Serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki na wezeshi
kwa wadau wa maendeleo nchini wanaotaka kuwekeza kwenye sekta ya Afya.
Hayo yamesemwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan wakati wa Matembezi ya Hisani yenye lengo la
kukusanya Fedha zitakazo saidia kugharamia mafunzo ya uuguzi na ukunga katika
viwanja vya Green ground jijini Dar es salaam.
Mh. Samia Suluhu amesema Serikali imekwisha weka mikakati
thabiti ikiwemo kuongeza viwanda vya kutengeneza Dawa na Vifaa tiba ili
kuongeza upatikanaji na uboreshaji wa huduma muhimu za Afya kwa binadamu.
“Waziri wa Afya muongeze jitihada za kupunguza vifo
vitokanavyo na uzazi kwa kina mama, mfanye tafiti na mchunguze kifo chochote
cha mama na mtoto wakati wa kujifungua”
Aidha, Makamu wa Rais alitaka kila kifo cha mama wakati
wakujifungua lazima kijadiliwe vizuri na ikionekana kama kulikuwa na uzembe
hatua zichukuliwe kama itakavyostahili.
Awali akimkaribisha Makamu wa Rais, Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alisema katika
kuimarisha uzazi salama kwa kina mama, upatikanaji wa dawa zote za uzazi salama
umeimarika na zinapatikana kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vya
Serikali.
“Hivi sasa ukipita katika vituo vyetu vya Afya vya
Serikali angalau utakuta dawa zote muhimu tunashukuru kwa kazi
kubwa unayofanya ya kuzungumzia umuhimu wa kuboresha huduma za Afya
nchini.
Katika matembezi yaliyofanyika mwaka jana shilingi
Bilioni 290 zilikusanywa na kuwekwa kwenye fungu la kusomesha wakunga 75
kwa ngazi ya cheti.
0 on: "SERIKALI ITAENDELEA KUWEKA MAZINGIRA RAFIKI KWA WANAOTAKA KUWEKEZA KWENYE SEKTA YA AFYA,"