WATUMISHI wa sekta ya Afya nchini
wametakiwa kujiepusha na vitendo vya kutaka rushwa kutoka kwa wananchi
wanapokuwa sehemu zao za kazi ili kuendana na maadili ya utumishi wa
Umma.
Hayo yamezungumzwa na Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto katika kikao cha Baraza la
Wafanyakazi wa Wizara hiyo kilichofanyika leo jijini Dar es salaam ili
kujadili mustakabari wa utoaji huduma za Afya nchini.
"Marufuku Watumishi wa sekta ya
afya nchini kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa na kama wapo naomba waache
mara moja kwani atakayebainika anajihusisha na rushwa sheria itafuata mkondo
wake mara moja" alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa
watumishi wa sekta ya afya hasa katika sehemu ya kutolea huduma za afya
wanatakiwa kuwa na lugha nzuri kwa wananchi pindi wanapotoa huduma sehemu zao
za kazi.
Mbali na hayo Waziri Ummy amewaambia
watumishi wa sekta ya afya kuwa kipaumbele katika kutoa elimu juu ya magonjwa
yasioambukiza kwani yamekuwa yakiongezeka kila kukicha kutokana na ukosefu
elimu ya kutosha kuhusu magonjwa hayo.
"Watumishi wa Afya wanatakiwa
kuwa mfano hasa katika kufanya mazoezi, kula lishe bora pamoja na kutoa
elimu ya magonjwa mbalimbali ili kuisaidia kuondoa ongezeko la magonjwa
yasioambukiza" alisema Waziri Ummy.
0 on: "JIEPUSHENI NA RUSHWA, MHE. UMMY MWALIMU"