Na.WAMJW,Ruangwa
Wizara
ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto inatarajia kutoa
mwongozo wa utoaji tiba kwenye hospitali zote nchini ili kuwe na mfumo
mzuri wa dawa muhimu ili kuepusha madaktari kuagiza dawa ambazo zipo
nje ya mfumo wa dawa muhimu.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa
Afya Dkt.Faustine Ndugulile wakati wa ziara yake ya kuangalia hali ya
upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vya
Serikali
“Kabla ya mwisho wa mwaka tunataka kutoa muongozo
huo(Standard Treatment Guidline) kwa sababu imekua changamoto kwani
wale wauzaji wakubwa wa dawa wamekua wakizitembelea hospitali kubwa na
kuwarubuni wanunue dawa zao ambazo zipo nje ya dawa zetu muhimu”
Kwahiyo
muongozo huo itakua kila ugonjwa dawa ya kwanza itakua ipi na kama
itashindika dawa itakayofuata dawa ipo na hizo dawa zitaagizwa na
kutunzwa na Bohari ya Dawa(MSD)
Hata hivyo Dkt.Ndugulile
amewataka watendaji wa hospitali hiyo kuweka utaratibu na mpangilio
mzuri na unaohitajikwa wa utunzaji wa dawa kwenye stoo ya madawa
iliyopo hospitalini hapo,baada ya kukuta hakuna upangaji mzuri wa dawa
na vifaa tiba
“mmenithibitishia kwamba dawa zote mnazipata kwa
asilimia 90 hivyo ni vyema Mfamasia wa Wilaya kuzipanga dawa hizo
vizuri na kuweka kiyoyozi ambacho kitasaidia kutunza dawa kwa muda bila
kuharibika”
Alisema hivi sasa nchi haina tatizo la
upatikanaji wa dawa kwani bajeti ya dawa hivi sasa imeongezeka kutoka
shilingi bilioni 30 mpaka zaidi ya bilioni 260 kwa mwaka huu wa fedha
“bajeti hii imekua ikitolewa na Mhe.Rais amekua akizitoa fedha
zote,hivyo hatuna shida ya fedha hivyo nasi hatutarajii kuwa na shida ya
dawa na dawa tunazokuwa tunazipata zitunzwe vizuri”
Aidha,amezitaka
kamati za afya katika ngazi za zahanati,vituo vya afya na hospitali
zinafanya kazi ipasavyo kwa kusimamia matumizi mazuri ya dawa
Kwa
upande wa ubora wa huduma za afya kwa vituo vya kutolea huduma za afya
vya serikali hivyo kumekua na mkakati wa kuwa na ubora wa vituo vya
serikali kwa kuwapatia nyota kulingana na ubora uliopo kwenye vituo kwa
kuangalia utoaji wa huduma,maabara na sehemu zingine za kutolea huduma
Kwa
upande wa Mfuko wa afya wa jamii(CHF) Dkt.Ndugulile amewapongeza wilaya
hiyo kwa kusajili kaya 13,788 kutoka 978 mwaka 2016/2017,ambapo
wamewapatia vitambulishovya matibabu wazee 4,000.
“hivi sasa
Serikali inataka kuwa na bima kwa wote kwani gharama ya matibabu kwa
sasa ni kubwa sana hasa na kumekua na ongezeko la magonjwa yasiyo ya
kuambukizwa,hivyo tunataka kuwasaidia wananchi ambao hawawezi kumudu
gharama hizo ili anavyokwenda kwenye vituo vyetu asiwaze masuala ya
kutoa fedha”alisema Dkt.Ndugulile.
Akisoma ripoti ya Wilaya
hiyo Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt. Ernest Ntahuka Alisema
Halmashauri hiyo imeweza kuboresha hali ya upatikanaji wa dawa kwa
asilimia 85 kutoka asilimia 60 ya mwaka 2015/2016
Hata hivyo
alisema Halmshauri ya Ruangwa kwa mwaka 2017/2017 imetenga shilingi
milioni 650 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali mpya ya wilaya na tayari
imeshatenga eneo la ujenzi lenye ukubwa wa hekari 60 ambapo ramani ya
ujenzi huo tayari imeandaliwa
0 on: "SERIKALI KUTOA MUONGOZO WA UTOAJI TIBA KWA HOSPITALI ZOTE"