Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki
Ulisubisya akipokea vifaa vya kufundishia kutoka kwa Balozi wa Shirikisho la
Jamhuri ya Ujerumani Dr Detlef Wachter
katika maazimisho ya siku ya mtoto njiti duniani inayoazimishwa kila Novemba
17.
Picha
ya pamoja ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya katika maazimisho ya siku ya
mtoto njiti duniani, ambapo shirika la GIZ kutoka Ujerumani lillikabidhi vifaa
vya kufundishia watoa huduma jinsi ya kuwasaidia watoto njiti.
Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Dtk. Wedson Sichalwe akiwasilisha taarifa fupi mbele ya
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Viongozi
na waandishi wa habari(hawapo kwenye picha) katika maazimisho ya siku ya
mtoto njiti duniani.
Meneja
mipango wa Shirika la Giz kutoka Ujerumani
Dkt. Susanne Grimm akielezea baadhi ya mafanikio na mipango ya Shirika
hilo wakati wakitoa msaada wa vifaa vya kufundishia watoa huduma jinsi ya
kuwasaidia watoto njiti.
Balozi
wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Dr
Detlef Wachter akitoa taarifa mbele ya mgeni rasmi na waandishi wa habari
wakati wa utoaji msaada uliofanywa na
shirika la Giz katika Taasisi ya Saratani Ocean road jijini Dar es salaam,
mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mpoki
Ulisubisya akimpa mkono wa shukurani
Balozi wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Dr Detlef Wachter baada ya kupokea msaada wa
vifaa vya kufundishia watoa huduma jinsi ya kuwasaidia watoto njiti.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mpoki
Ulisubisya akifungua mkutano katika maazimisho ya siku ya mtoto njiti duniani,
ambapo shirika la GIZ kutoka Ujerumani lillikabidhi vifaa vya kufundishia watoa
huduma jinsi ya kuwasaidia watoto njiti.
Na WAMJWW
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imepokea msaada wa
vifaa vya kufundishia watoa huduma kwa watoto njiti vyenye thamani ya shilingi
milioni 22. 19 kutoka shirika lisilo la kiserikali GIZ la Ujerumani ili kuweza
kutoa huduma bora katika kuwakuza watoto
hao kwa uangalifu wa hali ya juu na kwenye mazingira mazuri.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya mtoto
njiti duniani yaliyofanyika katika Taasisi ya Saratani Ocean Road Katibu Mkuu
wa Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema msaada wa vifaa hivyo
utaboresha huduma kwa watoto njiti.
“Kutokana na msaada wa vifaa hivyo naamini rufaa
zitapungua kwa kiasi kikubwa na kufanya huduma hizo kutolewa kwenye zahanati
zitazopelekewa vifaa hivyo “ alisema Dkt. Ulisubisya.
Aidha Dkt. Ulisubisya amesema kuwa watumishi wa
afya ambao wamepata mafunzo wanatakiwa kuwaangalia wamama wanaotaka kujifungua
ili kuweza kupunguza vifo vya wamama wajawazito na watoto nchini.
Mbali na hayo Dkt. Ulisubisya amesema kuwa wamama
wajawazito wanatakiwa kuhudhuria kliniki mara kwa mara pindi wanapopata
ujauzito ili kuweza kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya ili kuepuka
kuzaa watoto njiti.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Dkt.
Wedson Sichalwe amesema kuwa anashukuru Shirika la GIZ kwa mafunzo pamoja na
vifaa vya kutolea huduma kwa watoto njiti katika mkoa wake ili kutoa huduma
bora kwa watoto hao.
“Tumepata msaada mkubwa sana kwa mkoa wetu kwani
tulikua tunakabiliwa na changamoto za vifaa vya vya kuhudumia watoto njiti
wanaozaliwa katika zahanati na hospitali mkoani kwetu” alisema Dkt. Sichalwe.
0 on: "SERIKALI YAPOKEA MSAADA WA VIFAA VYA KUFUNDISHIA WATOA HUDUMA ZA WATOTO NJITI NA WAMJW-DAR ES SALAAM"