Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya jopo la
madaktari bingwa wa Upasuaji wa upandikizaji wa figo kutoka Tanzania na India
pamoja na Waandishi wa habari (hawapo kwenye picha), katika uzinduzi rasmi wa huduma
za upasuaji wa upandikizaji wa figo uliofanyika katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili.
Madaktari Bingwa
kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
walioshiriki katika Upasuaji wa upandikizaji wa figo kwa kushirikiana na
Jopo la madaktari bingwa kutoka Hospitali ya BLK ya New Delhi, India.
Prof. Lawrence Museru akimueleza
jambo Waziri
wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa
uzinduzi rasmi wa huduma za upasuaji wa upandikizaji wa figo uliofanyika katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili .
Mkuu wa Kitengo cha Upandikizaji wa Figo
kutoka India Dkt. H.S Bhatyal akimtambulisha Mkurugenzi Mkuu wa Nephroway Dkt.
Sunil Prakash mbele ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Ummy Mwalimu.
Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa
Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika uzinduzi
rasmi wa huduma za upasuaji wa upandikizaji wa figo uliofanyika katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Na WAMJWW, DSM
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
ikishirikiana na wataalam kutoka Hospitali ya BLK ya New Delhi, India,
wamefanikiwa kufanya upasuaji wa kihistoria wa upandikizaji wa figo (Renal
Transplant).
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi
rasmi wa upandikizaji wa figo uliofanyika katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili jijini Dar es salaam.
“Kupitia hadhara hii nipende kutumia
fursa hii kuwafahamisha rasmi Watanzania kwamba sasaivi Hospitali yetu ya Taifa
ya Muhimbili kwa kushirikiana na Hospitali ya BLK ya New Delhi, nchini India
wamefanikiwa kufanya upasuaji wa upandikizaji wa figo” alisema Mh. Ummy
Pia Waziri Ummy amesema kuwa kuanzishwa
kwa huduma hizi zakibingwa za kupandikiza figo hapa nchini ambazo awali zilikua hazipatikani kutaleta nafuu katika gharama ambazo zingetumika, hii inatokana na ongezeko kubwa la
wagonjwa wa figo huku wengi wao wakihitaji huduma ya utakasishaji damu (Renal
Dialysis).
Kwa upande mwingine Mh. Ummy ameongeza
kuwa Serikali imeanzisha vituo vya utakasishaji damu katika hospitali za Mbeya
Rufaa, Chuo Kikuu cha Dodoma, KCMC na Bugando kwaajili ya wagonjwa wanaohitaji huduma za dialysis. Vile
vile, huduma hii inapatikana katika hospitali za binafsi hapa Dar es Salaam
zikiwemo za Kairuki, TMJ, Regency, Aga Khan, Access na Hindu Mandal.
Mh. Ummy Mwalimu amewahasa Watanzania kuendelea
kuiamini Hospitali ya taifa ya Muhimbili kutokana na huduma bora zinazotolewa
na amewahakikishia serikali itaendelea kuboresha huduma zaidi katika vituo
vyote vya Afya nchini.
Aidha Mh. Ummy Mwalimu (MB) ameendelea kuwakumbusha
na kuwahasa Watanzia kujiunga na mifuko ya Bima ya Afya ili kupunguza gharama
kubwa inayoweza kuwakumba pindi watakapopata magonjwa.
Pia Mh. Ummy (MB) hakusita kumpongeza
Raisi wa awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli kwa kwa kuwa karibu sana na
sekta ya Afya kwa kuboresha huduma za
matibabu yakibingwa,
“Wakati Mh. Raisi anaingia madarakani
Muhimbili walikuwa wana vitanda vya ICU 21 tu, leo Muhimbili wanavitanda 74,
wagonjwa 74 wanaweza kuhudumiwa mara moja kwa wakati mmoja ambao wanahitaji
huduma za dharura” alisema Mh. Ummy Mwalimu.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili Prof. Lawrence Museru amewashukuru Madaktari bingwa wa upandikizaji
wa figo kutoka Hospitali ya BLK ya New Delhi India kwa kukubali kutoa mafunzo
kwa madaktari wa Tanzania bila gharama yoyote.
0 on: "UPASUAJI WA KIHISTORIA WA UPANDIKIZAJI WA FIGO WAFANYIKA."