Dkt.Ndugulile akimkabidhi Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu
Dkt.Furaha Mwakafyila Ngao baada ya kuibuka mshindi wa Huduma za afya
katika vituo vya afya.
Afisa Tawala wa Wilaya ya Nanyumbu Salumu Palango akimpongeza Kaimu Mganga Mkuu wake baada ya kupokea ngao.
Mkurugenzi wa Idara ya Ubora na Uhakiki wa Huduma za Afya toka Wizara ya
Afya Dkt.Mohamed Mohamed akielezea tathimini ilivyofanyika katika Mkoa
huo mwaka 2016 na Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu Kuibuka mshindi kwa
kupata ngao na cheti.
Mkuu wa Wilaya MHE.Evod Mmanda akiongea wakati wa mkutano huo.
Naibu Waziri Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine
Ndugulile(katikati)akiongea na Viongozi na Watendaji wa Afya Afya Mkoa
na Wilaya ya Mtwara wakati wa zoezi la kutoa ngao na vyeti kwa vituo
vya afya vilivyo na ubora wa huduma za afya.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya
Mtwara Mhe.Evod Mmanda na kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt.Wedson
Sichalwe.
Naibu Waziri akimpongeza Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu baada
ya kuibuka mshindi.Dkt.Ndugulile aliipongeza Wilaya hiyo kwa mpangilio
mzuri wa utoaji huduma pamoja na utunzaji wa kumbukumbu kwenye stoo ya
dawa katika kituo cha afya cha Mtambaswala ambacho kimeanza miezi miwili
iliyopita lakini kimeonyesha ufanisi wa hali ya juu.
Picha ya pamoja mara baada ya Naibu Waziri kutoa ngao na vyeti kwa washindi kwa Mkoa wa Mtwara.
Dkt.Ndugulile akisoma taarifa ya dawa katika Zahanati ya Ziwani iliyopo
Manispaa ya Mtwara,ambapo Naibu Waziri huyo alichukizwa hali ya
miundombinu na uwajibikaji wa Zahanati hiyo na kuwapa miezi miwili wawe
wamefanya marekebisho kama walivyoelekezwa.
Na.WAMJW,Mtwara
Serikali
inatarajia kutoa leseni kwa hospitali na vituo vya afya vya Umma
vitakavyokidhi vigezo vya ubora wa kutoa huduma za afya ili mwananchi
wajue kituo atakachoenda kina ubora gani wa huduma hivyo nchini
Hayo
yamesemwa jana na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee
na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile wakati akiongea na Viongozi na
Watendaji wa afya wa Mkoa na Wilaya zake kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu
wa Mkoa wa Mtwara wakati wa zoezi la kutoa ngao kwa wilaya iliyofanya
vizuri na vituo vya afya vilivyofanya vizuri wakati wa zoezi la
tathimini ya kutoa nyota kwa vituo vya kutolea huduma za afya.
Dkt.Ndugulile
alisema hivi sasa serikali inasisitiza kuweka ubora wa huduma za afya
katika vituo vyote vya afya vya umma ili kukidhi ubora unaotakiwa wa
kutoa huduma kwa wananchi”tunakwenda mbali zaidi usipokuwa na vigezo
hospitali yako na kituo chako hutopewa leseni”
Hata
hivyo amewataka wale wote waliopewa maelekezo ya nini wafanye basi
viongozi wawajibike kwa kurekebisha changamoto zilizopo na wasingoje
idara ya uhakiki ubora kutoka wizarani waje kukagua kwani Lengo
liliowekwa na wizara ni kila kituo cha afya kupata nyota tatu hadi
kufikia mwezi juni mwakani.
“Nyinyi
wengine wote hamkustahili kupata cheti hata kimoja hapa,Mkoa wa Mtwara
asilimia 3 za vituo vyenu vina nyota mbili na asilimia 51 vina nyota
moja na zaidi ya nusu mna nyota 1 na asilimia 46 mna nyota sifuri hali
ya utoa huduma bado”Nimetoka hapo zahanati ya Ziwani,kwakweli
hapana,ubora wa kutoa huduma pale hapana wakati mpo mjini.
Kwa
upande mwingine amewataka kamati za afya ngazi ya Mkoa na Wilaya
kufanya kazi na kusimamia katika kuyafanyia kazi maelekezo yote
waliyopatiwa kwani maboresho mengine hayahitaji fedha hivyo kamati hizo
zitimize wajibu wao”Niwaombe mbadilike kwani mambo madogo madogo
yatakuja kuwagharimu hivyo msimamie hali ya utoaji wa ubora na huduma za
afya kwa mkoa wa mtwara ni mbaya,nikirudi wakati mwingine sitoongea
kirafiki hivi”alisisitiza
Aidha,aliwataka
watendaji hao kubadilika katika utendaji wao na hivyo kusimamia
upatikanaji wa dawa katika vituo vyao vya afya ili kusiwepo na
malalamiko kutoka kwa wananchi kwamba wamekosa dawa
“Dhama
imebadilika,hivyo kila mmoja awajibike,awamu hii ni nyingine,hatutaki
kusikia dawa hakuna na mwananchi analalamika amekosa dawa kwenye kituo
cha afya,Mhe.Rais anaipenda sekta ya afya na ameongeza bajeti ya dawa na
anatoa pesa zote,sitaki kusikia dawa hakuna na Wilaya itakayoshindwa
basi viongozi wake nao hawatoshi”aliongeza Naibu Waziri
Naye
Mkurugenzi wa Idara ya Uhakiki Ubora toka Wizara ya afya Dkt. Mohamed
Mohamed alisema wizara ilingia kwenye mpango wa kuboresha huduma kwenye
vituo vinavyotoa huduma za afya ya Msingi mwaka 2014 kwa kuhusisha
kufanya tathimini vituo vyote vya afya nchini na kuvipa kategoria ya
nyota moja hadi tano ikiwemo wa kuandaa mipango ya kuimarisha ubora
katika vituo hivyo.
"Tathimini ya awali ilifanyika katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya ya msingi nchini mwaka Aprili,2015 na Desemba 2016"
Alitaja maeneo yaliyoangaliwa na kufanyiwa tathimini ni uendeshaji wa vituo ,utendaji wa wafanyakazi,uwajibikaji, miundombinu ya kituo,mkataba kwa mteja pamoja na mazingira salama ya kutolea huduma na ubora wa huduma wenyewe.
Jumla
ya vituo 6997 vilifanyiwa tathimini nchini na katika Mkoa wa Mtwara
tathimini ya awali ilifanyika mwezi mei 2016 na vituo 221 vilifanyiwa
tathimini na matokeo ya awali yalikua vituo 6 vilipata nyota 2(3%),vituo
112 vilipata nyota 1(51%) na vituo 103 vilipata nyota 0(47%).
Katika
zoezi hilo Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu iliibuka mshindi kwa
kupata ngao,na kituo cha afya Nanyumbu kilipata cheti.Kituo kingine cha
afya kilichopaya cheti ni kituo cha Nagaga cha Masasi pamoja na za
zahanati ya Nanjota na Nambaya zote za Halmashauri ya Masasi zilifanya
vizuri.Pia zahanati ya Shangani ya halmashauri ya Manispaa ya Mtwara
ilipata cheti.
0 on: "SERIKALI YATARAJIA KUTOA RESENI KWA HOSPITALI NA VITUO VYA AFYA VYA UMMA VITAKAVYOKIDHI VIGEZO VYA UBORA."