Na WAMJWW
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, wazee na Watoto yauomba ugeni wa Viongozi wa masuala ya Tiba Asili na
Tiba Mbadala kutoka China kuisaidia kujenga kituo cha uendeshaji wa Tiba Asili
ambacho kitakuwa kinatoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi, utafiti wa kina na kuwa
na eneo la kumbu kumbu la kutunza miti dawa.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa
Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya mapema leo wakati apokea ugeni wa Viongozi
wa masuala ya Tiba Asili na Tiba Mbadala kutoka China uliofika nchini tangu
Novemba 12, huku ugeni huo ukitarajia kuwepo nchini mpaka Novemba 16.
Pia Dkt. Mpoki ameuomba ugeni huo kuwekeza
zaidi katika uanzishwaji wa viwanda vya kuzalisha Dawa, sambamba na kuiruhusu
Tanzania kuuza Dawa zake za Asili katika nchi ya China jambo litalosaidia Tanzania kuwa na mashamba
makubwa ya kuzalisha Dawa.
Nae Mganga Mkuu wa Serikali Prof.
Mohhamad Bakar Kambi ameahidi kushirikiana bega kwa bega na jopo la uongozi huo
hususani katika kuboresha huduma za Afya nchini , huku akitia mkazo kuimarisha
zaidi ushirikiano katika kufanya tafiti na kubadilishana ujuzi kupitia mafunzo.
Nae kaimu Mkurugenzi msaidizi wa Tiba
Asili na Tiba Mbadala Dkt. Peter Mhane amefurahishwa na ujio wa huo huku
akiamini kwamba ushirikiano huu ni faida kwa nchi ya Tanzania kwani itasidia kuondokana
na umasikini na kuondokana na upungufu wa Dawa.
0 on: "WIZARA YA AFYA YAUOMBA UONGOZI WA TIBA ASILI KUTOKA CHINA KUISAIDIA KUJENGA KITUO CHA UENDESHAJI WA TIBA ASILI."