Rais wa Jamhuri ya muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongozana na Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto kwake) mapema leo
jijini Dar es salaam wakati akizindua magari mapya 181 ya Bohari ya Dawa (MSD)
yatayotumika kusambaza Dawa na Vifaa tiba.
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelekezo kutoka kwa Bw. Byekwaso Tabula wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kuhusu hali ya upatikanaji wa Dawa katika Bohari hiyo, wa pili kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalim.
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelekezo kutoka kwa Bw. Byekwaso Tabula wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kuhusu hali ya upatikanaji wa Dawa katika Bohari hiyo, wa pili kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalim.
Rais wa Jamhuri ya muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo mbele ya Viongozi wa
Serikali na wafanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD) wakati akizindua magari mapya
181 ya Bohari ya Dawa (MSD) yatayotumika kusambaza Dawa na Vifaa tiba.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya
Dawa (MSD) Mhe. Laurean Bwanakunu akisoma taarifa ya utendaji ya Bohari ya Dawa
(MSD) mbele ya mgeni rasmi Mhe. Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli na viongozi wa Serikali.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimkaribisha mgeni rasmi Mhe.
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati
akizindua magari mapya 181 ya Bohari ya Dawa (MSD) yatayotumika kusambaza Dawa
na Vifaa tiba.
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakari
Kambi na Mkurugenzi wa ubora wa huduma Dkt Mohamed Ally Mohamed wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Mhe. Rais wa Jamhuri ya muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akizindua magari mapya 181 ya Bohari
ya Dawa (MSD) yatayotumika kusambaza Dawa na Vifaa tiba.
Rais wa Jamhuri ya muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza meza kuu kuimba wimbo wa taifa
wakati akizindua magari mapya 181 ya Bohari ya Dawa (MSD).
Rais wa Jamhuri ya muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuonesha uzinduzi rasmi wa magari mapya 181 ya Bohari ya Dawa
(MSD) yatayotumika kusambaza Dawa na Vifaa tiba.
Picha ya Pamoja ikiongozwa na
Mhe. Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya
kuzindua magari mapya 181 ya Bohari ya Dawa (MSD) yatayotumika kusambaza Dawa
na Vifaa tiba.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimsikiliza kwa makini Bibi
aliyejumuika katika uzinduzi wa magari mapya 181 ya Bohari ya Dawa (MSD)
yatayotumika kusambaza Dawa na Vifaa tiba.
Na
WAMJW-DAR ES SALAAM.
ILI kufikia katika uchumi wa kati kwa
kutumia sekta ya viwanda Serikali inatakiwa kujikita katika kuimarisha sekta ya
afya kwa watanzania ili kuwa na rasilimali watu wenye afya njema kwa ajili ya
kuleta mafanikio hayo kupitia viwanda.
Hayo yamesemwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa uzinduzi wa magari 181
ya kusambazia dawa uliofanyika leo katika Bohari Kuu ya Dawa ya Taifa (MSD)
jijini Dar es salaam.
“Tunatakiwa kuwekeza kwenye uchumi wa
Viwanda ili tufikie uchumi wa kati hivyo ni lazima tuwekeze kwenye sekta ya
afya kwa kiwango kikubwa ili kuwa na wananchi wenye afya njema tayari kutumikia
viwanda vyetu kwa muda wote” alisema Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli amesema kuwa Tanzania
inatakiwa kujijengea viwanda vya dawa na vifaa tiba hapa nchini ili fedha
zinazotumika kununua bidhaa hizo nje ya nchi zirudi mikononi kwa watanzania
wenyewe pamoja na kutoa ajira kupitia viwanda hivyo.
Mbali na hayo Rais Magufuli amesema kuwa
katika kuimarisha Sekta ya afya Serikali imetenga shilingi Bilioni 269 za
kununua dawa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 kutoka bilioni 31 katika
bajeti ya fedha mwaka 2016/2017.
Kwa upande wake Waziri wa afya,Maendeleo
ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa katika kuimarisha
Afya ya mama na Mtoto Serikali imepunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa
asilimia 60 kutoka asilimia 20 ya upunguzaji wa vifo hivyo.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa fedha
zilizotengwa kwa ajili ya dawa zina mgawanyo ikiwemo asilimia 42 zahanati na
vituo vya afya ,asilimia 16 zinatumika kwa chanjo za watoto ,asilimia 10.2
zianenda hospitali za wilaya ,asilimia 6.8
zinatumia hospitali za mikoa ,asilimia 3.4 zinaenda hospitali maalum na
asilimia 3 zinatumika kwa ajili ya dawa za saratani.
“Fedha hizo za dawa zipatazo Shilingi
Bilioni 269 asilimia kubwa zinaenda kwenye vijiji na kata pamoja na zahanati na
vituo vya afya na kufanya hali ya upatikanaji wa dawa kuwa juu mpaka kufikia
hivi sasa” alisema Waziri Ummy.
Waziri Ummy amesema kuwa licha ya kuwa
tu kuna upatikanaji dawa wa hali ya juu nchini lakini Serikali kupitia Wizara
ya Afya imetengeneza muongozo wa matibabu kwa ajili na kuwataka waganga wafawidhi wote nchini
kutumia muongozo huo ili kutoa matibabu sahihi kwa wagonjwa .
Kwa mujibu wa Waziri ummy amesema kuwa
katika kuimarisha sekta ya Afya nchini Serikali imejitahidi kuongeza huduma za
matibabu ya kibingwa kwani hivi sasa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
inapandikiza figo pamoja na vifaa vya usikivu kwa watoto ambapo imepelekea
kupunguza rufaa za nje na kuokoa fedha nyingi.
Naye Mkurugenzi wa Bohari Kuu ya Dawa ya
Taifa nchini (MSD) Bw. Laurean Bwanakunu amesema kuwa wanasambaza dawa za
shilingi bilioni 18 kila mwezi na lengo ni kufikia bilioni 21 kufika mwezi
julai mwaka huu.
Aidha Bw. Bwanakunu amesema kuwa mbali
na upatikanaji wa dawa kuongezeka lakini kuna chanagamoto za maoteo kutoka
ngazi ya zahanati kwani wanashindwa kujua mahitaji yao sahihi ya dawa
zinazohitajika kwa mwaka hivyo kufanya MSD kushindwa kupeleka dawa kwa wakati.
Samabamba na uzinduzi huo wa magari hayo 181 ya kusambazia dawa na vifaa tiba
hapa nchini yaliyotolewa kwa ushirikiano wa Seikali ya Tanzania pamoja na Mfuko
wa Dunia wa pamoja (Global Fund) pia Mhe. Rais Magufuli alipata kutembelea
maghala ya dawa yaliyopo MSD jijini Dar
es salaam.
0 on: "ILI KUWEPO NA UCHUMI WA VIWANDA IMARA NI LAZIMA KUWA NA SEKTA YA AFYA ILIYO BORA."