JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA
WIZARA YA AFYA,
MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
TANGAZO LA KUITWA KAZINI.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto ilipokea kibali cha kuajiri watumishi 3,152 wa kada mbalimbali
za Afya nchini. Kibali hiki kilikuwa kwa
ajili ya Wizara, Hospitali za Mikoa, Halmashauri na Taasisi mbalimbali. Maombi yalipokelewa kuanzia
tarehe 25/07/2017 hadi 31/08/2017.
Waombaji thelathini
(30) wamechaguliwa na kupangiwa ajira Wizara ya Afya kama jedwali linavyoonesha
kwenye Tovuti ya Wizara ya Afya, ili kuona majina ya waliochaguliwa ingia www.moh.go.tz
Waombaji 2,058 waliochaguliwa
katika Hospitali za Mikoa na Halmashauri wametangazwa kwenye Tovuti ya OR TAMISEMI. Waombaji wote
wanajulishwa kutembelea Tovuti hiyo www.tamisemi.go.tz. Aidha, Sekretarieti
ya Ajira inaendelea kushughulikia ajira kwa Taasisi nyingine.
Waombaji
wote waliochaguliwa wanatakiwa kuzingatia kwa
ukamilifu maelekezo yafuatayo:-
i)
Kuripoti
Ofisi za Wizara ya Afya Dodoma
katika muda wa siku kumi na nne (14)
kuanzia tarehe ya tangazo hili kwa ajili ya kukamilisha taratibu za ajira
Serikalini. Ofisi za Wizara ya Afya zipo
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Kitivo cha
Sanaa na Sayansi ya Maendeleo ya Jamii, Jengo namba 11.
ii)
Ambao
hawataripoti ndani ya siku kumi na nne
(14) nafasi zao zitajazwa na waombaji wengine wenye sifa.
iii)
Wakati
wa kuripoti kila aliyechaguliwa atapaswa kuwasilisha vyeti halisi (original Certificates) ambavyo nakala zake
zilitumiwa wakati wa kuombea ajira zao.
Hii ni pamoja na Vyeti halisi vya Elimu,
vyeti vya Taaluma, Leseni kulingana na sifa za kada zao.
iv)
Awe
na Cheti halisi cha Kuzaliwa (Original
Birth Certificate) ambacho nakala yake aliambatisha kwenye maombi
aliyowasilisha.
v)
Mwombaji
anatakiwa kuwa na picha mbili ndogo
(passport size). Picha ziwe na muonekano kamili wa sura na ziwe zimepigwa si
zaidi ya miezi mitatu.
Imetolewa na:-
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Afya
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto.
0 on: "TANGAZO LA KUITWA KAZINI."