Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Ajira. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Ajira. Onyesha machapisho yote

Jumatano, 25 Machi 2020

TAASISI YA BENJAMIN MKAPA YAMWAGA AJIRA 307 ZA WATUMISHI WA AFYA

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akieleza jambo wakati wa kikao na Waandishi wa habari, kilichofanyika Jinjini Dodoma.

 Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula akifafanua jambo wakati wa kikao na Waandishi wa habari, kilichofanyika Jinjini Dodoma.

Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Benjamin Mkapa Dkt. Ellen Mkondya akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari, katika Mkutano ulioongozwa na Waziri wa Afya leo Jijini Dodoma.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akieleza jambo wakati wa kikao na Waandishi wa habari, kilichofanyika Jinjini Dodoma. katikati ni naibu waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula (wakwanza kushoto).

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na Waandishi wa habari.


TAASISI  YA BENJAMIN MKAPA YAMWAGA AJIRA 307 ZA WATUMISHI WA AFYA.

Na Rayson, Mwaisemba, WAMJW-DOM

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Taasisi ya Benjamini Mkapa inayotekeleza mradi wa Uimarishaji mifumo endelevu na stahimivu ya Afya kwa ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na UKIMWI, Malaria na Kifua Kikuu, imeajiri jumla ya watumishi 307 ikiwa ni muendelezo wa kuimarisha huduma za Afya nchini.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa kikao na Waandishi wa habari, kilichofanyika Jinjini Dodoma.

“Tunapenda kuwataarifu mwendelezo wa kazi nzuri inayotekelezwa kupitia mradi huu na kwamba taratibu za ajira kwa wataalam wa afya wengine 307 zimekamilika. Lengo kuu la zoezi hili ni kuongeza nguvu katika utoaji huduma katika sekta ya afya”, alisema Waziri Ummy.

Katika kikao hicho kilichohudhuliwa na Naibu Waziri wa Afya na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula, Waziri Ummy amesema kuwa, Serikali kwa kushirikiana na Taasisi ya Mkapa, kuanzia mwaka 2018 hadi February 2020, imeweza kuajiri jumla ya watumishi wa afya 461 ambao wanatoa huduma za afya sehemu mbalimbali nchini.

Aliendelea kusema kuwa, Watumishi hawa watahudumu kwenye hospitali, vituo vya afya na zahanati zilizopo katika mikoa 12 ya Kagera, Mwanza, Geita, Simiyu, Mara, Shinyanga, Kigoma, Tabora, Katavi, Dodoma, Songwe na Kilimanjaro.

Aidha, Waziri Ummy alisema kuwa, wataalamu hao 307 wameshapangiwa kufanya kazi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa 68 zilizopo katika Mikoa 11, huku akibainisha kuwa Mikoa iliyonufaika ni Mwanza (34), Shinyanga (33), Mara (43), Simiyu (51), Geita (30), Kagera (34), Katavi (41), Tabora (43), Dodoma (27), Arusha (10) na Kigoma (42).

Alisema kuwa, Kupitia mchakato huu wa ajira, Kada sita za wataalamu wa Afya zimenufaika na kibali hiki kwa mgawanyo ufuatao; Kada ya Wauguzi wenye cheti (59), Wauguzi wenye Diploma (30), Maafisa Tabibu (73), Maafisa Tabibu Wasaidizi (100), Wataalamu wa maabara ngazi ya cheti (25) na ngazi ya Diploma (20).

Mbali na hayo, Waziri Ummy ameendelea kuwahimiza wataalamu wote waliopangiwa maeneo ya kufanyia kazi kuripoti mara moja kuanzia tarehe 23 hadi 27 Machi 2020, na kuanza kutekeleza majukumu yao katika vituo watakavyopangiwa.

“Napenda kuwahimiza wataalamu wote waliopangiwa maeneo ya kufanyia kazi kuripoti mara moja kuanzia tarehe 23 hadi 27 Machi 2020, ili kuanza kutekeleza majukumu yao katika vituo watakavyopangiwa” alisema

Nae, Katibu Mkuu Wizara ya  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula amesema kuwa, Serikali imeendelea kuimarisha mfumo wa upataji taarifa (mawasiliano), huku akiwataka waombaji kufanya maombi ndani ya muda ulioelekezwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Benjamin Mkapa Dkt. Ellen Mkondya amesema kuwa, taasisi ya Benjamin Mkapa kwa miaka 14 imetoa ajira za wataalam wa afya 2181 ambao wamekuwa wakitoa huduma katika Hospitali na Vituo vya tiba nchini kote, hususan vituo vya serikali na baadhi kwenye vituo vya kidini.

“Taasisi ya BMF kwa miaka 14 yote tokea mwaka 2006 hadi Desemba 2019, tumeshaweza kutoa ajira za wataalam wa afya 2181 ambao wamekuwa wakitoa huduma katika Hospitali na Vituo vya tiba nchini kote, hususan vituo vya serikali na baadhi kwenye vituo vya kidini” alisema.

Mwisho.

Jumatano, 31 Januari 2018

TANGAZO LA KUITWA KAZINI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya.



