Matukio ya Mkutano wa 65 wa Mawaziri wenye dhamana ya Sekta ya Afya katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Mashariki, kati na kusini mwa Afrika (Eastern, Central and Southern Africa Health Community, ECSA-HC), yanayoendelea jijini Dar es salaam, yakiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, kikao hicho kilifunguliwa juzi machi 19 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitembelea Mabanda ya LAB EQUIP LMTD na Banda la Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi TFDA baada ya mapumziko mafupi ya Mkutano wa 65 wa Mawaziri wenye dhamana ya Sekta ya Afya katika nchi
wanachama wa Jumuiya ya Mashariki, kati na kusini mwa Afrika (Eastern,
Central and Southern Africa Health Community, ECSA-HC).
Kikao cha ndani cha Mawaziri wenye dhamana ya Sekta ya Afya katika nchi
wanachama wa Jumuiya ya Mashariki, kati na kusini mwa Afrika (Eastern,
Central and Southern Africa Health Community, ECSA-HC), huku wakikubaliana kuimarisha utawala na kuweka mikakati ya pamoja ya kudhibiti na kupambana na magonjwayanayolipuka baina ya nchi hizo, pia kudhibiti magonjwa yasiyoyakuambukiza kama vile magonjwa ya Saratani, ambayo yanasababishwa na aina ya vyakula vyenye mafuta kupita kiasi, matumizi ya vilevi na matumizi ya sigara.
Pia kuongeza uwajibikaji ili kuimarisha Sekta ya Afya hasa katika Afya ya mama na mtoto.
Viongozi wa Serikali kutoka Wizara ya Afya wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto- Idara kuu ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya (Watatu kutoka Kushoto) wakwanza ni Mkurugenzi wa Ubora wa Huduma za Afya Dkt. Mohamed Mohamed, wa pili ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhamed Bakari Kambi na wa mwisho ni Dkt. Kwasi. wakiwa katika hafla ya chakula cha usiku baada ya Mkutano wa 65 wa Mawaziri wenye dhamana ya Sekta ya Afya katika nchi
wanachama wa Jumuiya ya Mashariki, kati na kusini mwa Afrika (Eastern,
Central and Southern Africa Health Community, ECSA-HC) uliofanyika katika Hotel ya Kilimanjaro jijini Dar es salaam.
NA WAMJW-DAR ES SALAAM
Mkutano wa 65 wa Jumuiya ya Mawaziri
wa Afya wa Nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini ECSA umemalizika leo jijini
hapa kwa nchi wanachama kukubaliana maazimio mbali mbali yanayolenga
kutekeleza kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza kama vile kisukari, saratani,
magonjwa ya moyo na ya mfumo wa hewa.
Akizungumza wakati wa kufunga mkutano
huo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
amesema makubaliano hayo yamelenga kuimarisha na kuboresha sekta hiyo na afya
ya wananchi kwa ujumla.
Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa
wamekubaliana pia kuongeza uwajibikaji kwenye afya ya mama na mtoto ili
kuepusha vifo vya mama na mtoto vinavyotokana na uzazi.
“Tumekubaliana kudhibiti magonjwa
yasiyoambukiza tumegundua katika nchi hizo magonjwa yanayoongoza ni pamoja na
kisukari, saratani, magonjwa ya moyo na ya mfumo wa hewa" alisema Waziri
Ummy.
Kwa mujibu wa Waziri Ummy amesema
kuwa Suala lingine walilokubaliana ni kutilia mkazo suala la heshima kwa
wajawazito kwa sababu mawaziri wameshauri pia Tanzania kukitambua Chuo cha
Upasuaji cha Afrika Mashariki, Kati na Kusini.
Waziri Ummy ambaye pia ni Mwenyekiti
wa Jumuiya hiyo, amesema wamkubaliana wamekubaliana pia kuimarisha ushirikiano
na ulinzi katika maeneo ya mipaka.
“Kwa sababu nchi zina mipaka lakini
magonjwa hayana mipaka tukiimarisha itasaidia kuondoa na kudhibiti uwezekano wa
magonjwa hasa ya mlipuko kuenea ikiwemo Zika, Ebola, Dengue, Chikungunya na
mengineyo,” alisema Waziri Ummy.
Pamoja na mambo mengine, Waziri
Ummy amesema pia wamekubaliana kuimarisha masuala ya utawala kwamba kila
mmoja ana wajibu kwa nafasi yake kwani sekta ya afya ni mtambuka.
“Tumeona kuna umuhimu mkubwa wa
kushirikisha sekta zingine ikiwamo kilimo, maji, elimu, utumishi, mazingira
zinahusika kwa ukaribu na masuala ya Afya” alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa azimio
la saba walilokubaliana katika mkutano huo ni kuweka mkakati wa pamoja
kukabiliana na magonjwa akitolea mfano nchi ya Uganda ambao wamepata ugonjwa wa
Marbugy unaofanana dalili na ugonjwa wa Ebola.
Mkutano huo wa kujadili masuala
mbalimbali ya afya yalijumuisha nchi 9 kutoka
Nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini ECSA umefanyika nchini Tanzania
kwa siku tatu.
0 on: "MAWAZIRI WA AFYA WA JUMUIYA YA ECSA WAKUBALIANA KUIMARISHA SEKTA YA AFYA"