia akifuatilia kwa makini maagizo ya
Waziri Wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa
Wizara ya Afya uliofanyika jijini Dar es salaam.
Meza kuu ikiongozwa na Waziri wa
Afya Mhe.Ummy Mwalimu na mganga Mkuu wa Serikali Prof. Kambi wakati wakiimba
wimbo wa kuhamasisha umoja na mshikamano kwa Wafanyakazi, pindi wakifanya
mkutano wa Baraza la Wafanyakazi, Wakwanza ni Katibu wa Baraza hilo Mary Ntira
na wa mwisho ni Afisa Elimu kazi na mratibu wa Jinsia taifa TUGHE Bw. Nsubisi
Mwasandende.
Watumishi wa Wizara ya Afya
wakiongozwa na Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Dorothy Gwajima wapili kutoka kulia.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu katikati waliokaa akiwa kwenye
picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi kutoka Wizara ya
Afya mara baada ya kikao cha Baraza hilo kilichofanyika Leo jijini Dar es
salaam.
Na WAMJW-Dar es salaam.
WATUMISHI wa sekta ya Afya nchini
wametakiwa kujiepusha na vitendo vya kutaka rushwa kutoka kwa wananchi
wanapokuwa sehemu zao za kazi ili kuendana na maadili ya utumishi wa
Umma.
Hayo yamezungumzwa na Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto katika kikao cha Baraza la
Wafanyakazi wa Wizara hiyo kilichofanyika leo jijini Dar es salaam ili
kujadili mustakabari wa utoaji huduma za Afya nchini.
"Marufuku Watumishi wa sekta ya
afya nchini kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa na kama wapo naomba waache
mara moja kwani atakayebainika anajihusisha na rushwa sheria itafuata mkondo
wake mara moja" alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa
watumishi wa sekta ya afya hasa katika sehemu ya kutolea huduma za afya
wanatakiwa kuwa na lugha nzuri kwa wananchi pindi wanapotoa huduma sehemu zao
za kazi.
Mbali na hayo Waziri Ummy amewaambia
watumishi wa sekta ya afya kuwa kipaumbele katika kutoa elimu juu ya magonjwa
yasioambukiza kwani yamekuwa yakiongezeka kila kukicha kutokana na ukosefu
elimu ya kutosha kuhusu magonjwa hayo.
"Watumishi wa Afya wanatakiwa
kuwa mfano hasa katika kufanya mazoezi, kula lishe bora pamoja na kutoa
elimu ya magonjwa mbalimbali ili kuisaidia kuondoa ongezeko la magonjwa
yasioambukiza" alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa ili
kufikia adhma ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jonh Pombe
Magufuli la kujenga uchumi wa Viwanda ni lazima kuzingatia utoaji wa huduma
bora za afya ili kuwa na wananchi wenye afya ambao watasukuma gurudumu
kufikia lengo hilo.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Katibu
Mkuu Taifa wa Balaza la Wafanya kazi TUGHE Bw. Nsubisi Mwasandende amesema kuwa
katika kutatua changamoto za magonjwa mbalimbali watendaji wa Wizara ya Afya
wanatakiwa kuzingatia hali ya upatikanaji wa chanjo ili kuboresha huduma za
afya.
Aidha Bw. Mwasandende amesema
kuwa watumishi wanatakiwa kulifanyia kazi haraka agizo la Waziri Ummy
Mwalimu la kutokomeza vitendo vya rushwa haraka iwezekanavyo ikiwa kama
moja la adhimio la katiba ya balaza la wafanyakazi.
0 on: "WATUMISHI WA AFYA WAJIEPUSHE NA VITENDO VYA RUSHWA SEHEMU ZAO ZA KAZI"