Watumishi wa Wizara ya Afya wakiongozwa na Mkurugenzi wa
kituo cha Lishe na Chakula Wizara ya Afya
Dkt. Vicent Assey (aliyevaa tisheti ya bluu) mapema leo katika matembezi
ya Siku ya Kisukari Duniani yaliyoanza chuo cha Muhimbili mpaka Viwanja vya
Mnazi mmoja.
Watumishi na Wadau
mbali mbali wa masuala ya Afya wakinyoosha viungo baada ya matembezi yaliyo
anzia Chuo cha Muhimbili na kukomea viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es
salaam katika maazimisho ya siku ya Kisukari Duniani huku kauli mbiu ikiwa ni Wanawake na Kisukari.
Kaimu Mkurugenzi wa Elimu ya Afya kwa Umma (HEU) Said Makora
(wakushoto) akimsikiliza Mkurugenzi
msaidizi wa NCD Wizara ya Afya Dkt. Sara Maongezi wakati wa maazimisho ya siku
ya Kisukari Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi wa kituo cha Lishe na Chakula Wizara ya Afya Dkt. Vicent Assey akitoa neon mbele ya wadau
wa Afya na Ugonjwa wa Kisukari (Hawapo kwenye picha) wakati wa maazimisho ya
siku ya Kisukari Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini
Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kinga
Dkt. Neema Rusibamayira ambae alimwakilisha mgeni rasmi Mh. Ummy Mwalimu
akisoma taarifa mbele ya wadau wa Afya na Kisukari nchini (hawapo kwenye picha)
katika maazimisho ya Siku ya Kisukari
Duniani ambayo kikomo chake ni Novemba 14. Wakwanza kushoto ni Dkt Waane na wa mwisho ni
Mkurugenzi msaidizi wa NCD Wizara ya Afya Dkt. Sara Maongezi.
Picha ya pamoja ikiongozwa na Mkurugenzi wa Kinga Dkt. Neema Rusibamayira katika maazimisho ya Siku ya Kisukari Duniani
yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Wadau wa Afya na Kisukari katika matembezi ya Siku ya ugonjwa wa Kisukari Duniani yaliyoanzia Chuo cha Muhimbili na kukomea katika viwanjwa vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam mapema leo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 on: "MATEMBEZI YA SIKU YA UGONJWA WA KISUKARI DUNIANI."