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,
WAZEE NA WATOTO
 
 
 
 
TANGAZO LA KUITWA KAZINI
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto -Idara Kuu Afya anawajulisha wafuatao kuripoti kazini Makao Makuu ya Wizara Mjini Dodoma ndani ya siku 14 wakiwa na vyeti halisi vya  elimu ya Sekondari, Taaluma,usajili wa Baraza/Bodi ya kitaaluma,cheti cha kuzaliwa pamoja na nakala mbili za picha ndogo (passport)
Imetolewa na :

Katibu Mkuu-Afya
31/1/2018




ORODHA YA MAJINA YA WOAMBAJI WANAOTAKIWA KURIPOTI WIZARA YA AFYA MEANDELEO YA JAMII JINSIA WAZEE NA WATOTO KUKAMILISHA TARATIBU ZA AJIRA  






NA JINA CHEO KITUO CHA KAZI







1 LILIAN DIDAS LYAKURWA KATIBU WA AFYA II KATIBU MKUU AFYA







2 NKWIMBA NYALALI AFISA MUUGUZI MSAIDIZI II KATIBU MKUU AFYA







3 MARY MATHIAS OTTARU AFISA AFYA MAZINGIRA II KATIBU MKUU AFYA







4 JACOB R. TARIMO MUUGUZI  KATIBU MKUU AFYA







5 SOPHIA ISSA LUCAS MHUDUMU WA AFYA KATIBU MKUU AFYA







6 HAPPY ALEX YOHANES MHUDUMU WA AFYA KATIBU MKUU AFYA







7 MARTHA ADRIANO MHUDUMU WA AFYA KATIBU MKUU AFYA







8 JENIPHER JOSEPH GHULIKU MTEKNOLOJIA MSAIDIZI MAABARA KATIBU MKUU AFYA







9 SURAIYA A. DULE MHUDUMU WA AFYA KATIBU MKUU AFYA







10 NEEMA MWASENGA MHUDUMU WA AFYA KATIBU MKUU AFYA







11 SCHOLASTICA OFAMAN MHUDUMU WA AFYA KATIBU MKUU AFYA







12 BLANDINA VICTOR SHUMA AFISA MUUGUZI MSAIDIZI II KATIBU MKUU AFYA

Ijumaa, 24 Novemba 2017

UPASUAJI WA KIHISTORIA WA UPANDIKIZAJI WA FIGO WAFANYIKA.

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya jopo la madaktari bingwa wa Upasuaji wa upandikizaji wa figo kutoka Tanzania na India pamoja na Waandishi wa habari (hawapo kwenye picha), katika uzinduzi rasmi wa huduma za upasuaji wa upandikizaji wa figo uliofanyika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

 
 Madaktari  Bingwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili  walioshiriki katika Upasuaji wa upandikizaji wa figo kwa kushirikiana na Jopo la madaktari bingwa kutoka Hospitali ya BLK ya New Delhi, India.

 Prof. Lawrence Museru akimueleza jambo Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma za upasuaji wa upandikizaji wa figo uliofanyika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili .

 Mkuu wa Kitengo cha Upandikizaji wa Figo kutoka India Dkt. H.S Bhatyal akimtambulisha Mkurugenzi Mkuu wa Nephroway Dkt. Sunil Prakash  mbele ya  Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu.

Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika uzinduzi rasmi wa huduma za upasuaji wa upandikizaji wa figo uliofanyika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.




Na WAMJWW, DSM
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ikishirikiana na wataalam kutoka Hospitali ya BLK ya New Delhi, India, wamefanikiwa kufanya upasuaji wa kihistoria wa upandikizaji wa figo (Renal Transplant).
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi rasmi wa upandikizaji wa figo uliofanyika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.
“Kupitia hadhara hii nipende kutumia fursa hii kuwafahamisha rasmi Watanzania kwamba sasaivi Hospitali yetu ya Taifa ya Muhimbili kwa kushirikiana na Hospitali ya BLK ya New Delhi, nchini India wamefanikiwa kufanya upasuaji wa upandikizaji wa figo” alisema Mh. Ummy
Pia Waziri Ummy amesema kuwa kuanzishwa kwa huduma hizi zakibingwa za kupandikiza figo hapa nchini ambazo awali zilikua hazipatikani kutaleta nafuu katika gharama ambazo zingetumika, hii inatokana na ongezeko kubwa la wagonjwa wa figo huku wengi wao wakihitaji huduma ya utakasishaji damu (Renal Dialysis).
Kwa upande mwingine Mh. Ummy ameongeza kuwa Serikali imeanzisha vituo vya utakasishaji damu katika hospitali za Mbeya Rufaa, Chuo Kikuu cha Dodoma, KCMC na Bugando kwaajili ya  wagonjwa wanaohitaji huduma za dialysis. Vile vile, huduma hii inapatikana katika hospitali za binafsi hapa Dar es Salaam zikiwemo za Kairuki, TMJ, Regency, Aga Khan, Access na Hindu Mandal.
Mh. Ummy  Mwalimu amewahasa Watanzania kuendelea kuiamini Hospitali ya taifa ya Muhimbili kutokana na huduma bora zinazotolewa na amewahakikishia serikali itaendelea kuboresha huduma zaidi katika vituo vyote vya Afya nchini.
Aidha Mh. Ummy Mwalimu (MB) ameendelea kuwakumbusha na kuwahasa Watanzia kujiunga na mifuko ya Bima ya Afya ili kupunguza gharama kubwa inayoweza kuwakumba pindi watakapopata magonjwa.
Pia Mh. Ummy (MB) hakusita kumpongeza Raisi wa awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli kwa kwa kuwa karibu sana na sekta ya Afya kwa  kuboresha huduma za matibabu yakibingwa,
“Wakati Mh. Raisi anaingia madarakani Muhimbili walikuwa wana vitanda vya ICU 21 tu, leo Muhimbili wanavitanda 74, wagonjwa 74 wanaweza kuhudumiwa mara moja kwa wakati mmoja ambao wanahitaji huduma za dharura” alisema Mh. Ummy Mwalimu.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Prof. Lawrence Museru amewashukuru Madaktari bingwa wa upandikizaji wa figo kutoka Hospitali ya BLK ya New Delhi India kwa kukubali kutoa mafunzo kwa madaktari wa Tanzania bila gharama yoyote.