Naibu Waziri Dkt. Godwin Mollel akiongea wakati wa mahafali ya wahitimu
wa famasia wanaoingia kwenye taaluma,mahafali hayo yamefanyika kwenye
Jijini Dodoma.
Msajili wa Baraza la Famasi Elizabeth Shekalaghe akiongea wakatibwa
mahafali hayo ambapo wahitimu 252 walikula kiapo na kuingia rasmi kwenye
taaluma ya famasia.
Mwakilishi wa wahitimu hao Mkapa.Madebele akitoa neno wakati wa mahafali hayo.
Dkt. Mollel akibadilishana mawazo na Msajili wa Baraza la Famasi kwenye
mahafali ya kiapo cha wafamasia wanaoingia kwenye taaluma.
Wahitimu hao wakisaini viapo mara baada ya kuapa.
Wafamasia hao wakila kiapo cha famasia,moja ya wajibu wao ni kuhakikisha
sehemu wanayofanya kazi au kuisimamia ni halali na ina vibali.
Naibu Waziri Dkt. Mollel akimpatia cheti mmoja wa wahitimu wa taaluma ya famasia kwenye mahafali hiyo
DKT. MOLLEL AWAFUNDA WAFAMASIA WANAOINGIA KATIKA TAALUMA.
Na. Catherine Sungura, WAMJW-Dodoma
Wafamasia wote nchini wametakiwa kutoishia kutoa dawa kwa wagonjwa bali kusimamia ili kujua kama dawa zimefika kwa mgonjwa.
Hayo
yamesemwa leo na Naibu Waziri Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Dkt. Godwin Mollel wakati wa mahafali ya kiapo cha wafamasia
wanaoingia katika taaluma iliyofanyika jijini hapa.
Akiongea
wakati wa sherehe hizo Dkt. Mollel amesema kuwa wafamasia hao wanalo
jukumu kubwa la kuokoa maisha ya wananchi hivyo kutokuhakikisha dawa
walizotoa zinamfikia mgonjwa ni kupoteza maisha kwa wagonjwa wanaofika
kupata huduma kwenye vituo vyao.
“Wizara
inawategemea sana na kutambua kazi kubwa inayofanywa na wafamasia licha
ya wachache waliopo kuiangusha taaluma hiyo,hii ni kuvunja kiapo
mlichoapa leo na kituo kinapokosa dawa wapo wananchi wanaopoteza maisha
na unapokuta upotevu wa dawa lazima mfamasia ahusike”.
Alisema Dkt. Mollel.
Hata
hivyo Naibu Waziri huyo amewata wafamasia hao walioingia rasmi leo
kwenye taaluma wasisubiri kuingiza dawa au kumpatia mgonjwa dawa bali
wametakiwa kuwa wabunifu kwa kutengeneza dawa kwenye maeneo yao kazi ili
kuweza kuipunguzia gharama Serikali.
“Mtakapoenda
kwenye ajira nataka mjue eneo la dawa ni muhimu sana kwenye uhai wa
hospitali hivyo mkiisimamia vyema serikali itakaa vizuri, muhakikishe
mnasimamia vizuri eneo hilo hususani kwenye maamuzi katika vituo vya
kutolea huduma za afya nchini”.
Kwa upande wa
matumizi ya fedha Dkt. Mollel amewataka wafamasia kuwajibika ipasavyo
kwani kumekuwepo na matumizi mabaya ya fedha za dawa kwenye vituo vya
umma na hivyo kusababisha kukosekana kwa dawa na vitendanishi na hivyo
kusababisha wananchi kutojiunga na bima za afya ikiwemo CHF na wengine
wenye uwezo kukimbilia kwenda kwenye hospitali binafsi.
Naye
Msajili wa Baraza la Famasi Bi. Elizabeth Shekalaghe amesema Serikali
imewekeza fedha nyingi kwenye dawa hivyo wanapaswa kusimamia kikamilifu
huduma zote za famasi kwa kuzingatia sheria,kanuni, taratibu ,vigezo
vilivyopo ,maadili na miiko ya utendaji kazi za kila siku.
“Tumesisitiza
sana suala ya uwajibikaji,tunafahamu taalama ya famasi imeanza toka
mwaka 1978, lakini ukuaji wake umekua kwa taratibu sana ila hivi sasa
imekua ikiongezeka kila mwaka na wastani kila mwaka wanahitimu wanafunzi
wasiopungua 250 na hivyo tumeweza kusajili wafamasia 2329 hadi
sasa”.Alisema.
Shekalaghe amesema Serikali
imewekeza fedha nyingi kwenye sekta ya afya ikijumuisha huduma
zitolewazo ikiwemo huduma za dawa“Mhe Rais ametuona hivyo hatupaswi
kumuangusha tuhakikishe tunasimamia kikamilifu rasiliamali hizi ambazo
serikali imewekeza katika utoaji wa huduma za dawa”. Alisisitiza
Shekalaghe.
Hata hivyo amesema, katika mahafali
hayo wameweza kujadili namna gani wanaweza kutumia mifumo iliyopo ili
kuweza kufanya huduma zinazotolewa katika mnyororo wa dawa, kusimamiwa
na kuhakikisha dawa zinawafikia wagonjwa kwa kuweka kumbukumbu vizuri.
Wakati
huo huo mwakilishi wa wahitimu hao Mkapa Madebele amewaasa wahitimu
wenzie kufuata na kuzingatia sheria za taaluma yao kwani wanahusika kila
siku kwenye famasi na kutaka kulinda weledi kwani afya za wananchi zipo
juu yao.
Madebele amesema wapo tayari kutumika
na kuajiriwa sehemu yoyote nchini ili kuwasaidia wananchi ambao ndio
wazazi na walezi wao kwenye jamii kama wanataaluma wa dawa.
Baraza
la Famasi moja la jukumu lao ni kuwasajili wanataaluma hao waliokidhi
vigezo, jumla ya wahitimu 252 wamehitmu katika mahafali ya tisa
yanayofanyika kila mwaka kwa awamu mbili.
-Mwisho-
0 on: "DKT. MOLLEL AWAFUNDA WAFAMASIA WANAOINGIA KATIKA TAALUMA."