Naibu Waziri wa Afya Dkt.Faustine Ndugulile akikata utepe kuashiria uzinduzi wa
upasuaji wa mabusha na ngirikokoto kwa wagonjwa wapatao 200 wa Manispaa
ya Lindi. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Statoil Bw.Oyotein Michelsen na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Kinga toka Wizara ya Afya
Dkt.Neema Rusibamayila.
Naibu Waziri wa Afya Dkt.Faustine Ndugulile akimjulia hali mmoja ya wagojwa wakati wa ziara yake katika hospitali ya rufaa ya
Mkoa Sokoine mkoani Lindi. pembeni yake ni Mkurugenzi wa Statoil Bw.Oyotein Michelsen.
Mkurugenzi wa Statoil Bw.Oyotein Michelsen akisoma hotuba kwenye
ufunguzi wa kambi ya upasuaji inayofanyila kwenye hospitali ya rufaa ya
Mkoa Sokoine mkoani Lindi
Baadhi ya wananchi wanaotarajia kufanyiwa upasuaji wa magonjwa hayo.
Naibu Waziri wa Afya akimkabidhi Mkurugenzi wa Kinga toka Wizara ya Afya
Dkt.Neema Rusibamayila ambapo Mpango wa Taifa wa kutokomeza Magonjwa
yaliyokuwa hayapewi Kipaumbele ndiye mratibu wa upasuaji huo.
Dkt.Faustine Ndugulile akipokea mashine ambayo ina kisu cha moto ambacho
kinazuia damu wakati wa upasuaji kutoka kwa Mkurugenzi wa Statoil.
Dkt.Faustine Ndugulile akihutubia wananchi waliofika kwenye uzinduzi wa
upasuaji wa mabusha na ngirikokoto kwa wagonjwa wapatao 200 wa Manispaa
ya Lindi.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto akipokea
hundi yenye thamani ya shilingi milioni 264 toka kwa Mkurugenzi wa
Kampuni ya utafiti na uchimbaji wa mafuta ya Statoil bw.Oyotein
Michelsen .Fedha hizo ni kwa ajili ya kambi za upasuaji wa mabusha na
ngirikokoto kwa watu wapatao 400 kwa mwaka 2017 na 2018.
Na WAMJW-LINDI
WAKAZI
wa Lindi na vitongoji vyake wametakiwa kushiriki katika kampeni ya
kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa kumeza kingatiba
za kutokomeza magonjwa hayo pamoja na kutunza mazingira kwa kuondoa
mazalia ya mbu wanaenezao magonjwa hayo.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa uzinduzi wa kambi ya upasuaji
wa Mabusha na Ngirikokoto(Henia) unaofanyika mkoani Lindi.
"Wakazi
wa Lindi na Vitongoji vyake tunatakiwa kushiriki katika zoezi la kumeza
dawa za kukinga magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele pamoja na
kufanya usafi wa mazingira ili kuondoa mazalia ya mbu"alisema Dkt.
Ndugulile
Aidha, Dkt.
Ndugulile amewataka wananchi wa Lindi kuondoa dhana potofu ya kuwa kila
mwenye mabusha au ngirimaji basi atakuwa amerogwa ila ajue ugonjwa huo
unasababishwa na vimelea vinavyotokana na mbu na kuzingatia umezaji wa
dawa hizo.
Dkt. Ndugulile
amesema kuwa katika kuhakikisha wanapambana kutokomeza ugonjwa huo
Serikali kwa kushirikiana na Kampuni ya Utafiti ya uchimbani mafuta na
gesi ya Statoil wamepata fedha za kuwafanyia upasuaji wagonjwa 200 wa
mabusha na ngirikokoto kwa awamu ya kwanza ya mwaka 2017 na wagonjwa 200
kwa awamu ya pili ya mwaka 2018.
Mbali
na hayo Dkt. Ndugulile amesema kuwa wananchi wa Lindi wanatakiwa kutoa
taarifa sehemu husika pindi wanapoambiwa kuwa dawa muhimu hakuna kwenye
vituo vya afya vya Serikali kwani dawa hizo zipo kwa asilimia 90 Mkoani
humo.
Kwa upande wake
Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi Bw. Ramadhani Kaswa amesema kuwa umezajii
wa kingatiba ya magonjwa hayo umefikia asilimia 70 kwa mwaka 2016/2017.
Aidha,
Bw. Kaswa amesema kuwa kutokana na zoezi la kuwatambua wagonjwa wenye
mabusha na ngirikokoto wamejiandikisha wagonjwa 1294 kwa mkoa wa Lindi
ikiwemo Manispaa ya Lindi wagonjwa 67,Wilaya ya Nachingwea wagonjwa
101,Halmashauri ya Lindi wagonjwa 633, Wilaya ya Liwale wagonjwa 387 na
Wilaya ya Luongo wagonjwa 106.
Uzinduzi
huo uliambatana na zoezi la kumeza Kingatiba za magonjwa yaliyokuwa
hayapewi kipaumbele ikiwemo mabusha na matende,usubi,minyoo,trakoma( vikope) na vichocho.
0 on: "LINDI WATAKIWA KUSHIRIKI KATIKA ZOEZI LA UMEZAJI KINGATIBA YA MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE, ASEMA DKT. FAUSTINE NDUGULILE "