Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Mkurugenzi wa sera na
mipango,, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ,
akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa TEHAMA kutoka Wizara ya Afya na
Taasisi zake.
Mkuu wa kitengo cha TEHAMA, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, ndugu Hermes S. Rulagirwa, akiwakaribisha Maafisa
TEHAMA kutoka Wizara ya Afya na Taasisi zake.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Mkurugenzi wa sera na mipango, Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (WAMJW),Ndg Edeard
Mbanga Akifungua kikao cha maafisa TEHAMA wa Wizara na Taasisi zake,
kinachopitia utekelezaji wa mpango mkakati wa eHealth Strategy
2013-2018. Kikao hiki kinafanyika katika ukumbi wa LAPF Dodoma.
Na WAMJWW
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto leo imeendelea na utekelezaji wa mkakati wa
matumizi ya TEHAMA katika Sekta ya Afya (Health Strategy 2013-2018) katika ukumbi wa LAPF jijini Dodoma.
Sambamba na hiyo, Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI,
Wakala ya Serikali Mtandao (EGA), imetoa mwongozo unaoelekeza namna bora
ya usimikaji na matumizi ya mifumo ya kielektroniki katika sekta ya
Afya.
Malengo ya kikao kazi hiki ni kuwajengea ufahamu wa pamoja
washiriki juu ya mikakati, sera na miongozo ya TEHAMA iliyopo katika
sekta ya Afya. Vilevile, kupata maendeleo ya mikakati yote ya TEHAMA
kutoka katika Miradi, Taasisi na Hospitali zote zilizopo chini ya Wizara.
Hata hivyo, kikao kazi hiki kinajadili kwa upana mafanikio na
changamoto ya utekelezaji wa mkakati huu wa 2013-2018 ili kuboresha
mkakati mpya wa mwaka 2018-2023.
0 on: "KIKAO KAZI CHA KUJADILI UTEKELEZAJI WA MIKAKATI, SERA NA MIONGOZO YA TEHAMA KATIKA SEKTA YA AFYA CHAENDELEA JIJINI NDODOMA."