Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi akieleza jambo mara baada ya kufanya
kikao na Viongozi wakuu wa sekta ya afya kwa njia ya mtandao"ZOOM"
kilichowajumuisha Waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya,Wajumbe wa kamati ya
usimamizi wa huduma za afya za mikoa(RHMT) na wilaya (CHMT) pamoja na
Wakurugenzi wa hospitali za Taifa,Kanda na Maalumu.
VIONGOZI SEKTA YA AFYA TATUENI KERO ZA WANANCHI:PROF. MAKUBI
Na. Catherine Sungura,WAMJW-Dodoma
Wizara
ya Afya ipo tayari kupokea kero na malalamiko ya wananchi endapo
itaonekana wameshindwa kusikilizwa ama kusaidiwa na viongozi wao wa
ngazi za chini na wale wa vituo vya kutolea huduma za afya kwenye maeneo
yao.
Hayo yameelezwa leo
na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi mara baada ya kufanya
kikao na Viongozi wakuu wa sekta ya afya kwa njia ya mtandao"ZOOM"
kilichowajumuisha Waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya,Wajumbe wa kamati ya
usimamizi wa huduma za afya za mikoa(RHMT) na wilaya (CHMT) pamoja na
Wakurugenzi wa hospitali za Taifa,Kanda na Maalumu.
Prof.
Makubi amesema kuwa wananchi wana matumaini na Serikali yao hivyo
wanayo haki ya kusikilizwa na kutatuliwa kero zao kutoka kwa watendaji
kwenye vituo vyote vya huduma za afya nchini hivyo kamati zote
zinapaswa kufanya tathimini za kero zote kwa muda wa wiki nne na
kuzitatua pia kuwasilisha ripoti Wizarani pamoja na TAMISEMI .
“Tunaanzisha
utaratibu ambao sisi viongozi wa sekta ya afya tunaenda kutafuta kero
kutoka kwa wananchi na kuzitatua,Hili ni agizo na tumekubaliana wasambae
kwenye ngazi zote kuanzia zahanati,vituo vya afya na kwenye
hospitali,tunatakiwa kuhakikisha wananchi wapate huduma bora licha ya
kuwa tumeboresha huduma kwenye vituo vyetu”.
Aidha,
amesema utaratibu huu utaweza kurahisisha kutatua kero za wananchi na
kuweza kupunguza kero hizo na zingine sio lazima zimfikie Mhe. Waziri
hivyo kama watendaji wanatakiwa kujitafakari wanaweza kutatua vipi
changamoto wazipatazo wananchi.
“tumekubalikia
suala la kuimarisha suala la uongozi, uwajibikaji na usimamizi kwani
kila mmoja ameona kuna mapungufu kwenye usimamizi wa huduma za afya
nchini,hivyo tumekubaliana kila kiongozi kuanzia Taifa hadi vijijini
kusimamia sehemu zenye mapungufu kwani wananchi wanahitaji mazuri kutoka
kwetu,hatuwezi kuwaridhisha kwa kila kitu lakini tutapunguza matatizo
yao.
Upande wa kuimarisha
vitengo vya huduma kwa wateja, Mganga Mkuu huyo wa Serikali amesema
kitengo hicho kinatakiwa kuboreshwa na hivyo wanapaswa kuchakata kero
zote na kuzifanyia kazi na hivyo kuzibandika kwenye ubao wa matangazo wa
vituo vyao pia wanapaswa kuwa hai wakati wote kwakuwa mwananchi
wanataka huduma za afya jinsi wanavyohitaji.
“Viongozi
hao pia wanatakiwa kukagua ndani ya hospitali zao kwenye maeneo ya
kutolea dawa na stoo kuona kama dawa zipo na zinawatosheleza
wananchi,kama kuna wizi tuweze kuchukua hatu,waende kwenye wodi na OPD
kuwasalimu wagonjwa na kama wana kero waseme ili wazitatue,pia maabara
kuweza kuona kama vipimo vinafanyika”.Alisisitiza.
Hata
hivyo wamekubaliana kuwepo na magroup ya ‘Whatsap’ ambayo watapokea na
kushughulikia kero kwenye kila wilaya au mkoa husika ili kila mwananchi
awezo kutoa kero zake.
“Tumeagiza
kuwe na namba ambazo zitatangazwa kwa wananchi,pia wawashirikie
wananchi kupitia mikutano na kutaja namba zao ili wananchi wajue
wanawasilisha vipi malalamiko yao ”.
Aliongeza
kuwa wananchi wanapaswa kujenga imani na kuwaamini watendaji wote wa
sekta ya afya, na kusema kuwa baada ya Mhe. Waziri kutangaza namba yake
ya malalamiko kwa muda wa wiki mbili ameweza kupokea kero elfu tatu
kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Kikao
hicho kwa njia ya mtandao kimehudhuriwa na washiriki wapatao 220 na
ajenda kubwa ilikuwa ni jinsi ya kupunguza kero za wananchi zinazousiana
na huduma za afya nchini ambazo wanatuma kupitia namba ya malalamiko
iliyotangazwa na Waziri wa afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Doroth Gwajima mwishoni mwa mwaka jana ambayo ni 0734124191.
-MWISHO-
You described el concept de manera tan clara y detallada. Gracias por compartir con nosotros este magnífico artículo. I'm convinced que a lot of readers will appreciate it enormemente. Agradezco que haya dedicado tiempo a redactar tanto un post tan relevante. Reading esto me ha enseñado mucho. Continuar con tu magnífica labor! I'm eager to read your posts to come.
JibuFutaResearch sweeping information on Maryland Rape Lawyer, including definitions, disciplines, and genuine resources for setbacks and their families.
JibuFuta